UVUMILIVU UTAKUVUSHA TAABUNI

                 UVUMILIVU UTAKUVUSHA TAABUNI

Bwana asifiwe karibu tujifunze tena hapa

UVUMILIVU ni tunda la Roho ambalo ni lazima kila mtu wa Mungu alijue na awe nalo kwasababu linakufanya nafsi yako iwe na utulivu kwa Bwana hata kama unapitia taabu...

Tambua kwamba taabu ni sehemu ya maisha ya kila mtu, yaani
👉Kuna wakati wa kukosa na wakati wa kupata
👉Pia Kuna wakati wa kuwa chini,
👉wakati wa kudharauliwa,
👉 wakati wa kutenga,
👉wakati wa kukosa kazi n. K

Yaani hayo hayakwepeki... Lakini cha msingi ni kujua kwamba hayo yote yana muda fulani wala si ya kudumu..

Taabu zina uwezo wa kumfanya mtu kurudi
👉Wengine hurudi nyuma kwenye wokovu kwasababu wametafuta kazi kwa muda bila kupata wakaona kana kwamba Mungu wao hawaoni
👉Wengine huacha wokovu kwasababu tu ya magonjwa
👉Wengine hurudi nyuma kwa kukosa Mume au mke kwa muda mrefu
👉Wengine hurudi nyuma kwasababu ya njaa tu...

Lakini mambo hayo hayapaswi kabisa kututenga na Mungu...

Warumi 8:35
[35]Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?

Lakini watu hurudi nyuma kwa kushindwa kuvumilia...

Yakobo 5:10-11
[10]Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.
[11]Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.

Unaona hapo, biblia inasema tujifunze kwa manabii kuvumilia, kumbe hata watu waliotumwa na Mungu kwa ukubwa, pia walipitia taabu hizi za hapa duniani lakini walitengeneza na kuvaa vazi la uvumilivu wakavumilia...

Tunajua Ayubu alipitia kwenye taabu kubwa ya kufiwa na watoto wote, mifungo yote, na afya yake hata akabaki pekeyake lakini aluvumilia kwa kile kitambo na mwisho wake ukawa mzuri kuliko hata alivyikuwa mwanzo...

Naomba ujue kuwa
👉Kupitia taabu siyo kwasababu umemkosea Mungu
👉Si kwasababu Mungu hakuoni
👉Si kwasababu wewe hujasoma
👉Na si kwasababu wewe ni mvivu
 
BALI maisha yameundwa katika namna ambayo kila jambo baya na zuri linawakati wake na ndiyo maana Biblia ikasema Kuna wakati utatakiwa kuvumilia kama vile manabii na watu kama ayubu walivyovumilia...

Na pia ujue kuwa kutenda mema si sababu ya wewe kutokupitia taabu....

Na ndiyo maana Ayubu alikuwa mwenye haki lakini alipitia taabu

Ayubu 1:1
[1]Palikuwa na mtu katika nchi ya Usi, jina lake alikuwa akiitwa Ayubu; mtu huyo alikuwa mkamilifu na mwelekevu, ni mmoja aliyemcha Mungu, na kuepukana na uovu.

Kwahiyo tunda la Roho la uvumilivu inatengenezwa kwa kumuomba Mungu na kujizoeza katika kuvumilia magumu unayopitia..

Mungu hakuchukii, wala siyo mbaya kwako lakini magumu ni sehemu ya maisha ya kila mtu, na hata ukiyapitia isiwe sababu ya kukata tamaa na kurudi nyuma maana Mungu yupo pamoja na wewe na anajua hicho ni kipindi cha Muda fulani tu

Lakini ikiwa ni jambo la maisha yote hapo sasa tunaanza kutazama kwa jicho Lingine kujua kama Kuna jambo lisilokuwa kawaida kama vile roho ya kuchelewesha lakini kwa taabu za kawaida tu tambua ni kipindi cha kimaisha ambacho lazima kila mtu akipitie...

Mungu akubariki sana

@Taifa Teule Ministry
Minister Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?