MWANAMKE, USIKAE KINYONGE WEWE SI DHAIFU

MWANAMKE, USIKAE KINYONGE WEWE SI DHAIFU

Na: Minister Mathayo Sudai 

Bwana asifiwe mabinti Safi wa Yesu...

Kuna mambo mengi Sana huwa yanafanyika katika Dunia hii na mwanamke huwekwa katika nafasi ya mwisho jambo linalopelekea kusomeka kama mtu ambaye ni dhaifu ...

lakini vile mambo yanavyoenenda mara nyingi katika Dunia hii iliyoaanguka huwa ni kinyume kabisa na vile ambavyo Mungu anatazama na kutamani...

KIMSINGI

👉Mwanamke ni imara kuliko Mwanaume

👉Mwanamke ana msimamo na si rahisi kukata tamaa zaidi ya Mwanaume

👉Wanawake Wana nguvu Sana kuliko na jinsi wanavyotazamwa...

👉Mwanamke Akiwepo nyumbani basi hata mgeni akifika anajua kwamba nyumba ina mwanamke....

na jambo la msingi ni kwamba katika Dunia hakuna Mwanaume hata mmoja anayeweza kumjua kiundani mwanamke... hayupo .. kwasababu mwanamke ni fumbo.... (Mwanzo 2:21)

👉mwanamke ni lango la baraka fulani kutoka kwa Mungu ambazo Mwanaume hataweza kupata mpaka atakapokuwa amemuoa  mwanamke huyo.... 


Mithali 18:22  

Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.


👉mwanamke ndiye Mwenye uwezo wa kujenga familia au kuibomoa na si Mwanaume ( MITHALI 14:1-2 )

kumtaja mwanamke kama kiumbe kisicho na nguvu si sauti ya Mungu Bali SHETANI huhitaji kuangamiza kizazi na njia pekee ni kumdhoofisha mwanamke...


tambua kwamba wewe si dhaifu, na unaweza kufanya mambo makubwa Tena kwa wakati mwingine zaidi ya Mwanaume.... japo ni ngumu kulipokea Hilo kwasababu ya dhana uliyojengewa lakini simama imara, kama una maono yako yafanye kwa nguvu zote kama wengine, na usiweke akilini mwako kwamba bila Mwanaume Huwezi kitu....


yajue haya👇

👉Mungu alipotaka kujidhihilisha Dunia alipita kwa mwanamke

👉Aliyemuandaa Yesu kwakumpaka marhamu kichwani alikuwa mwanamke

👉Mtu wa kwanza kufanya uinjilisti ndani ya Biblia alikuwa mwanamke

👉mtu wa kwanza kumuona Yesu alipofufuka alikuwa mwanamke...


unaweza kuniambia ni pionti gani inayokufanya ujione dhaifu angali Mungu amekuona kuwa ni shujaa na kukupa kipaumbele kwenye hayo yote??


Wewe ni shujaa .... 

wewe ni jeshi kubwa ...

wewe ni shupavu.....

wewe ni silaha ya Mungu .....


Mungu akubariki Sana


ladies In Christ

Minister Mathayo sudai

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI