KWEPA FITINA KWA UPENDO
Bwana asifiwe karibu tujifunze tena asubuhi ya Leo..
Biblia Inaweka wazi jinsi ya kukimbia fitia au kuikwepa miongoni mwa watu...
Haebu soma hapa 👇
[12]Kuchukiana huondokesha fitina;
Bali kupendana husitiri makosa yote.
Kumbe kama chuki Inasababisha kuwe na FITINA basi njia sahihi Kwa hapa ni Kutokuwa na chuki kati au baina ya watu...
Kukiwa na chuki miongoni mwa rafiki, kikundi au watu basi haya yaweza kutokea...
👉Kila mtu hatamuona mwingine kama msaada bali adui
👉Kila mtu atamtazama mwenzake kama chanzo cha huzuni yake
👉Moyo wa mtu na mtu wanaochukiana huwa hauwezi kukaa pamoja
👉Hakuna mtu atakuwa tayari kumsaidia mwenzake
👉Watu hawa wanaweza kushindwa kukosa fursa kwasababu mara zote fursa inayotengenezwa na Mungu huja kwa mtu kupitia watu
Na mbaza nyingine ni kwamba kunakuwa na FITINA kati yao.. Watu kusingiziana maneno ya uongo ilimradi tu mwenzake aonekane hafai...
Lakini badala yake biblia inasisitiza watu kupendana kwasababu upendo....
[4]Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni;
[5]haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya;
[6]haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli;
[7]huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
[8]Upendo haupungui neno wakati wo wote; bali ukiwapo unabii utabatilika; zikiwapo lugha, zitakoma; yakiwapo maarifa, yatabatilika.
👉Hata kama Kuna mtu amekukosea mara ngapi ukimpenda tu hutamuhukumu kwa ubaya wake bali utamsitili
👉Hata kama shetani alitaka kuileta FITINA miongoni mwenu kwa lango la chuki basi upendo hulifunga lango hilo
Tambua kwamba katika maisha yako
👉Wasiokupenda na kukukubali ni lazima wawepo
👉Wanaokuchukia lazima wawepo
👉Wanaotamani ushindwe maisha ili uanguke na kuabika lazima wawepo
Lakini Ashukuliwe Mungu kwamba si hivyo tu lakini katika wengi wanaokuzunguka Mungu atakuinulia watu wanaokupenda, kukujali, Wanaotamani ufike mbali kimaendeleo, wanaokuwazia mema.. Yaani Mungu hawezi achwa uzungukwe na waovu tu bali atakuzungushia na wema ili Tafsiri ya maisha itimie
Kwako ni kwamba katika maisha yako
👉Huna sababu ya kumchukia mtu yeyote bila kujali alivyo.
👉Huna sababu ya kujua kwanini watu fulani hawakupendi na wanakuchukia kwasababu
👉Kuna wanakuchukia kwa wivu
👉Kuna walioona unakitu kizuri ambacho wao hawana
👉Wengine wanaweza kukuona jinsi ulivyo rohoni wakajua wewe ni nani na wakaamua kuanza chuki... Sasa usipokuwa makini unaweza kujikuta umefungua mlango wa FITINA kumkaribisha shetani maishani mwako..
Kwanzia Leo sema NAUFUNGA MILANGO WA FITINA KWA KUTOKUMCHUKIA MTU YEYOTE NA NITAWAPENDA WATU WOTE BILA KUJALI WANAVYONITAZAMA KWA JINA LA YESU. AMINA
Minister mathayo Sudai
Maoni
Chapisha Maoni