IJUE MAANA SAHIHI YA KUPENDA
IJUE MAANA SAHIHI YA KUPENDA...
Bwana asifiwe... njoo tujifunze kitu kuhusu upendo hapa na jinsi ya kujua kama una upendo....
UPENDO ni jambo la kiroho, kimwili, kihisia na kimatendo lililopo kati ya watu..
MATENDO huambatana na Hali na MATENDO mbalimbali kama vile
👉kuhudumiana,
👉 kuthaminiana,
👉kutii,
👉kujali na
👉kuwa tayari kuwa pamoja katika mapito mbalimbali...
UPENDO haupo mdomoni tu, yaani isiishie kusema una upendo Bali inatakiwa ufikie hatua ya kuuonyesha upendo...
kwamfano...
tunapokuwa tunasema tunampenda Mungu, haitakiwi kutamka tu Bali upendo wa Mungu ni kuzishika amri zake yaani kufanya sawasawa na maagizo ya Mungu.... ( MATENDO lazima yahusike )
Yohana 14:21
[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
unaona hapo kumbe kumpenda Mungu siyo lazima useme au umwambie Mungu, Bali kitendo Cha kushika Sheria zake na kutenda sawasawa na amri hizo basi yeye anakutaza kama mtu unayempenda...
KUMBE
"UPENDO hausemwi mdomoni, Bali unaonyeshwa".
na ndiyo maana Biblia inasema...
1 Yohana 3:18
[18]Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.
tukisoma hapo tunaona kuwa biblia inaweka bayana kwamba upendo hautakiwi kuwa kwa kutamka tu, Bali lazima yawepo matendo..
kumbuka Mungu hawezi kukwambia ufanye jambo ambalo yeye hawezi kulifanya na ndiyo maana yeye mwenyewe alionyesha Nini maana ya upendo....
Yohana 3:16
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
unaona hapo hakuishia kutupenda lakini aliudhihirisha upendo kwa tendo la kumtoa mwanae wa pekee...
hii ikusaidie kujua kwa.....
"Ni heri mtu anyekufanyia matendo ya upendo bila kumwambia anakupenda, kuliko yule anayekupa maneno ya upendo bila matendo"
lakini sambamba na Hilo, moyo wako pia lazima uhusike kwasababu kumsaidia mtu tu, au kumfanyia mtu jambo zuri na moyo wako kuwa mbali na MATENDO yako pia si upendo huo....
na ndiyo maana Biblia inasema hivi...
1 Wakorintho 13:3
[3]Tena nikitoa mali zangu zote kuwalisha maskini, tena nikijitoa mwili wangu niungue moto, kama sina upendo, hainifaidii kitu...
hapa tunaelewa kwamba upendo lazima uanzie moyoni Kisha ujifhihirishe kwa MATENDO na huo ndiyo mtu anahesabiwa kuwa na upendo...
KUMBE
👉maneno pekee siyo upendo
👉kumbe kupenda kunapimwa na MATENDO yanayoambatana na moyo....
👉Haitoshi kumwambia Mungu au kusema unampenda, Bali Unatakiwa kufanya analokuagiza kuanzia moyoni mwako...
Ndugu, jifunze kupenda kama vile Mungu alivyokupenda....
je una upendo wewe au una maneno ya upendo ambayo hayamsaidii kitu......?????
TAFAKARI, na Kisha simama katika upendo w kweli....
Mungu akubariki
Taifa Teule Ministry
Minister Mathayo Sudai
Maoni
Chapisha Maoni