ATAKULETA HUKUMUNI

                

       

                                      ATAKULETA HUKUMUNI

Bwana asifiwe wana wa Mungu, njoo tujifunze tena

Ni dhahiri katika maisha haya watu wa rika zote hususani vijana na watu wazima, wana mambo yao na shughuli zao ambazo hupenda kuzifanya za kuwafurahisha mioyo yao hapa duniani


Hebu tusome hapa👇

Mhubiri 11:9-10
[10]Kwa hiyo ondoa majonzi moyoni mwako, nawe uuondoe ubaya mwilini mwako; kwa maana ujana ni ubatili, na utu uzima pia. 
[9]Wewe kijana, uufurahie ujana wako, na moyo wako ukuchangamshe siku za ujana wako, ukaziendee njia za moyo wako, na katika maono ya macho yako, lakini ujue wewe ya kwamba kwa ajili ya hayo yote Mungu atakuleta hukumuni. 

Hapo biblia inazungumza na watu wawili kwasababu kwa asilimia kubwa watu hawa ndio Taifa la sasa yaani vijana na watu wazima..

Sasa kijana ni mtu anaishi katika ulimwengu wa ujana, n mtu mzima pia katika ulimwengu wa utu uzima ambapo sehemu zote Kuna mambo yao na viburudisho vyao ambavyo hufarahisha mioyo yao..

Lakini Mungu Kuna kitu cha kutisha amekisema hapo... Amesema hivi UJANA NA UTU UZIMA NI UBATILI...

Kama ujana na utu uzima ni ulimwengu au hatua ambazo watu hhuzipitia, na hatua hizo au maeneo hayo ni UBATILI, hii inamaanisha kuwa mtu anapofika katika hatua hizo moyo wake unajazwa mambo ya eneo hilo yaani mambo ya ujana au utu uzima ambapo mambo hayo ni UBATILI.. Kumbe katika hatua hiyo mtu hatakiwi kufuata mambo ya moyo wake bali afuate mambo na maneno ya Bwana... Kwasababu kwa hayo na hizi hatua Mungu huwahukumu watu...

Na ndiyo maana akasema hukatazwi kujifurahisha, au kutufurahisha moyo uwapo kwenye ujana au utu uzima lakini ujue na ukumbuke na uwe na hakika Moyoni mwako kwamba kwa hayo yote Mungu atakuhukumu.. Yaani Mungu atahukumu kwa kutazama kile utendacho...

Kumbe kila unachokiita starehe na burudani za ujanani ni UBATILI hivyo kuwa makini, acha kufuata moyo bali fuata neno la Mungu

Biblia imeongea kwa njia ya tofauti sana kwenye eneo hili... Anawaruhusu watu waziendee njia za mioyo yao na kujifurahisha lakini katika yote wajue Bwana atawaleta HUKUMUNI katika hayo...

Na ndiyo maana Mungu akasema jinsi ambavyo mtu anatakiwa kuifuata njia iliyonyooka.. 

Zaburi 119:9
[9]Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. 

Je wewe unaifuta njia gani?? Ni njia ya moyo wako au njia ya Mungu?? Basi ifuate njia ya Mungu ili uwe salama kwenye maisha ya sasa na ya milele..

Mungu akubariki sana

@Taifa Teule Ministry
Minister Mathayo Sudai 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?