KWANINI ULIMWENGU HAUKUMKUBALI YESU ANGALI YEYE NDIYE ALIYEUUMBA???


KWANINI ULIMWENGU HAUKUMKUBALI YESU ANGALI YEYE NDIYE ALIYEUUMBA???

Bwana asifiwe, karibu tujifunze...

Biblia inasema hivi 👇

Yohana 1:10-11
[10]Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
[11]Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.

Tunaposoma biblia Kuna kitu cha msingi tunakiona hapo kwamba Yesu ndiye aliyehusika kuumba ulimwengu lakini inaonekana alipokuja ulimwenguni tena ulimwengu aliouumba mwenyewe na siku zote yupo humo lakini ulimwengu haukumtambua na hata wale ambao walikuwa wake walimkataa yaani hawakumpokea.. Je ni kwanini???

Ni jambo la ajabu sana kama umemzaa mtoto halafu baadae anakuwa hakujui tena na hata ukimfuata anakukataa yaani hakupokei bila shaka ni lazima Kuna kitu ambacho kimempata mtoto huyo maana si kawaida....

NI HIVI👇

Adamu alipoumbwa na Mungu (kristo Yesu ), ulimwengu ulikuwa chini yake na kila kitu kilikuwa sawa maana nuru ya Mungu ilikuwepo lakini baada ya shetani kumdanganya Adamu na kufanya dhambi basi shetani alianza kupata nafasi na mamlaka katika uumbaji wa Mungu ambao kimsingi ulikuwa umewekwa chini ya Adamu na hapo shetani alianza kutia giza maeneo mbalimbali na hata nuru ya Mungu kwenye maeneo hayo au viumbe hivyo ilipotea na wakawa chini ya giza...

Kuwa chini ya giza ni sawa na kuwa mbali na Mungu kwasababu Mungu ni nuru kwahiyo ukiwa gizani maana yake haupo nuruni au kwa lugha nyingine haupo ndani ya Mungu...

1 Yohana 1:5
[5]Na hii ndiyo habari tuliyoisikia kwake, na kuihubiri kwenu, ya kwamba Mungu ni nuru, wala giza lo lote hamna ndani yake.

Hapa tuelewe kwamba adui wa giza ni nuru na sehemu yoyote inapoonekana nuru basi giza hupotea na likionekana giza basi nuru inapotea lakini ashukuruwe Mungu kwani nuru ikionekana tu giza haliwezi kuishinda...

Yohana 1:5
[5]Nayo nuru yang’aa gizani, wala giza halikuiweza.

Sasa Yesu alipokuja walio wake hawakumpokea kwasababu ndani ya fikra za watu kulikuwa Kuna giza ambalo ni kinyume na nuru iliyokuwa ndani ya kristo na hilo giza kwenye fikra za watu ndilo huwa lina fanya watu wamkatae Mungu, waikatae nuru....👇

2 Wakorintho 4:3-4
[3]Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
[4]ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.

Unaona hapo, kumbe shetani anapotaka watu wasiitii au waikatae injili(nuru) basi anapofusha fikra zao yaani anatia giza kwenye fikra zao...

Sasa kwasababu fikra za watu ndizo zinazoendesha au kuongoza matendo ya mtu basi mtu huyu utaona anaikataa injili au anamkataa Mungu kwa matendo... Unaweza kumkubali kwa maneno kwa kuigiza lakini matendo yako haswa ambayo yanaongozwa na fikra ndiyo yatakudhihirisha... Na ndiyo maana mafarisayo walimtii Yesu kwa maneno ila kwasababu ya fikra kuwa zimetiwa giza basi matendo yao yalienda kinyume n nuru... Wlimkataa YesuHata wewe Leo unaweza kujua kiwango cha jinsi unavyomkataa Mungu na kujua kiwango ch giza kwenye fikra yako kwa jinsi unavyoenenda.. Na ukiwa umeokoka na ukampa ibilisi nafasi ya kutia giza kwenye fikra yako basi utaikuta siku moja ukifanya jambo baya na ovu ambalo pengine ulishawahi kusema kwamba hutalifanya.... Na ndiyo maana yafaa kujali sana wokovu tulionao maana tukimpa ibilisi nafasi basi hali itakuwa mbaya....

Waefeso 4:27
[27]wala msimpe Ibilisi nafasi.

Huu ni mstari unaojitosheleza kabisa uko peke yake.....

Waebrania 2:3
[3]sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia;

Walio wake hawakumpokea kwasababu walikuwa wametawaliwa na giza, basi kwa kuwa na wewe ni wake pia basi hata wewe unaweza kumkataa kwa matendo, Maneno yako na mwenendo wako kama ukiruhusu giza (mambo ya dunia, dhambi ) likutawale

Mungu akubariki sana

@Taifa Teule Ministry
Minister Mathayo Sudai


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA