MUNGU ANAJIBU MAWAZO YAKO SIYO MANENO YAKO...
MUNGU ANAJIBU MAWAZO YAKO SIYO MANENO YAKO...
Min Mathayo Sudai
Bwana asifiwe wana wa Mungu... Njoo tujifunze kuhusu jinsi Mungu anavyoyatazama mawazo yako, na ukilijua hili hautadharau mawazo yako tena....
Kimsingi Mungu na Shetani wanapenda au hutenda kazi kupitia ulimwengu wa mawazo ya mtu yaani jinsi unavyowaza... (The realm of thoughts)
Isaya 65:24
[24]Na itakuwa ya kwamba, kabla hawajaomba, nitajibu; na wakiwa katika kunena, nitasikia.
Unaona kujibiwa kunaanza hata kabla ya mtu kutamka kile anachokihitaji... Kwasababu kile ambacho unakitamka ni matokeo ya vile unavyowaza, kabla hujaanza kuomba ni lazima utawaza kile kitu ambacho utakiomba...
Kwa mfano. Unaweza kuwaza kuhusu kuhitaji kuwa Mtakatifu, unavyowaza basi Mungu anakuwa ameshapata hitaji lako na kimsingi anakujibu hapohapo kwa KUKUPA roho ya utakatifu hii ni dhahiri kwamba Mungu anajibu mawazo yako na si maneno yako.....
Mfano mwingine,
Katika kitabu cha Danieli tunamuona Daniel akiwa anaomba mambo fulani kwa Mungu kwa muda Wa siku 21... Lakini malaika ailipokuja alimwambia hivi👇
Danieli 10:12
[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Unaona kumbe danieli maombi yake yalijibiwa ile siku ya kwanza alipotia Moyoni (alipowaza) kile anachokihitaji hata kabla hajaanza kutamka maneno /kuomba...
Hii nayo inaonyesha kwamba Mungu alisikia mawazo ya moyo wa danieli hata kabla hajaomba kwa mdomo....
Hata kuletwa Eva haukuwa mpango timilifu wa Mungu bali ni matokeo ya kuwaza kwa Adamu.... 🤔🤔 (unaweza kushangaa lakini usijali karibu kwenye nyumba ya ufunuo kimaandiko.)
Sasa hapo tunaona kumbe mawazo yetu ni moja ya nguvu ya msingi sana ambayo Mungu amempa mtu ili kuwa vile atakavyo mtu mwenyewe, na ili kuelewa hivyo tambua kwamba jinsi ulivyo ni matokeo ya jinsi unavyowaza....
Mithali 23:7
[7]Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo.
Akuambia, Haya, kula, kunywa;
Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe.
Aonavyo mtu nafsini mwake ni sawasawa na kusema awazavyo mtu Moyoni mwake...
For as he thinketh in his heart, so is he: Eat and drink, saith he to thee; but his heart is not with thee.
Neno thinketh (think) maana yake kuwaza( kufikiri).. Sasa kumbe awazavyo mtu ndivyo alivyo... Yaani vile unavyowaza ndivyo unavyokuwa kwasababu mawazo yako ni nguvu ya kiroho inayovuta uhalisia wa rohoni kuwa dhahiri mwilini... Hata kama unafanya kazi au unaomba kwa bidii lakini kama mawazo yako ni tofauti na maneno unayotamka kinywani basi hayo maombi hayana faida yoyote.... Na ndiyo maana kabla ya kuomba lazima kutafakari neno la Mungu ili unapoanza kuomba basi uombe sawasawa na ulivyokuwa unawaza /kutafakari neno... Mawazo yako na maneno yako yanakuwa sambamba... YANAONGEA kitu kimoja au niseme yamepatana....
Kiwango cha majibu yako kina mahusiano makubwa sana na aina ya mawazo yako kwasababu mawazo ni moja ya nguvu ya kiuimbaji aliyonayo mtu inaweza kuleta kitu kutoka rohoni hadi mwilini..... Hata Mungu pia anajibunkwa kadiri ya jinsi unavyowaza Moyoni mwako...
Som hapa....
Waefeso 3:20
[20]Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;
Unaona hapo kumbe Mungu hufanya mambo kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani mwetu... 🤔🤔
Zipo nguvu kadhaa hapo zinazounda hiyo nguvu itendayo kazi ndani mwetu( siyo ujumbe wa leo) lakini moja ya nguvu hizo ni mawazo yako....
Na ndiyo maana Leo hii shetani anatengeneza vitu vingi kama vile
👉Video za ngono
👉Nyimbo za kidunia
👉Staili mbalimbali za kucheza
👉Video/movies mbalimbali
Ambavyo watu wengi hawaelewi ajenda yake lakini ni kwamba shetani anatageti kukufanya uwaze sawasawa na anavyopenda yeye kwasababu unachokitazama, kukisikiliza na kukifanya kina nguvu ya kusababisha mawazo yako kuwa sawa na ulichokitazama au kukisikiliza... Mawazo yako yanajaa kile unachokitazama au kukisikiliza.. Sasa fikra ikisha kuwa na mawazo ya hivyo basi Kumbuka mawazo yanaweza kuvuta uhalisia wa unachokiwaza ukadhihirika kwenye maisha yako kwasababu awazavyo mtu ndivyo alivyo..
Sasa kupitia mawazo yako shetani anakuwa amefanikisha kukufanya kuwa kama alivyokuwa anataka.... Kimsingi lazima ujue shetani hawezi kukuharibia maisha yako kwasababu hana nguvu hiyo lakini anajua nguvu uliyonayo wewe hivyo atakachokifanya ni kukusababisha wewe unafanya vitu kwa nguvu yako hiyo hiyo na unajikuta unajiangamiza mwenyewe na baadae unaanza kumtafuta mchawi kumbe mchawi ni wewe mwenyewe....
Shetani anavyoendelea kuweka giza kwenye mawazo yako ndivyo anavyopofusha fikra zako na unajikuta hutaki mambo ya kimungu bali Unapenda ya kidunia kwasababu ndiyo uliyoruhusu ayaweke kwenye fikra zako na hata mtu akikwambia habari za Yesu unamuona ni mshamba bila kujua kwamba wewe ndiye mshamba mwenyewe... 😄 😄
2 Wakorintho 4:3-4
[3]Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
[4]ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Kwa hiyo elewa kwamba Mungu anataka kutumia mawazo yako kuleta matunda na hivyo hivyo shetani anataka mawazo yako kuleta uharibifu kwasababu hao wote hawawezi kufanya kitu duniani mpaka wamtumie mtu...
Hivyo Mungu anajibu mawazo yako hata kabla hujaomba..
TUJIULIZE KIDOGO
👉Kama ni hivyo kwamba Mungu anajibu mawazo Kuna haja gani ya kuomba???
👉Je nikiwa nawaza tu pekeyake si inatosha mimi kupata majibu??
Jibu ni kwamba
Japo kuwa Mungu ameyajibu mawazo yako lakini majibu yako hutayapata mkononi mwako mpaka utakapoomba🤔🤔
Usifikirie sana bofya link hii hapa kujifunza hilo👇
https://elimuyabiblia.blogspot.com/2025/03/kama-mungu-anajibu-mawazo-kwanini.html
Minister Mathayo Daudi Sudai
0744474230
Maoni
Chapisha Maoni