IJUE MITHALI 18:24
IJUE MITHALI 18:24
Bwana Yesu asifiwe... Leo tuangalie mstari huu wa Mithali 18:24 tujue Mungu anasema Nini kupitia eneo hili kwenye maisha yetu....
Soma hapa....
Mithali 18:24
Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.
hapo Kuna mambo mawili ya msingi sana ambayo inatakiwa tuyajue...
1. kujifanyia rafiki wengi...
katika jamii au maisha Kuna kitendo cha mtu kupata au kuwa na mtu mwingine wa karibu yaani rafiki... katika hili inatakiwa kuelewa kwamba kila mtu ambaye utamruhusu aingie kwenye maisha yako kama rafiki basi jua ana mchango fulani kwenye maisha yako ..(ana influence fulani)... na sehemu kubwa ya shida au matatizo watu wengi wanapitia ni kwasababu ya rafiki zao au aina ya watu walioambatana nao yaani 75% ya shida watu hupata kutokana na watu waliowaweka Katibu Yao.....
👉wengine huingizwa kwenye makundi mabaya na rafiki zao
👉wengine hufundishwa njia ya kuishi na rafiki zao..
👉wengine hushawishiwa kufanya jambo hata hakuwahi kufikiri kama anaweza kulifanya
👉Lakini pia wapo wengine wamefaikiwa kulingana na aina ya rafiki walionao....
usipojua Siri ambayo ipo kwa rafiki au watu unaombatana nao basi utakosa busara na kujikuta unaambatana na kila mtu kwenye maisha yako jambo ambalo ni HATARI kwa wewe Binafsi...
watu hubeba vipindi na majira hivyo kuwa makini na ujue kuwa kila utakayemfanya awe karibu yako basi anakuingiza kwenye majira mapya ambayo yanaweza kuwa mazuri au mabaya...
zungumza na uwe na amani na watu wote lakini usimfanye kila mtu awe rafiki yako, watu hubeba vitu...
Yesu alisema tupendane wote had wale ambao ni adui zetu lakini hakusema tuambatane na wote, kwenye kuambatana alisema kupitia mtume Paulo kwamba ...
2 Wakorintho 6:14
Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
kwahiyo hapo ametuonyesha ni aina gani ya rafiki unapaswa kuwa nae...
pia hata kama Kuna watu unawaona kuwa wameokoka hiyo nayo si sababu ya kuwafanya wawe rafiki zako... ninyi ni ndugu katika Kristo lakini si rafiki....
2.Kuna rafiki ambaye ni zaidi ya ndugu
Katika hili ni lazima tujue kwamba kwa sehemu Kuna ndugu ambao wanaleta madhara kwako kuliko rafiki ....
Kuna ndugu ambao wanafanyika CHANZO cha maumivu ya mtu kuliko mtu mwingine... sasa, undugu nao siyo sababu ya mtu kuwa rafiki yangu kwasababu Kuna rafiki ambaye anaweza kuwa mzuri kuliko ndugu yako...
👉si kila ndugu Unatakiwa kufanya naye Biashara
👉si kila ndugu Unatakiwa kufanya naye ushirika katika maisha yako...
👉si kila ndugu anatakiwa kuyasogelea maisha yako....
" Linda Sana mtu anayesogea au kumuingiza kwenye maisha yako kwasababu watu wamebeba vitu na vitu vinaweza kuwa vibaya au vizuri ... kuwa makini"
Mungu akubariki Sana
Minister Mathayo Sudai
Taifa Teule Ministry
Maoni
Chapisha Maoni