KUMWAIBISHA MWENYE KOSA SI TABIA YA MWENYE HAKI
KUMWAIBISHA MWENYE KOSA SI TABIA YA MWENYE HAKI
Na: Min. Sudai.
Bwana asifiwe wana wa Mungu.
Karibu tujifunze jambo fulani la mtu mwenye haki.
Ni kweli kwamba kila mtu aliyeokoka au anayesali hujisema au hujihesabu kuwa ni mwenye haki, lakini si wote ni wenye haki, kwasababu kuwa mwenye haki haina mahusiano na unavyojiona bali kuwa na sifa za mwenye haki ambayo baadhi yake tunaiangalia hapa leo...
Tunajifunza kupitia Yusufu mume wa mariamu mama wa Yesu..
Soma hapa👇
Mathayo 1:18-19
[18]Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. [19]Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.
Kilichomfanya Yusufu atake kumwacha mariam ni kwasababu aligundua kuwa mariamu ana mimba.. na kilichomfanya atake kumwacha kwa siri ni kwasababu hakutaka kumwaibisha na hakutaka kumwaibisha kwasababu Yusufu alikuwa mwenye haki..
Kwahiyo hapo maandiko yanakiri kwamba hakutaka kumwaibisha mariamu kwasababu Yusufu alikuwa mwenye haki..
Sasa hapo unaweza kujiuliza swali kwamba... mariamu kijamii angeonekana ni mwanamke mwasherati/mzinifu kwasababu Yusufu angemwacha hadharani inamaana kwamba kila mtu angejua kwamba mariamu ameachwa kwasababu alikuwa na mimba ya nje ya ndoa au kabla ya ndoa.
Pia katika jamii ya israeli na utamaduni wao, Mariamu asingefaa katika jamii kwani angeonekana kupoteza ubikira wake nje au kabla ya ndoa jambo ambalo ni tabia mbaya kwenye jamii hasa kwa mwanamke..
Lakini Yusufu kwa kuyajua hayo yote, na akijua kwamba mariamu amemsaliti kwa kuzaa na mwanaume mwingine na nje ya ndoa lakini hakutaka kumuumbua, au kumuongezea shida ya aibu mbele za jamii kwahiyo aliazimia kumwacha kisirisiri. Na biblia inadai kuwa alikusudia kufanya hivyo kwasababu alikuwa ni mtu wa haki..
Hii inaonyesha kuwa mwenye haki...
🫳Huificha aibu ya watu wengine na si kuwadharirisha
🫳Hawezi kufanya jambo kwa kujua litakuletea aibu.
🫳Huumia na kuvaa viatu vya mtu mwenye aibu na hujisemea kwamba ingekuwa mimi je ingekuwaje
🫳Hupambana kumfanya kila mtu awe na heshima kwenye jamii
🫳Huumia akiona unachafuliwa
🫳Hapendi kuona ukisingiziwa au kusemwa kwa mabaya
🫳Hufikiria heshima ya wengine kabla yake
🫳Atasimama kama mpatanishi hasa watu wanapofarakana kwa mambo yenye kuleta aibu
🫳kama ni ndani ya kanisa mtu huyu atamlinda mchungaji wake dhidi ya aibu na kulihifadhi kanisa pale linaposhambuliwa na hawezi kuwa mmojapo wa kulishambulia kanisa.
🫳Kama ni rafiki yako basi hawezi kukushambulia kwa pembeni wala kujusema
🫳Mwenye haki hufanya ya haki na kujiepusha na mabaya.
Je wewe ni mwenye haki..???
Ukijiona wewe ni mtu anayependa kuwaumbua sana watu wenye udhaifu, waliokosea, wenye changamoto katika namna ya kuwapiga kwasababu ya kuwachafua na kuridhisha nafsi yako basi jua hata kama umeokoka au unasali lakini wewe SI MWENYE HAKI kwasababu hiyo si tabia ya wenye haki...
Minister Mathayo Sudai

Maoni
Chapisha Maoni