NA WEWE HUIPENDI HEKIMA ??
NA WEWE HUIPENDI HEKIMA ??
Bwana Yesu asifiwe
njoo tujifunze kitu kizuri Leo kwa msaada wa Mungu
NI HIVI
👉Hekima huwa ni jibu kwa maswali mengi Sana...
👉Hekima inaweza kumlinda mtu mwenye nayo... kama vile fedha ilivyo na nguvu ndivyo Hekima ilivyo na nguvu pia kwa Mwenye Hekima..
Muhubiri 7:12
Kwa maana hekima ni ulinzi, kama vile fedha ilivyo ulinzi; na ubora wa maarifa ni ya kwamba hekima humhifadhi yeye aliye nayo.
👉Hekima inaweza KUMPA mtu njia ya Nini afanye pale anapokutana Na jambo linalotaka uamuzi
👉Hekima inaweza kumfanya mtu akawa salama kaka ataisikiliza
👉Hekima inaweza KUMPA mtu Mali nyingi katika Dunia hii...
👉Hekima inaweza kumfanya mtu akafatwa na watu ili awafundishe hekima
👉Hekima inaweza kufanya Mali za wengine zikakuhudumia .... watu kutoka pande nyingi watakuja na mali zao kwako na weweutajivunia Utajiri wa watu wa mataifa .... Soma habari za suleimani... malkia wa sheba alikuja na wengine wengi pamoja na mali zao ili kuiona na kusikiliza Hekima ya sulemani..
lakini biblia inasema kuwa ...
Kuna kundi la watu ambao huidharau Hekima na inawataka kuwa ni wapumbavu...
👉mpumbavu anataka kufanya kama anavyoona yeye na si kama isemavyo Hekima
👉Mpumbavu, haangalui njia njema ya uamuzi Bali hufanya tu kulingana na kile anachokiona..
👉Mpumbavu anaweza kusikiliza mhemuko, na sauti ya makundi yaani mkumbo na kujikuta amefanya mambo ambayo hata yeye hafananii nayo...
👉Mpumbavu anapenda upumbavu na ukizungumza kwa Hekima atakuona unajiona kuwa Bora kuliko wengine
👉mpumbavu akionywa na kurekebishwa basi atakuchukia
👉Stori za kijinga ndizo anazizipenda, habari za Hekima hazimfurahishi mpumbavu
👉mpumbavu humchukia Mwenye Hekima na Hekima yake bila sababu...
👉Mpumbavu akiwa juu yako, kiongozi wako, mbeba maono wako, tegemeo lako basi jiandae kuumia hata kama wewe ni mlokole Safi...
👉Mpumbavu anapenda majivuno na kuonyesha nguvu aliyonayo, hivyo katika hasira ya mpumbavu Kuna madhara makubwa kwasababu anapochukia basi anaweza kufanya jambo bila kujali madhara yake.. na ndiyo maana Biblia inasema...
Mithali 29:11
Mpumbavu hudhihirisha hasira yake yote; Bali mwenye hekima huizuia na kuituliza.
Waefeso 4:26
Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka;.....
Mungu akikujalia, Hekima basi usijaribu kufikiri kwamba unaweza kupendwa na mpumbavu kwasababu Hekima ni kinyume Cha upumbavu na kila utakachokifanya hatakipenda, na wewe Wala usihangaike kupatana na mpumbavu.. maana huko ni kupoteza muda kwani yeye hataki Hekima yako...
Mithali 23:9
Usiseme masikioni mwa mpumbavu; Maana atadharau hekima ya maneno yako.
ukiwa mkristo nakushauri, chagua kuwa na Hekima kuliko upumbavu ... na Hekima ya kimungu inadhihirika hapa👇
Ayubu 28:28
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu....
hakuna Mwenye Hekima ya kimungu asiyemcha Mungu.. na Hekima mbali na hili bais ni Hekima ya Dunia ambayo kimsingi ni upumbavu mbele za Mungu ...
1 Wakorintho 1:20
Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mlete hoja wa zamani hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu?....
" Huwezi kuwa na Hekima ya Mungu kaa upo mbali na Mungu ....."
Mungu akubariki Sana...
Taifa Teule ministry
Minister Mathayo Sudai
Maoni
Chapisha Maoni