TAFUTA KUKUA, USIRIDHISHWE NA SHETANI

TAFUTA KUKUA, USIRIDHISHWE NA SHETANI

Na:Minister Sudai

Bwana Yesu asifiwe sana watu wa Mungu, karibu tujifunze kitu cha msingi kuhusu kukua kiroho...

Soma hapa👇

Wakorintho 13:11
[11]Nilipokuwa mtoto mchanga, nalisema kama mtoto mchanga, nalifahamu kama mtoto mchanga, nalifikiri kama mtoto mchanga; tokea hapo nilipokuwa mtu mzima, nimeyabatilisha mambo ya kitoto.

Hapa Paulo anazungumza jinsi ambavyo unapaswa kuwa na utofauti kwa jinsi ulivyokuwa mtoto na ulivyo Leo...

Jambo hili ni la kulitazama zaidi kwa mambo ya rohoni kwasababu kabla hujawa mtu Mzima kiroho ni lazima uwe mtoto na si ajabu biblia inalithibitisha hilo.....👇

Waebrania 5:13-14
[13]Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.
[14]Lakini chakula kigumu ni cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.

Unaona hapo...??

Mtu mzima si mtu aliyeokoka muda mrefu au Ana umri Mkubwa bali kunahusisha sana jinsi anavyoenenda kwa mambo ya kiroho...

Kama umeokoka lakini
👉Bado unamchukia mtu
👉Bado Huna upendo
👉Bado unalazimishwa kwenda kanisani
👉Bado unaitamani dhambi na kuifanya
👉Bado unaishi kwenye michanganyo
👉Bado Huna mahusiano na neno la Mungu
👉Bado unapenda kuyafanya yale uliyoyaacha zamani
👉Bado unona utakatifu kuwa ni ushamba
👉Bado huna ujasiri wa kusema umeokoka mbele za rafiki zako
👉Bado hupendi kuonekana tofauti na dunia

BASI jua wewe ni mtoto kiroho, kwasababu akili yako kwa kutenda haijui kupambanua jema na baya...

Lazima ujue Kuna namna ambavyo mtoto anaishi na Kuna namna ambavyo mtu mzima anaishi,
👉Usiishi kama ulivyokuwa unaishi mwaka jana
👉Usiombe kama ulivyokuwa unaomba mwaka jana

Ishi maisha ya kiroho ambayo yanaonyesha ukuaji kiroho, na ndiyo maana hapa Paulo aliwaambia Waebrania kitu...

Hebu soma hapa..👇

Waebrania 5:12-13
[12]Kwa maana, iwapasapo kuwa waalimu, (maana wakati mwingi umepita), mnahitaji kufundishwa na mtu mafundisho ya kwanza ya maneno ya Mungu; nanyi mmekuwa mnahitaji maziwa wala si chakula kigumu.
[13]Kwa maana kila mtu atumiaye maziwa hajui sana neno la haki, kwa kuwa ni mtoto mchanga.

Kwa hiyo kulingana na walivyokuwa wana muda mwingi kwenye wokovu ilitegemewa wawe katika kiwango fulani cha kiroho cha kuweza kujihusisha na mambo makubwamakubwa kiroho lakini cha ajabu walikuwa ni kama watu waliookoka jana...

Walipotakiwa kusimama kama wasimamizi wa wengine lakini ilionekana bado na wao wanahitaji kusimamiwa na kufundishwa mafundisho ya awali yaani mafundisho ya kuukulia wokovu.....

Kimsingi hata Mungu anahitaji watu wake wakue kiroho hata wafikie utimilifu na hata kimo cha kristo na ndiyo maana akaweka watumishi wake kwa lengo la kuifanya kazi hiyo....

Waefeso 4:11-13
[11]Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu;
[12]kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe;
[13]hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;....

Dalili za mtu kuwa mchanga kiroho ni kama vile👇

👉Hapendi kufunga na kuomba
👉Kufunga na kuomba mpaka asikie tangazo kanisani, kwasababu yeye binafsi hajui maana na kazi ya kufunga na kuomba
👉Michanganyo
👉Ni mtu wa kiburi, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho
👉Anaweza kumkana Mungu kwa matendo yake kwa kitu kidogo sana, kwa starehe ya muda mfupi sana, kwa shida ndogo anayopitia... Nilishawahi kuona wakristo wakicheza disko kwasababu kulikuwa na SHEREHE, hivyo wakamsahau Mungu kwa muda ule mfupi na sherehe ulipoisha wakamrudia Mungu tena
👉Hana muda na mambo ya Mungu anachojua yeye ni kuingia kanisani jumapili na akishatoka basi anasubiri hadi jumapili nyingine tena
👉Anaweza na ni rahisi sana kushirikiana na Mungu na Shetani kwa wakati mmoja
👉Si mjuzi wa mambo ya kiroho....

Ukiendelea kuwa mchanga kiroho basi shetani atakuwa anakusumbua sana kwa uchanga wako na kwa kutokujua kwako, lakini pia Kuna vitu fulani hutakuwa na uwezo wa kushindana navyo, hivyo mambo mengi ya kifamilia, kibinafsi, kikanisa hutakuwa na uwezo kuyashughulikia kwasababu wewe ni mtoto....

Tamani kukua kiroho na usikubali uongo wa shetani anayekwambia kwamba hivyo hivyo ulivyo ni sawa tu na Huna haja ya kujisumbu ili kumtafuta Mungu na kukua kiroho....

Tafakari hilo chukua hatua..

Mungu akubariki sana..

@Taifa Teule Ministry
Minister Mathayo Sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

WANAWAKE 21 KATIKA BIBLIA NA MAHUDHUI YAO

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

TOFAUTI KATI YA DHAMBI UOVU NA MAKOSA