MALI vs MOYO
MALI vs MOYO Bwana asifiwe wana wa Mungu... Leo naomba tujifunze mambo machache hapa kuhusu utoaji na jinsi jambo hilo lililivyo na Mahusiano mbele za Mungu... Nitatumia vifungu hivi👇 Mathayo 6:19-21 [19]Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; [20]bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; [21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. Mithali 3:9-10 [9]Mheshimu BWANA kwa mali yako, Na kwa malimbuko ya mazao yako yote. [10]Ndipo ghala zako zitakapojazwa kwa wingi, Na mashinikizo yako yatafurika divai mpya. Mathayo 15:7-8 [7]Enyi wanafiki, ni vema alivyotabiri Isaya kwa habari zenu, akisema, [8]Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami. Karibu tujifunze Ukiangalia hapo kwenye MATHAYO 6:19-21 kuna jambo tunaliona kuhusu hazina....