MALI vs MOYO
MALI vs MOYO
Bwana asifiwe wana wa Mungu...
Leo naomba tujifunze mambo machache hapa kuhusu utoaji na jinsi jambo hilo lililivyo na Mahusiano mbele za Mungu...
Nitatumia vifungu hivi👇
Mathayo 6:19-21
[19]Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba;
[20]bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi;
[21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Mithali 3:9-10
[9]Mheshimu BWANA kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
[10]Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi,
Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
Mathayo 15:7-8
[7]Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
[8]Watu hawa huniheshimu kwa midomo;
Ila mioyo yao iko mbali nami.
Karibu tujifunze
Ukiangalia hapo kwenye MATHAYO 6:19-21 kuna jambo tunaliona kuhusu hazina.....
hazina ni kitu cha thamani alichonacho mwanadamu ambacho ndicho kinachompa heshima kimaisha na hukilinda kitu hicho kwa hali zote kwani kikipotea basi thamani ya maisha ya huyo mtu inapotea pia.
sasa katika maisha, Yesu alitufundisha kwamba hazina hutunzwa katika maeneo mabalimbali kwa matumizi ya baadae, na akaonyesha kwamba hazina inaweza kuwekwa duniani na pia inaweza kuwekwa mbinguni.. lakini katika kuitunza hazina ili iwe na maana kwa maisha yajayo au ya kesho yako, akasema USIWEKE hazina duniani.
ukiangalia maneno hayo utagundua kwamba Yesu hakutoa ushauri kwa watu bali aliwapa njia sahihi na salama na kuonyesha kabisa kwamba ikiwa utajiwekea hazina duniani basi ufahamu kwamba hazina hiyo haitakuwa na msaada kesho au kwa maisha ya baadae kwasababu duniani kuna aina nyingi za uharibufu na hakuna usalama katika kutunza hazina zako.
lakini si hivyo tu, akasema pia hazina ya mtu hufungamana au kuambatana na moyo wa mtu, (kumbuka hazina ni kitu kinachothaminiwa na mtu au moyo wa mtu ), hivyo pale unapoiweka hazina yako hapohapo ndipo moyo wako unakuwepo.. japo kuna watu wanasema mioyo yao iko kwa Mungu au mbinguni na huku hazina zao zimeng'ang'ania duniani, lakini maandiko matakatifu yanapingana na madai yao. maandiko yanasema ilipo hazina yako na moyo wako utakuwa hapohapo.
sasa fahamu kwamba katika dunia hii ya mwili, mali, pesa tulizonazo ni moja ya hazina ambazo Mungu ametubariki kuwa nazo na Mungu anatupa hizo ili tuzitumie lakini pia tuweke akiba kwa maisha yajayo. kumbuka ni mwanadamu mpumbavu tu ndiye hajui kwamba kuna maisha ya baadae lakini ukiwa mwerevu basi utaungana na Yesu kusema kwamba baada ya maisha haya, kuna maisha mengine ya baadae ambapo hazina zetu zinatakiwa kuhifadhiwa kwaajili ya maisha hayo.
sasa ikiwa mali na pesa zetu ni hazina katika maisha ya sasa tunaouhuru kuchakuwa kihifadhi wapi hizo hazina zetu lakini Yesu alisema kuna maghala mawili tu ya kuhifadhi hazina hizo yaani duniani na mbinguni.
kwahiyo twaweza sema mioyo ya watu huambatana na mali zao. na kila mahali ambapo hazina ya mtu itakwenda basi hapohapo utaukuta moyo wa huyo mtu.
sasa unaweza kuungana na mimi kwamba Mungu anasema hivi... MPENDE/MHESHIMU BWANA MUNGU WAKO KWA MOYO WAKO WOTE, AKILI YAKO YOTE NA KWA NGUVU ZAKO ZOTE....... nadhani maandiko hayo si mageni kwetu.
kumbe Mungu anapenda kuheshimiwa au kupendwa kwa mioyo yetu yote...!!!!!!!
lakini kumbuka mioyo yetu huambatana na hazina zetu, na anasema ulipo moyo wa mtu hapohapo ndipo ilipo hazina yake.
hivyo kumheshimu Mungu kwa mioyo yetu kunahusisha kumuheshimu kwa hazina zetu pia. na moja ya hazina zetu leo hii ni pesa na mali tulizonazo. Na ndiyo maana kwenye Mithali kuna kitu anakisema hapo kwamba
Mithali 3:9-10
[9]Mheshimu BWANA kwa mali yako,
Na kwa malimbuko ya mazao yako yote.
[10]Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi,
Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya.
Maandiko hayo yanaonyesha jinsi ambavyo hazina zetu zikiambatana na mioyo yetu zinavyompendeza Mungu hata kuendelea kutujazia GHALA ZETU
KUMBUKA
GHALA ni sehemu hazina zetu zinapohifadhiwa. sasa kumbe ili Mungu azijaze ghala zetu basi yafaa kwanza kumheshimu yeye kwa mioyo yetu yote. ambapo tukimuheshimu kwa mioyo yetu basi tunaweza kumuheshimu kwa mali na pesa zetu kwasababu ilipo hazina ya mtu ndipo na moyo wa mtu ulipo.
kwahiyo kumbe unaweza kujua moyo wa mtu kwamba unamuheshimu Mungu au la! kwa kuangalia jinsi mtu huyo anavyoenenda mbele za Mungu kwa mali na pesa zake. kwasababu tumeona vitu hivyo huambatana na mioyo ya wanadamu
Mali zako zisihusike katika kufanya kazi ya udhalimu na ya uovu bali zitumike sawasawa na mapenzi na makusudio ya Mungu kukupa mali hizo.
lakini pia anaongelea kuhusu MALIMBUKO.
kutokutoa malimbuko si tu kunakufanya wewe kutokuwa mtii mbele za Mungu bali kunaonyesha sura yako halisi ya namna unavyomuheshimu Mungu au la!.
kwahiyo usihangaike kujionyesha kwa watu kwamba wewe ni mtu wa Mungu au unamuheshimu Mungu kwa jinsi unvyonena kwa lugha au jinsi unavyohudhuria kanisani na vipindi vya maombi, na huku mali zako na malimbuko yako yako mbali na huyo Mungu kwani kwa kufanya hivyo MOYO Wako unakuwa umejionyesha uliopo yaani palipo na hazina ako ndipo na moyo wako utakuwepo.
Unajua kwenda kwenye maombi pamoja na kunena kwa lugha si vitu vinavyompa Mungu utukufu kwasababu waweza kuwa unafanya hivyo kwasababu unataka Mungu akufanyie mambo yako kisha upotee mitini, lakini habari njema ni kwamba Mungu huangalia MATUNDA (Yohana 15) ambapo matunda hayawezi kuwa kwenye maisha ya mtu bila kuwa na utii wa neno la Mungu...
Kipengele hiki kukusaidie kujua kuwa makanisa mengi sikuhizi yamejaa watu ambao kimsingi wanasema kwa vinywa vyao kwamba wanampenda na kumuheshimu Mungu lAKINI mioyo yao hawa watu iko mbali sana na huyo Mungu. na wengine wamewekwa mbali na Mungu kwasababu tu ya mali zao. walipoweka pesa zao,na mali zao mbali na Mungu ghafla na mioyo yao ikiwa mbali na Mungu kwasababu ilipo hazina yako moyo wako ndipo ulipo.
kwahiyo unaweza kuingia kanisani kukutaa na Mungu lakini moyo wako umeuacha nje. upo kwenye mali zako huko nje, na hilo ndilo linaloendelea kwa baadhi ya tulio wengi. tunampenda Mungu kwa midomo ila mioyo iko nje mabli kabisa kwenye mali zetu na pesa zetu... na Mungu anapotuona tunamfuata angali tumeiacha mioyo yetu mbali hapendezwi na sisi na anatuona kuwa ni wanafiki... na ndiyo maana akasema kwenye Mathayo pale kwamba;
Mathayo 15:7-8
[7]Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema,
[8]Watu hawa huniheshimu kwa midomo;
Ila mioyo yao iko mbali nami.
Kwenye Biblia kuna mtu fulani alitaka kumfuata Yesu kama vile sisi tunavyotaka, lakini Yesu akamwambia unazijua amari za MUNGU, yule mtu akasema anazijua na amezishika tokea utotoni mwake, basi Yesu akamwambia NENDA KAUZE MALI ZAKO ZOTE KISHA NJOO UNIFUATE, yule mtu alichukia sana na nadhani aliona kumfuata Yesu haina maana yoyote ile...
unajua ni kwanini?
ni hivi... yule mtu alichukia kwasababu Yesu alijua kwamba yule mtu hakuwa anampenda wala kumheshimu kwa moyo wake bali alitaka kumfuata tu ilimradi naye aonekane pamoja na mtu mahiri, mzuri, shujaa Yesu lakini hakuwa na dhamiri haya ya kumfuata Yesu kwa moyo wake. na ndiyo maana ilipoguswa hazina yake ulipo moyo wake aligeuka kuwa mbogo.
unajifunza nini hapo?..... Kumbe hata sisi tunaweza kumfuata Yesu ili tuonekane kuwa ni watumishi wa Mungu tu lakini hatuna maana ya kumfuata kwa mioyo yetu. na hii inadhihirishwa na jinsi tunavyoweka mali zetu na pesa zetu mbali na Yesu bila kujua tunaiweka mioyo yetu mbali na yeye.
hivyo wapendwa katika Bwana naomba kuwakumbusha kuhusu kumuheshimu Mungu wetu kwa mali zetu na kwa MALIMBUKO YETU ili kuonyesha heshima kwa mioyo yetu mbele za Mungu na KUFANYA baraka za Bwana ziwe pamoja na ghala zetu.
Mtolee Mungu sadaka kwa mali na pesa zako na pia Kila mwezi wa kwanza wa Mwaka jitahidi kuusukuma moyo wako umfuate Yesu kwa kujitahidi kumpa Mungu malimbuko yako na baada ya hapo uwe na uhakika kwamba mwaka wako wote utabarikiwa katika ghala zako.
Mungu awabariki sana
Taifa Teule Ministry
Min. Mathayo Sudai.

Maoni
Chapisha Maoni