TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA


          TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA


DHAMBI 

ni uasi wa sheria ya MUNGU.

Ni matendo yote yaliyo chukizo kwa MUNGU.

1 Yohana 3:4 

"Kila mtu afanyaye dhambi,afanya uasi maana dhambi ni uasi."


UOVU

Ni dhambi iliyokomaa na kuwa ya kujirudiarudia kwa mhusika

👉Hii ni pale ambapo mtu anakuwa ameifanya dhambi kuwa desturi yake, na hutenda mara kwa mara. 


Isaya 59:2 

"lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na MUNGU wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia."


MAKOSA

Hii inahusisha utendaji wa mambo mabaya/ yasiyofaa kwa kukusudia au kutokukusudia, kwa kujua au kwa kutokujua.

  👉 Lakini kwenye maisha ya kawaida si kila kosa ni dhambi ila dhambi zote ni makosa 

Maneno yote matatu yanabeba kile na yana uwezo wa kumfanya mtu kuwa mbali na Mungu.  na husamehewa kwa kutubu tu! wala si kutenda wema. ni lazima utubu ndipo uanze kufanya wema

👍Mtu akitubia DHAMBI zake na kuacha kabisa anasamehewa.

👍Mtu akitubia UOVU wake na kuuacha anasamehewa.

👍Mtu akitubia MAKOSA yake anasamehewa.

Soma hapa👇


Kutoka 34:6-7

[6]BWANA akapita mbele yake, akatangaza, BWANA, BWANA, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli;

[7]mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, mwenye kusamehe UOVU na MAKOSA na DHAMBI;.......... 

Sasa kwa njia hii na namna hii ni lazima tujue kuwa kinachoweza kukupa kibali na kukuhakikia usalama wako ni mahusiano mazuri na Mungu, lakini kutubu pale unapofanya dhambi, kosa au kama upo katika uovu


1 Yohana 1:9-10

[9]Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote.

[10]Tukisema kwamba hatukutenda dhambi, twamfanya Yeye kuwa mwongo wala neno lake halimo mwetu.


Mungu atusaidie sana, tuwe watu wa kujitafakari kila wakati ili kama iko njia iletayo majonzi tutubu na kuacha.


Mungu akubariki



Taifa Teule Ministry
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI