KUMWAIBISHA MWENYE KOSA SI TABIA YA MWENYE HAKI
KUMWAIBISHA MWENYE KOSA SI TABIA YA MWENYE HAKI Na: Min. Sudai. Bwana asifiwe wana wa Mungu. Karibu tujifunze jambo fulani la mtu mwenye haki. Ni kweli kwamba kila mtu aliyeokoka au anayesali hujisema au hujihesabu kuwa ni mwenye haki, lakini si wote ni wenye haki, kwasababu kuwa mwenye haki haina mahusiano na unavyojiona bali kuwa na sifa za mwenye haki ambayo baadhi yake tunaiangalia hapa leo... Tunajifunza kupitia Yusufu mume wa mariamu mama wa Yesu.. Soma hapa👇 Mathayo 1:18-19 [18]Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. [19]Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri. Kilichomfanya Yusufu atake kumwacha mariam ni kwasababu aligundua kuwa mariamu ana mimba.. na kilichomfanya atake kumwacha kwa siri ni kwasababu hakutaka kumwaibisha na hakutaka kumwaibisha kwasababu Yusufu alikuwa ...