SI KILA SILAHA INATUMIKA SEHEMU ZOTE...
SI KILA SILAHA INATUMIKA SEHEMU ZOTE...
Bwana asifiwe Wana wa Mungu.. Leo naomba nikushirikishe habari ya Vita ya kiroho na hapa nazungumzia kuhusu siraha za vita hiyo...
moja ya vitu ambavyo tunatakiwa kuvijua na kujua jinsi ya kuvitumia ni silaha za kiroho .... maana ukishindwa basi unaweza kujikuta unapigwa kwasababu huzijui au hujui jinsi ya kuiitumia...
kimsingi Vita ya kiroho ni jambo ambalo kanisa limelipuuzia Sana kiasi kwamba wakristo wengi hawaelewi chochote kuhusu Vita ya kiroho na wanabaki kushangaa tu pale wanapionanmambo hayaendi au kuharibika...
hebu tuone silaha za milele na sehemu ya kuzitumia...
hapa nazungumza kuhusu
👉jina la Yesu
👉Damu ya Yesu na
👉Neno la Mungu ....
Kuna silaha nyingi za kumlinda mtu na kushambulia pia kulingana na Waefeso 6..
1. Unapohitaji
👉kukemea pepo basi ni kwa jina la Yesu
👉kuombea wagonjwa ni kwa jina la Yesu
👉kunena kwa Lugha mpya ni kwa jina la Yesu
👉Kukanyaga nyoka na ng'e ni kwa jina la Yesu
👉kuokolewa/ Kuokoa ni kwa jina la Yesu...
2.Unapoona
👉unataka kupambana na roho za mababu..
👉Mizimu ya kwenu
👉Madhabahu za kifamilia au ukoo ambazo kupitia madhabahu na kafara zilizotolewa na waliokutangulia basi hizo Roho zilipata kibali Cha kukaa kwenye famila bas hapo utatumia damu ya Yesu,ukitumia jina la Yesu basi jua hiyo siyo kazi yake Bali damu ndiyo unayoondoa mashtaka na madai yote na haki yake kwenye maisha yako.. na ndiyo maana inaitwa damu ya ukombozi...
3.Unapoona
👉SHETANI amekuja moja kwa moja kwenye maisha yako na kukwambia jambo fulani basi ni lazima ujue kwamba amekuja kwako na mpango pamoja na lengo madhubuti kabisa ... hapo utatumia NENO LA MUNGU... yaani ujue kusema IMEANDIKWA..... (Mathayo 4)
SHETANI Huwezi kumpinga kwa jina na damu Bali ni kwa Neno ... na ndiyo maana unaona hata manabii wa uongo wanataja jina la Yesu na damu ya Yesu lakini wanachokifanya na kulipindisha neno la Mungu .....
👉na ndiyo maana hata Yesu mwenyewe alipofuatwa na SHETANI kujaribiwa alipokuwa jangwani basi alimtumia Neno la Mungu tu yaani alikuwa anasema IMEANDIKWA
👉Hii ikusaidie kujua kwamba maisha yako na maombi yako yakikosa Neno IMEANDIKWA .. Maana yake yasiwe na Neno la Mungu basi kumshinda SHETANI sahau.... unaweza kuwa unaota pepo kwa jina la Yesu, lakini anapokuja SHETANI mwenyewe basi ni lazima akushinde kwasababu huna Neno... na ndiyo maana akasema "Neno la Mungu na like kwa wingi ndani yenu"....
Mungu akinipa kibali basi nitakutumia voice note (Ujumbe wa sauti ) ili uelewe vizuri ..
Mungu akubariki sana...
Taifa Teule ministry
Minister Mathayo Sudai
Maoni
Chapisha Maoni