SI KWAAJILI YA NDOA BALI NI ASILI YAKO MWANAMKE
Bwana asifiwe mabinti wa Mungu...
Leo naomba nikukumbushe juu ya sifa ambazo mwanamke anafaa awe nazo ili awe mwanamke mzuri .....
sifa hizi si kwasababu unahitaji kuolewa, au unataka kudumu kwenye ndoa...
sifa ambazo Unatakiwa kuwa nazo pia si zawadi au karama ambazo zinatoka kwa Mungu.... Bali ni nilitihada zako Binafsi na huku ukilifuata Neno la Mungu....
Neno la Mungu ndio msingi sahihi wa tabia au sifa ambazo Unatakiwa kuwa nazo... ziko nyingi Sana Lakini Leo tuangalie kadhaa...
1 Petro 3:3-6
" Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. Kama vile Sara alivyomtii Ibrahimu, akamwita Bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, wala hamkutishwa kwa hofu yo yote."
1.WEMA
sifa hii inafa kila mtu awe nayo maana kwa hii jamani, familia na hata kizazi kunaweza kuwa Salama..
Sasa KUMBUKA mwanamke ni kiungo kikubwa Sana mahali popote, hivyo akikosa kuwa mwema kwa wale wanaomzunguka basi mambo mengi yanaweza kwenda tofauti... hebub jiulize nyumba yenye mama mwanamke ambaye si mwema, inakuwaje kwa wafanyakazi wake??... mama asipokuwa mwema inakuwaje kwa ndugu wa mumewe??, mwanamke asipokuwa mwema Hali huwa mbaya mahali popote alipo... hata kama Mwanaume Hana wema kiasi fulani, basi mwanamke akiwa mwema hata ndani ya nyumba mambo yanaenda vizuri.... wema utakufanya uwapende watu, utakufanya uwahurumie wanaokuzunguka na kuwasaidia, wema unaleta upendo baina ya ndugu...
2.UPOLE
Katika somo la nyuma tuliona, mwanamke ana nguvu kubwa sana ya kujenga kitu au kuiibomoa kitu zaidi ya Mwanaume... sehemu yoyote ikiwa na mwanamke mpole basi ni lazima uwepo usalama.... upole siyo ukimya, mtu anaweza kuwa mkimya lakini asiwe mpole... mpole anakuwa na uwezo mkubwa Sana wa kuambiwa jambo fulani na kulitii hata kama anaona ni vigumu.. mwanamke akiwa mpole hautakuwa mtu wa kuwasema watu vibaya, masengenyo yataondoka, na atajua kufanya Yale yanayomuhusu kikamilifu, lakini pia upole utamfanya mwanamke kuachilia hata kama Kuna mtu kamfanyia vibaya.. kumbuka jambo akilitenda mwanamke lina madhara makubwa kuliko Mwanaume nahii ni kwasababu ya nguvu iliyopo ndani ya mwanamke... na ndiyo maana Biblia ikawaambia wanawake wawe wapole hata ndani ya ndoa zao..
3.UTULIVU
mwanamke Mwenye papala, asiye na utulivu, hafai katika kujenga Bai humoboa mambo.. kukosa utulivu kutakufanya ubebe mambo bila hekima na mwisho kuumia na kuumiza wengine... Mwanamke mtulivu hawezi kubeba mabaya ya mtu na kuyasambaza, hawezi kuanika siri za nyumbani kwake... Bali hulitatua Jambo/tatizo bila hata wengine kujua kwamba alikuwa na tatizo.. mwanamke mtulivu hulinda kinywa chake, si mtu wa kuongea kwa kila kinachokuja mbele yake , si mmbeya..
4. HESHIMA
Katika familia hata kama mwanamke ana pesa kuliko Mwanaume, hata kama amesoma kuliko Mwanaume, hatakiwa kuwa juu ya MUME wake, kama mwanamke ni bosi kazini kwake, basi akiwa nyumbani hautakiwi kuwa na akili ya ubosi wake Bali ajuye yeye ni mke wa mtu na anatakiwa kumuheshimu huyo Mwanaume bila kujali ameokoka au hajaokoka... hata kamani mrembo hutakiwi kutumia urembo kama sababu ya kumsumbua MUME wako, kumtishia kwamba unaweza kwenda kwa Mwanaume mwingine kama hatakutimizia jambo fulani... kama MUME hana kile unachokitaka kwa wakati huo basi isiwe sababu ya kumdharau Bali endelea kumuheshimu kwasababu maisha ya mabonde, tambarare na milima pia...
5. USAFI
Mwanamke ni lazima awe msafi... mwanamke hufananishwa na mapambo... yaani sehemu ikikosa mwanamke huwa haipendezi kama Akiwepo... Sasa lazima uweke akilini kwamba ili mapambo yapendezeshe sehemu yenyewe kwanza yanatakiwa yawe yanapendeza yaani yawe masafi.... mwanamke akiwa mchafu hapendezwi kabisa ndani ya nyumba, kwenye jamii na popote pale anapokuwepo... kabla hujaanza mizunguko ya kimaisha, unapoenda kwenye mwingiliano na watu, usisahau japo kwa muda mfupi kukaa mbele ya kioo chako kujitaza na kuona kwamba unapendeza au la! ... wanaume wanaweza kutoka bila hata kujua kioo Kiko wapi lakini kwa mwanamke haipendezi... hata kama umeokoka siyo sababu ya kuwa wa kawaida Bali jiweke vizuri, si kwasababu unahitaji kuolewa au kudumisha ndoa yako Bali ni sifa ya mwanamke bora kuwa msafi....
na nyingine nyingi ...........
Mungu akubariki Sana
Ladies In ChristMinister Mathayo Sudai
Maoni
Chapisha Maoni