KAMA MUNGU ANAJIBU MAWAZO KWANINI TUNAOMBA??
KAMA MUNGU ANAJIBU MAWAZO KWANINI TUNAOMBA??
Na: Minister Mathayo Sudai
Bwana asifiwe karibu tujifunze tena hapa...
Katika somo la nyuma tulijifunza kwamba Mungu ANAJIBU MAWAZO YAKO SIYO MANENO YAKO...
Kama hujalipitia somo hili ni vizuri ukalipitia ili ukija Kuendelea uwe unaelewa vizuri...
Bofya link hii hapa kwa somo hilo kabla hujaendelea na hili👇👇
https://elimuyabiblia.blogspot.com/2025/03/mungu-anajibu-mawazo-yako-siyo-maneno.html
Kama umeshaelewa njoo tuendelee...
Tuliishia kwenye kujiuliza
👉Kama ni hivyo kwamba Mungu anajibu mawazo Kuna haja gani ya kuomba???
👉Je nikiwa nawaza tu pekeyake si inatosha mimi kupata majibu?? Lakini tukasema Jibu ni kwamba
Japo kuwa Mungu ameyajibu mawazo yako lakini majibu yako hutayapata mkononi mwako mpaka utakapoomba(kutamka uliyokuwa unawaza) 🤔🤔
SASA
Ili kuelewa hapa ni lazima tukubaliane na Biblia kwamba Mungu anapohitaji kumuhudumia mwanadamu huwa hafanyi yeye bali watumishi wake ndiyo huwa wanafanya kazi hiyo na watumishi wa Mungu kwaajili ya kuwahudumia watu ni MALAIKA..
Waebrania 1:13-14
[13]Je! Yuko malaika aliyemwambia wakati wo wote,
Uketi mkono wangu wa kuume
Hata nitakapoweka adui zako chini ya nyayo zako?
[14]Je! Hao wote si roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?
Unaona hapo kumbe malaika ni roho wanaotumika kuwahudumia watu wa Mungu..
Sasa unapowaza/kufikiri Mungu ANAJIBU MAWAZO YAKO hata kabla hujaomba yaani haya majibu yanakuwa mikononi mwa malaika anayepaswa kukuletea majibu hayo lakini haanzi safari ya kuja kwako...
Na unapoomba sasa ndipo yule malaika mwenye majibu yako anaachiliwa kuja kwako... ( Prayer release an angel)
Hebu tuangalie biblia tulione hili....
Tuangalie kwa danieli palepale
Tuliona kwamba danieli alipowaza tu ile siku ya kwanza Mungu alimjibu na malaika alipokuja alisema hivi👇
Danieli 10:12
[12]Ndipo akaniambia, Usiogope, Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu, na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami nimekuja kwa ajili ya maneno yako.
Hebu soma kwenye hicho kipande cha mwisho... Malaika alisema NAMI NIMEKUJA KWAAJILI YA MANENO YAKO... 😄
Yaani ni kwamba mawazo ya danieli yalikuwa ni maneno mbele za Mungu na ndiyo maana Mungu akamjibu na alipoanza kuomba maana yake alitamka maneno sawasawa na yale yaliyopo kwenye mawazo na hayo maneno aliyokuwa akitamka kwenye maombi ndiyo YALIYOSABABISHA MALAIKA AJE.
Si mimi niliyesema ila ni malaika mwenyewe alisema,, NAMI NIMEKUJA KWAAJILI YA MANENO YAKO... Kwahiyo kumbe ukiwaza Mungu anasikia na kukujibu lakini unapoomba sasa ndipo yule malaika mwenye majibu yako anaachiliwa kuleta hayo majibu....
Mfano mwingine, tuangalie kwa Petro...
Matendo ya Mitume 12:1-7
[1]Panapo majira yale yale Herode mfalme akanyosha mikono yake kuwatenda mabaya baadhi ya watu wa kanisa.
[2]Akamwua Yakobo, ndugu yake Yohana, kwa upanga.
And he killed James the brother of John with the sword.
[3]Na akiona ya kuwa imewapendeza Wayahudi akaendelea akamshika na Petro. Siku hizo zilikuwa siku za mikate isiyochachwa.
[4]Alipokwisha kumkamata, akamweka gerezani akamtia mikononi mwa vikosi vinne vya askari wanne wanne, wamlinde, akitaka baada ya Pasaka kumtoa na kumweka mbele ya watu.
[5]Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.
[6]Hata wakati Herode alipotaka kumtoa, usiku ule ule Petro alikuwa analala katikati ya askari wawili, amefungwa minyororo miwili; walinzi mbele ya mlango wakailinda gereza.
[7]Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.
Ukiendelea unaona Petro anaokolewa mpaka nje na huyo malaika
Unaona hapo... Herode alimuua YAKOBO lakini Mungu hakufanya chochote kumsaidia lakini alipokamatwa Petro tunaona Mungu alimuokoa kwa mkono wa malaika...
Je ni kwasababu Mungu alipanga iwe hivyo au alikuwa hampendi Yakobo??? Jibu ni hapana....
Lakini ukisoma vizuri wakati Petro kakamatwa kwenye mstari wa tano biblia inasema hivi👇
[5]Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.
Unaona hapo anasema NALO KANISA LIKAMWOMBA MUNGU KWA JUHUDI KWAAJILI YA PETRO...
Kwanini Yakobo hakuokolewa??? Ni kwasababu kanisa halikuomba lakini Petro alipokamatwa kanisa lilishtuka likaona huu siyo mpango wa Mungu ndipo likaomba...
Haya maombi ya kanisa ndiyo yaliyosababisha malaika kuachiliwa na kumuokoa Petro...Kwa hiyo maombi husababisha malaika kuachiliwa na kuleta majibu....
Katika wafilipi 4:6 Biblia inasema
Wafilipi 4:6
[6]Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.
HAJA ZENU NA ZIJULIKANE NA MUNGU...
Unaweza kuwa unapitia hali mbaya na wewe ukasema haina haja ya kuomba kwasababu Mungu anaona... Hapo utakuwa unakosea na hutapata au Mungu hatakusaidia na si kwamba hakupendi ila anasema tuseme haja zetu kwasababu unapotamka ndipo malaika mwenye majibu anaachiliwa (Maombi humuachilia malaika)...
Kwa hiyo tukiunganisha na somo la kwanza tunapata Kuelewa jambo hili hapa kwamba...
TUKIWAZA MUNGU ANASIKIA NA KUJIBU NA TUKIOMBA MALAIKA ANAACHILIWA KULETA MAJIBU YETU...
Si ajabu hata biblia inasema Mungu anayajua mawazo ya watu....
Zaburi 94:11
[11]BWANA anajua mawazo ya mwanadamu,
Ya kuwa ni ubatili.
Mathayo 9:4
[4]Naye Yesu, hali akijua mawazo yao, akasema, Mbona mnawaza maovu mioyoni mwenu?
Baada ya kuwa Mungu anajua mawazo yetu sasa anasisitiza Tuombe bila kuchoka maana yake tuyaseme yaliyopo kwenye mawazo yetu maana tunapotamka ndipo malaika wake anaachiliwa kuleta majibu...
Mungu akubariki sana
Kama una swali lolote hapo kuhusu somo hili karibu sana uliza, komenti pia
Minister Mathayo Daudi Sudai
0744474230
Maoni
Chapisha Maoni