MAFANIKIO SIYO AJALI NI MATOKEO


    MAFANIKIO  SIYO AJALI NI MATOKEO

Bwana asifiwe karibu tujifunze tena hapa asubuhi njema...

Tunaishi kwenye maisha ambayo ya a watu wawili katika viwango vya kimaisha yaani maskini na tajiri na mara zote kila mtu hutamani kuwa tajiri kwenye maisha yake ili aweze kujimudu na kuendesha maisha yake vizuri...

Lakini je unajua kuwa utajiri na umaskini siyo ajali???

Hali hizi mbili ni matokeo ya utendanji kazi, kufikiri na imani ya mtu mwenyewe..

Umaskini huanzia katika akili, kisha imani na mwisho kuongoza utendaji kazi wa mtu na hata umaskini kujidhihirisha kwa mtu...

Katika kutenda kazi hapa Kuna uvivu na uhodari,

Biblia inasema hivi 👇


 Mithali 10:4
Bali mkono wake aliye na bidii hutajirisha. 
[4]Atendaye mambo kwa mkono mlegevu huwa maskini; 

Ukiwa unafanya kazi kivivu na Huku unatarajia ustawi basi tambua unaidanganya nafsi yako 

Mafanikio ya kiuchumi hayahitaji maombi bila kufanya KAZI kwa bidii, ukikaa ndani, ukafunga na kuomba kwa bidii haina maana kuwa uchumi wako utastawi bali inahitaji mipango mizuri, kazi kwa bidii kisha hapo sasa unaweza kuongeza maombi, lakini maombi siyo ufunguo wa uchumi na ndiyo maana biblia ikasema afanyaye kazi kwa ulegevu lazima atakuwa maskini... Hakusema asiyeomba... 

Lazima tuwe na ufahamu huu kwamba kila kitu rohoni kina namna yake ya kiutendaji... 

 Na ndiyo maana ikifika wakati wakuangusha misingi ya kishetani na vifungo vya kipepo hapo maombi ndiyo yanayotakiwa na si kufanya KAZI kwa bidii

Unaweza kuuliza Mbona Kuna watu wanabidii lakini hawajafanikiwa???

Ni hivi kufanikiwa ni muunganiko imani, jinsi unavyofikiri na kazi..

Kama unafanya kazi pekeyake na Huna fikra au mawazo ya kitajiri au kufanikiwa pia huwezi kufanikiwa na ndiyo maana biblia inasema AWAZAVYO MTU NDIYO ALIVYO..

Ni kweli unafanya kazi lakini je mawazo yako yapoje,?? Je unawaza kama mtu aliyefanikiwa au kam mtu aliyekandamizwa na umaskini??

Unapopambana kwenye kazi zako basi Anza kuwa kama mtu ambaye amefanikiwa, Anza kuongea kama mtu aliyefanikiwa...

Ningependa ujue kuwa maisha ya mtu ni matokeo ya mawazo yake na jinsi anavyoongea mbali na bidii ya kazi

Na Unapokuwa unawaza na kuongea kama mtu aliyefanikiwa basi imani yako juu ya kufanikiwa inaanza kujengeka na utaanza kuishi katika uhalisia wa hiyo imani.. Na hivyo ndivyo hata watu wa Mataifa waliofanikiwa hufanya...

Wakristo wengi hupenda kuhusisha kila aliyefanikiwa na nguvu za giza kiasi cha kupelekea kuamini kuwa ili ufanikiwe lazima umuue mtu utoe kafara, jambo ambalo biblia zao zenyewe hazijawahi kusema njia hiyo haza zinaposungumzia mafanikio...

Hamisha imani yako huko wekeza katika fikra, imani na bidii ukiambatanisha na kumpenda Mungu .. Na kwa kuwa na juhudi bila mkono mlegevu basi Mungu atakubariki na kubariki kazi ya mikono yako


Mungu awabariki sana


 @Taifa Teule Ministry
 Minister Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?