USIMSAHAU MTOTO.

                    USIMSAHAU MTOTO.

Bwana asifiwe watu wa Mungu...

Leo naomba tutazame juu ya watoto na kile tunapaswa kuwafanyia ili wawe Salama....

Mithali 22:6 
 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.

MTOTO ni mtu ambaye haijafika katika hatua ya kujisimamia, yaani bado anahitaji kufanyiwa kila kitu ili awe Salama...

👉MTOTO anahitaji kununuliwa nguo
👉kufuliwa..
👉kuogeshwa 
👉na kila kitu ambacho Mwanadamu anakihitaji isipokuwa yeye anatafanyiwa hayo yote. 

mtoto anahitaji hayo katika Masha yake, na hayo yote anatakiwa kupewa au kufanyiwa na mtu mzima asiye  mtoto kama yeye....

lakini Kuna kitu Cha msingi Sana kwa watoto kinaitwa MALEZI..

MALEZI ndilo japo linalotengeneza njia ambayo mtoto anaifuata... kimsingi mtoto Hana uwezo wa kuchagua njia ya kupita, lakini mtu mzima lazima awepo ili kumwonyesha njia na kumsimamia mpaka pale atakapokuwa amekuwa na uwezo wa kujisimamia kwenye mambo Yake...

Tunaposoma Biblia tunaona Mungu anaagiza Wana wa Israeli wawafundishe watoto wake Sheria zake.. (Kumbukumbu la Torati 6)

kitu muhimu Sana Cha kujua kuhusu mtoto ni kwamba Kuna wakati ambao ni rahisi Sana mtoto kufuata kitu unachomfundisha, hapa ninamaanisha umri wa siku moja Hadi miaka nane,8 ....

huu ndiyo umri ambao kama mzazi, mlezi au mtu mzima Unatakiwa kuwa makini Sana juu ya kile unachompa, kumuonyesha, kumsikilizisha, n.k... kwasababu hapa ndipo msingi unajengeka ndani ya mtoto.... kumbuka kuwa makini Sana kwa mtoto Mwenye umri wa siku moja Hadi miaka 8, ni muhimu Sana...

Biblia inasema mlee mtoto kwenye njia nzuri naye hataiacha... hii inawezekana kwasababu niliyokuonyesha hapo juu... kina umri ambao mtoto wako anafuata kile ambacho umekiruhusu kwake ...


👉kama mtoto ana miaka ndani ya huo umri na anashinda kwenye TV kuangalia katuni, na wewe unamtazama tu basi jiandae kuumia baadae...
👉Mtoto usimfundishe Wala kumruhus kukaa kwenye TV kuangalia movie na siku hizi unakuta mzazi na watoto wake wote wanafuatilia movie fulani toka ilivyoanza Hadi mwisho 
👉mtoto usimfundishe kwenda kwenye maeneo ambayo yanatawalisha na roho chafu...
👉Jifunze kumuonyesha mwanao vitu vizuri
👉msikilizishe vitu vizuri 
👉mpeleke sehemu nzuri pia ... kwasababu mtoto huwa anajifunza na kulishika jambo pale anapolitazama, kusikiliza mara kwa mara n.k....

pia tambua roho chafu na Roho mtakatifu pia hupenda Sana kukaa katika mwili wa mtu... hii ikusaidie kujua kuwa  watoto hutazamwa Sana na roho nyingi kwasababu zikikaa kwa mtoto basi anaweza kukua nazo kiasi Cha kushindwa kumpendeza Mungu kabisa....

usiruhusu mtoto wako akawa jumba la maroho machafu, na hili ni kwa kumlea katika njia sahihi...

usijaribu kuwaza ustawi wako wa kiroho na kumpotezea mwanao tambua kuwa naye anahitaji kuingia kwenye ufalme wa Mungu kama wewe ..

👉Ombea mtoto wako
👉Mfundishe mtoto mapenzi ya Mungu taratibutaratibu..
👉Unapoenda kanisani hakikisha naye ameenda, Tena ikibidi nenda naye...
👉Usiweke hatima ya watoto wako kwa mfanyakazi wa ndani.... hapa sisemi usiwe na mfanyakazi lakini malezi sahihi ya mtoto wako hakikisha unayatoa wewe...

Ukimuanzà mwanao mapema basi jua hataiacha.. tatizo ni kwamba wengi huanza kuwazoesha watoto wao mambo sahihi angali wameshakua tayari, akili zao zimeshapokea mambo mengi yasiyofaa ....

TAFAKARI, chukua hatia


Mungu akubariki sana

Minister Mathayo Sudai

Taifa Teule Ministry 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI