KWEPA FITINA KWA UPENDO
KWEPA FITINA KWA UPENDO Bwana asifiwe karibu tujifunze tena asubuhi ya Leo.. Biblia Inaweka wazi jinsi ya kukimbia fitia au kuikwepa miongoni mwa watu... Haebu soma hapa 👇 Mithali 10:12 [12]Kuchukiana huondokesha fitina; Bali kupendana husitiri makosa yote. Kumbe kama chuki Inasababisha kuwe na FITINA basi njia sahihi Kwa hapa ni Kutokuwa na chuki kati au baina ya watu... Kukiwa na chuki miongoni mwa rafiki, kikundi au watu basi haya yaweza kutokea... 👉Kila mtu atatamani kumchafua mwenzake ili afunge kibali chake 👉Kila mtu hatamuona mwingine kama msaada bali adui 👉Kila mtu atamtazama mwenzake kama chanzo cha huzuni yake 👉Moyo wa mtu na mtu wanaochukiana huwa hauwezi kukaa pamoja 👉Hakuna mtu atakuwa tayari kumsaidia mwenzake 👉Watu hawa wanaweza kushindwa kukosa fursa kwasababu mara zote fursa inayotengenezwa na Mungu huja kwa mtu kupitia watu Na mbaza nyingine ni kwamb...