MSAADA WETU U KATIKA JINA LA BWANA MUNGU WA MAJESHI
MSAADA WETU U KATIKA JINA LA BWANA MUNGU WA MAJESHI
Zaburi 124:6-8
Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao.
[7]Nafsi yetu imeokoka kama ndege
Katika mtego wa wawindaji,
Mtego umevunjika, nasi tumeokoka.
[8]Msaada wetu u katika jina la BWANA,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
Bila Mungu hatuwezi kujipambania wenyewe anayetupigania ni Mungu pekeyake Wala hivi tulivyo si kwasababu ya hirizi au uganga fulani no no. ooooh watu wa Mungu tunajivunia kwasababu tunalindwa na nguvu za Mungu.
Ni hatari sana kuona mkristo unateswa na wachawi na waganga leo sema nalindwa na nguvu za Mungu, hivyo hakuna uganga wala uchawi juu ya maisha yangu. ISHI KWA IMANI SIKU ZOTE SEMA ATAKAYE KUNIDHURU MIMI NA FAMILIA YANGU KATIKA JAMBO LOLOTE AUSHINDE KWANZA MSALABA WA YESU AKIWEZA NDIPO TANIWEZA MIMI
Unajua shetani kazi yake ni akutese tu, akiangalia Huwezi hata kumshughulikia katika ulimwengu wa Roho
utakuta unaanzisha kabiashara kako anawafukuza wateja, anapiga mpaka mtaji nao mwee
Unawaza kusoma unajikuta unakosa Ada Wala mfadhiri hupati Shetani anazuwia njia zako zote za kufanikiwa kwa sababu hujazijua njia zake.
unajikuta leo mna amani kwenye ndoa / uchumba wenu lakini kesho mmeshavurugana na kutaka kuachana bila sababu ya msingi, anawasahaulisha na kusudi la Mungu kwamba ndiye aliye waunganisha, mweeee.
Kama ni huduma yako ilikuwa mpaka wewe mwenyewe unasema Safi, lakini unajikuta hujisikii kutumika tena ukipangiwa kuhudumi unakuwa na UDHURU usiona kichwa Wala miguu
kuomba tena huoni upako, kila wakati unajikuta bize hata kutenga muda wa kumuomba Mungu huna,
wewe hujishangai muda wa kulala au muda wa kula chakula husemi silali/ sili chakula leo niko bize mwishowe na mafunuo yanafungwa kabisa unaona giza tu.
shituka Kisha usikubali tena Shetani akuendeshee maisha yako kataa kabisa.
Elewa kwamba kazi ya shetani ni kuvuruga ,kuharibu na kuuwa kabisa Kama akiingia kwenye biashara yako anahakikisha amekula mpaka mtaji na wateja anawafukuza kabisa.
Kama ni mpango wako kufunga ndoa unajikuta hujisikii tena kuolewa unawaza kuwa single mother tu inatosha mmmmmh Kisa pesa unazo za kumtunza mtoto
Kama ni mwanaume unawaza kuzalisha mabinti tu halafu watoto wakikua utaenda kuwakusanya.
Shetani m baya sana, Wala hana mpango mzuri juu ya mwanadamu.
Ashukuriwe Mungu anayetuokoa na mkono wa Shetani ndio maana hata leo tumeamshwa salama pamoja na familia zetu Kama ni amani ipo mafanikio tunayaona , baraka za Rohoni na Mwilini tunaziona waoooow Sema tunalindwa na nguvu za Mungu atakayekuja kukujaribu kwa lolote akutane na Moto wa Yesu aunguzwe na kupotezwa milele.
Shetani hana chake tena kwasababu tumeshazijua njia zake na kwaajili hiyo tutashinda na zaidi ya kushinda kwasababu Mungu hajatuacha na hatatuacha kuwa mawindo kwa adui zetu haleluya.
TUOMBE
Baba yetu na Mungu wetu wa Mbinguni tuna kila sababu ya kukushukuru kwa kutuamsha salama , Tazama usiku wote hukutuacha kuwa mawindo kwa Yule mwovu Shetani. Ni kwa Neema na Rehema zako tu kuwa hivi tulivyo leo. Wewe Ni Mungu utupaye kushinda na zaidi ya kushinda, tunalisifu jina lako Yesu
umekuwa mwema na mwaminifu kwetu asubuhi, mchana, jioni, usiku hata usiku wa manane na alfajiri Bwana, majira yote kaa nasi mfalme mwema.
tupe nguvu za kupenda zaidi ,kukujua zaidi ili tukutumikie kwa uzuri wa utakatifu wako na kumshinda Shetani kwa mamlaka uliyotuachia Bwana.
tujalie moyo wa ibada ili tukuabudu wewe pekeyako katika Roho na kweli Mathayo 4:23-24,
AMEN.
Mwl Beata Silwimba
0742442164 /0620507212
Maoni
Chapisha Maoni