KAMA BWANA ASINGALIKUWA MSAADA WANGU....

KAMA BWANA ASINGALIKUWA MSAADA WANGU....

Min. Mathayo Sudai

Bwana asifiwe wana wa Mungu Karibu tujifunze neno la BWANA

Tuanze hivi👇

Zaburi 94:17
[17]Kama BWANA asingalikuwa msaada wangu,
Nafsi yangu kwa upesi ingalikaa penye kimya.

Ulimwengu huu umejawa na mambo mengi sana ya ajabu ambayo yanalenga kuangamiza nafsi za watu, na kuwatoa watu nje ya makusudi ya Mungu...

Kimsingi Mungu wetu ni mwaminifu kwasababu huilinda nafsi ya kila mtu mwenye dhambi na hata aliyeokoka na ndiyo maana watu wote hao wapo duniani....

Ni kweli kabisa kwamba kama Mungu asingekuwa anamlinda mtu basi wanadamu wangeshawekwa palipo na kimya (mautini)...

Hapo Daudi anakiri kwamba kuishi kwake yeye ni Mungu tu na kama isingekuwa hivyo basi yeye asingekuwepo yaani angeshakufa muda mrefu..

Si Daudi tu, unaweza kujiangalia wewe mwenyewe hapo ukaelewa kwasababu
👉Kama si mkono wa Mungu uliokuvusha kwenye ile kesi basi muda huu huenda ungekuwa jera
👉Kama si Mungu kuwa upande wako pengine ungeuawa kwenye ule wizi ulioufanya...
👉Ungekufa ile siku umetoa mimba....
👉Ungeshakufa pengine kwa ule ugonjwa uliokupata...
👉Ungekuwa kaburini pengine kwa ile ajali uliyopata
👉Ungekuwa muathirika wa ukimwi kwa jinsi ulivyokuwa na tabia mbovu ya zinaa pale mwanzo
👉Pengine ungekuwa unateswa na kutumikishwa na kuzimu muda huu....

Lakini Mungu alikutetea na anakutetea si kwasababu alipenda uovu wako lakini ni kwasababu anakupenda wewe na hapendi upotee...

2 Petro 3:9
[9]Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu ye yote apotee, bali wote wafikilie toba.

Katika magumu yote na matatizo yote ambayo uliyapitia ni dhahiri kabisa kwamba kama si Bwana Yesu kukupigania basi usingekuwa hapo ulipo..

👉Wengine wamepewa kazi na wanapata fedha basi lazima ujeu ni neema ya Mungu wala si akili zako na yote ni kwasababu Mungu anakuhitaji... Na katika hilo ni hatari sana kama utamuacha Mungu baada ya kuwa umefanikiwa  kwasababu kwenye maisha yangu binafsi nimeona wengi wakiwa wanyenyekevu na walikuwa wanamuomba sana Mungu wakati wanatafuta lakini walipopata walimsahau Mungu na wala maombi hayapo tena na wamekuwa wa ajabu, wajuaji kana kwamba wamejipa wenyewe hicho walichonacho....

Kumbukumbu la Torati 8:12-18
[12]Angalia, utakapokuwa umekula na kushiba, na kujenga nyumba nzuri na kukaa ndani yake;
[13]na makundi yako ya ng’ombe na kondoo yatakapoongezeka, na fedha yako na dhahabu yako itakapoongezeka, na kila kitu ulicho nacho kitakapoongezeka;
[14]basi hapo moyo wako usiinuke, ukamsahau BWANA, Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa;
[15]aliyekuongoza katika jangwa lile kubwa lenye kitisho, lenye nyoka za moto na nge, nchi ya kiu isiyokuwa na maji; aliyekutolea maji katika mwamba mgumu,
[16]aliyekulisha jangwani kwa mana, wasiyoijua baba zako; apate kukutweza, apate kukujaribu, ili kukutendea mema mwisho wako.
[17]Hapo usiseme moyoni mwako, Nguvu zangu na uwezo wa mkono wangu ndio ulionipatia utajiri huo.
[18]Bali utamkumbuka BWANA, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo.

Kila hatua utakayopiga lazima ujue kwamba kama si Mungu basi usingekuwa hapo...

Hatari ya kukshindwa kumuheshimu Mungu na kumsahau baada ya kupata ni hii hapa👇

Kumbukumbu la Torati 8:19
[19]Lakini itakuwa, kama ukimsahau BWANA, Mungu wako, na kuiandama miungu mingine, na kuitumikia na kuiabudu, nawashuhudia leo ya kuwa mtaangamia bila shaka.

Tambua kila kitu ambacho Mungu huwa anampa mtu kama majibu ya maombi yake huwa kipo ndani ya mapenzi ya ajenda zake Mungu, na Mungu hawezi kujibu mtu au kumpa mtu kitu ambacho kipo nje ya mpango na mapenzi yake...

1 Yohana 5:14
[14]Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia.

Mungu akukusikia basi anakujibu.. Kumbe kujibiwa kunaambatana na mapenzi yake...

Maana yake kila ulichonacho ni kwamba Mungu alikupa kwasababu ya kutumika sehemu fulani, au kwa jambo fulani... Yaani Kuna kusudi kwa kila akupacho Mungu.. Kumuacha yeye na kujifanya kana kwamba ni akiri na nguvu zako basi utapotea kwasababu umeyakimbia na kushindana na mapenzi ya Mungu....

JIFUNZE kusema kama si Mungu mimi nisingekuwa hapa nilipo..
Kama si Mungu aliyekuwa Nami nisingekuwa hivi nilivyo...

Hata kama bado hujapata unachokiomba, Endelea tu kutembea kwenye mapenzi ya Mungu, tembea kwenye kanuni za Mungu halafu utaona baadae katika wakati wa BWANA,... Mungu atakutendea makuu...

Mungu akubariki sana

Minister Mathayo Sudai
0744474230

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA