SHERIA YA MUNGU NI UZIMA SIYO UDIKTETA

SHERIA YA MUNGU NI UZIMA SIYO UDIKTETA

Bwana asifiwe karibu tujifunze tena katika asubuhi ya Leo jumapili...

Kuna watu wengi naamini huwa wanajiuliza au walishawahi kujiuliza maswali haya hapa👇👇

👉Kwanini Mungu ameweka sheria nyingi za kumuongoza mtu?? 

👉Mbona kama mtu hana uhuru wake mwenyewe?? 

👉Mbona Mungu anawaongoza watu kama dikteta kwa amri fulani fulani nyingi?? 

👉Mbona mambo ya Mungu yana taratibu nyingi sana za kuzitii ???

👉 Mbona biblia imejaa makatazo mengi sana ya Mungu kwa mwanadamu???

Sasa nilazima ujue kwamba yote aliyoyasema Mungu kwa watu wake... Si tu kwasababu anataka umuheshimu kwa kuyatii lakini mambo hayo ni ufunguo wa mambo fulani katika roho

 Kwa mfano

Mungu aliposema USIZINI si kwamba amekutawal kidikteta  lakini anajua ukifanya uzinzi si tu kwamba unamkosea yeye bali Kuna madhara makubwa sana utayapata ambayo ni matokeo ya zinaa hata kama atakusamehe ukitubu...

Ukitubu, Mungu anakusamehe dhambi lakini madhara ya dhambi hiyo utabaki nayo na yataangamiza au kudhoofisha nafsi yako....

 Mfano mwingine

Mungu akikwambia toa zaka, si kwamba anatawala uchumi wako kidikteta hapana, bali Mungu anajua kwamba zaka ni ufunguo wa kufungua  baraka fulani za kimaisha kwenye maisha yako.... Si kwamba Mungu anashida sana na hiyo pesa yako kwasababu kabla ya wewe kuwa nayo ni ya kwake na yeye ndiye alikufanikisha au alikupa sasa wawezaje kusema mtu aliyekupa kitu halafu yeye akawa maskini wa hicho kitu....


 Hagai 2:8

[8]Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi. 

Kumbe Sheria za Mungu ni kwaajili yetu wenyewe yaani

👉Ukiitunza Sheria ya Bwana ni kwaajili ya uzima wa nafsi yako na 

👉Usipoitunza si tu kwamba unamkosea Mungu bali unajiletea msiba kwa nafsi yako mwenyewe... 


Soma hapa 👇

Mithali 19:16

[16]Yeye aihifadhiye amri huihifadhi nafsi yake; Bali yeye asiyeziangalia njia zake atakufa. 

Na mtu anayeipenda nafsi yake basi ni lazima ampende na Mungu na ukiona humpendi Mungu (hushiki amri/ zake) basi hata wewe mwenyewe hujipendi kwasababu ungejipenda usingekubali kufanya jambo ambalo linaleta msiba kwako mwenyewe...


 Yohana 14:21

[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. 

Kumbe tunapokuwa na Sheria Za Mungu na tukazishika (tukazitenda) basi hiyo ndiyo maana ya kumpenda Mungu na kwa kufanya hivyo tu kulingana na Mithali 19:16, basi tunahifadhi nafsi zetu mbali na uharibifu (Mauti)....  Kinyume chake ni sawa utakuwa una haribu nafsi yako mwenyewe..... 


Mungu akubariki sana 


 Taifa Teule MinistryM

Minister mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?