Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2023

MSAADA WETU U KATIKA JINA LA BWANA MUNGU WA MAJESHI

Picha
  MSAADA WETU  U  KATIKA JINA LA BWANA MUNGU WA MAJESHI Zaburi 124:6-8 [6]Na ahimidiwe BWANA;  Asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao. [7]Nafsi yetu imeokoka kama ndege  Katika mtego wa wawindaji,  Mtego umevunjika, nasi tumeokoka. [8]Msaada wetu u katika jina la BWANA,  Aliyezifanya mbingu na nchi. Bila Mungu hatuwezi kujipambania wenyewe anayetupigania ni Mungu pekeyake Wala hivi tulivyo si kwasababu ya hirizi au uganga fulani no no. ooooh watu wa Mungu tunajivunia kwasababu tunalindwa na nguvu za Mungu.  Ni hatari sana kuona mkristo unateswa na wachawi na waganga  leo sema nalindwa na nguvu za Mungu, hivyo hakuna uganga wala uchawi juu ya maisha yangu.  ISHI KWA IMANI SIKU ZOTE SEMA ATAKAYE KUNIDHURU MIMI NA FAMILIA YANGU KATIKA JAMBO LOLOTE AUSHINDE KWANZA MSALABA WA YESU AKIWEZA NDIPO TANIWEZA MIMI Unajua shetani kazi yake ni akutese tu,  akiangalia Huwezi hata kumshughulikia katika ulimwengu wa Roho utakuta unaanzisha kabiashara kako anawafukuza wateja, anapiga mpaka mtaji nao mwee

BINTI USIKATE TAMAA, MUNGU ANATENGENEZA LOVE STORY YENYE MVUTO

Picha
  BINTI USIKATE TAMAA, MUNGU ANATENGENEZA LOVE STORY YENYE MVUTO Bwana Yesu asifiwe mabinti wa kristo Leo naomba tujifunze jambo ambalo lina nguvu ya kurejesha tumaini kwa mabinti wengi ambao huwa wanaingia kwenye kipindi cha kukata tamaa. 👉Ni kweli kwamba watu wengi kulingana na kawaida ya ulimwengu huu na dunia tunayoishi ,,kuweka vichwani mwao muda na majira ambayo yakifika ni lazima awe ameshaolewa na inaposhindikana kwa wakati huo wengi hukata tamaa. 👉Kukata tamaa kwa Mwanamke kwenye kipindi hiki siku zote husababisha Maumivu na pengine matatizo makubwa sana kwa binti huyo kwasababu huwa katika hali ya kufanya maamuzi ya ambayo yanalenga kile kinachomuumiza akili yake wakati wote ( kuolewa ). 👉Lakini leo nakuja kwako binti na ujumbe huu wa kuiponya nafsi yako na pengine hata maisha yako yasiharibiwe. 👉Ni lazima uwe na akili na mawazo ya juu zaidi kuliko kutumia mtazamo wa chini wenye Maumivu kwako. 👉Je umesahau kwamba silaha mojawapo ya Mungu anayoipenda na kuitazamia kwa wat

KUWA MAKINI NA AINA 02 ZA WANAUME

Picha
KUWA MAKINI NA AINA 02 ZA WANAUME   Bwana Yesu asifiwe mabinti wa kristo Leo naomba jifunze jambo moja kuhusu wanaume ambao kama binti ni lazima watakuja kwako. 👉Binti anapofika katika kipindi cha wanaume kumfuata, na kipindi ambacho yupo tayari kuolewa basi ni lazima atafatwa na wanaume wa aina mbili. 1: Mwanaume mwenye kupenda na kuwa na haja ya kuoa 2: Mwanaume ambaye atakuja kwa lengo la kupumzika na kutuliza hisia zake kwa kitambo tu 👉Hawa ni watu wawili ambao kuna wakati wanaweza kuja kwako binti kwa maneno na ahadi zinazofanana. 1c ANAYEHITAJI KUOA huyu ni mwanaume ambaye huwa na uhitaji wa kupata mke/Mwenza na anapokuja nyuma yake huwa amebeba mapenzi ya Mungu, pengine bila hata ya yeye kujua 👉Hata kwa watu ambao hawajaokoka ni lazima ujue hata wao pia, mtu anapokuwa na ajenda ya kupata mwenza basi amebeba ajenda nzuri ya Mungu bila hata kujua (ana jambo la kimungu ). 👉Hapa sina maana ya kwamba mpagani anaweza kumuoa binti aliyeokoka bali ninaweka tu ule msingi wa nini Mung

KITABU CHA SHERIA KISIONDOKE KINYWANI MWAKO......

Picha
  KITABU CHA SHERIA KISIONDOKE KINYWANI MWAKO...... Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu  Leo naomba kila mtu ajifunze jambo hili la msingi sana kwa ajili ya maendeleo yake na mafanikio yake binafsi. Ni kwa habari ya neno la Mungu, sheria za Mungu, au mapenzi ya Mungu ambayo tunayapata kutoka mahali yaliyoandikwa yaani Biblia. Ikumbukwe kwamba kuna namna ambayo Mungu alikuwa anatembea na Musa katika safari ya wana wa israeli 👉Alitembea naye kwa viwango vya juu hata Musa kumuona Mungu kwa umbo lake  👉Lakini hii yote ni kwasababu Musa alikuwa ametii maagizo ( neno ) la Mungu kwa ukamilifu na hivyo aliyajua mapenzi ya Mungu. Soma hapa👇 Hesabu 12:7-8 [7]Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa;  Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote; [8]Kwake nitanena mdomo kwa mdomo,  Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo;  Na umbo la BWANA yeye ataliona.... Kwahiyo hayo yote ni kwasababu Musa alikuwa amelishika sana neno la Mungu ( sheria ya Mungu), na hii ndiyo ilimfanya kutembea katika ulimwengu wa roho

BINTI USIWE PETE PUANI KWA NGURUWE

Picha
  BINTI USIWE PETE PUANI KWA NGURUWE Bwana Yesu asifiwe mabinti na wanawake ndani ya Kristo. Leo naomba tujifunze thamani ya mwanamke na jinsi inavyopotea pale tu anapokosa akili. Kumbuka Mwanamke ni mtu ambaye amebebeshwa dhamana ya nyumba au familia kama msaidizi wa Mume 👉Hivyo mtu huyu anategemewa kuwa makini zaidi ili kupinga na kulinda dhidi ya kile kinachoitwa uharibifu. Mara nyingi Mungu amewatumia wanawake wenye akili tu si wanawake tu kwasababu ya jinsia zao. 👉Kwenye ustawi wa eneo lako au nyumba yako, ndoa yako n.k haihitaji jinsia tu bali inahitaji akili ya mtu mwenye jinsia yako Ni lazima ujue kuwa unatakiwa kuwa na akili ya ziada ili tu kuziba mianya na matatizo ambayo pengeni yanaweza kuamka ndani ya familia yako. 👉Tena ni lazima ujue kuwa mwanamke mwenye akili ni simba jike aungurumaye kuweka mazingira yake katika usalama. 👉Kila mwanamke ambaye hana akili ni lazima familia, ndoa, na majukumu yake yatamshinda kwasababu ya kukosa kile kinachoitwa hekima na mwongozo . H

MWENYE HAKI ATASHIBISHWA MEMA NA MUNGU

Picha
  MWENYE HAKI ATASHIBISHWA MEMA NA MUNGU Isaya 54:14 [14]Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia. Shalom. Ili uhesabiwe haki lazima uwe thabiti na Mungu, umjue Mungu hasa. (Ayubu 22:21) Mungu anaposema  utathibitika katika haki,  maana yake, haki yake Mwenye haki itamthibitisha mahali popote. Wewe Mwenye haki hupaswi  kuishi maisha ya kuonewa , alionewa Yesu ili sisi tuwe na ujasiri Aliteswa ili sisi tuwe huru. Mwenye haki usitaabishwe na dhambi , Usitaabishwe na Mambo ambayo unajua kabisa ni haki yako kuwa nayo lakini huna kwa Sasa. Jua kabisa kwamba haki yako ipo palepale  ila ni suala la Muda tu Muda wako ukifika Wala hakuna atakayesimama kuzuwilia baraka zako. Hanna alikuwa Mwenye haki na alikuwa na sifa za kuzaa lakini wakati tumbo lake limefungwa ulikuwa si wakati wake, tunaona wakati wake ulipofika alifunguliwa na Bwana akampa kicheko. Mwenye haki  ni jasiri si Kama wao,  Bali Kama Mwenye haki. Mungu hum

MUNGU YUPO NA WEWE USIOGOPE.

Picha
  MUNGU YUPO NA WEWE USIOGOPE. Yeremia 1:5-7 [5]Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. [6]Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto. [7]Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Yeremia alikuwa ni nabii wa Mungu, ambaye alifanikiwa Kuanza huduma ya kumtumikia Mungu akiwa na umri mdogo Sana ( alitumwa na Mungu mwenyewe.) Oooh Kumbe udogo wa umri / Miaka uliyonayo siyo kigezo Cha wewe kutokujua Siri za Mungu aliye hai na kutafuta namna ya kumtumikia Mungu ingali bado una nguvu sasa. Usisubiri mpaka ukiwa mzee ndipo utumike ,mtumikie Mungu Sasa. Angalia Mungu anamwambia Yeremia kwamba ; Tazama kabla sijakuumba tumboni nalikujua, Tena kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, Tena nimekuweka kuwa nabii wa mataifa mengi. maana Yake hakumfanya kuwa mtumishi wa watu wachache pamoja na u

NAFASI YA MUNGU KATIKA MAOMBI/MIPANGO YANGU

Picha
NAFASI YA MUNGU KATIKA MAOMBI/MIPANGO YANGU Bwana Yesu asifiwe watoto wa Mungu  Karibu katika ujumbe huu👇 👉Katika Maombi / Mahitaji yetu tunayoyaomba kila wakati kwa Mungu, Wakati mwingine kuna mambo ambayo tunayataka na kuyaomba lakini mambo hayo yamebeba kusudi la Mungu pasipo sisi kujua. Tunaweza kusione mpenyo au majibu mpaka pale tutakapoyaomba katika njia sahihi inayoendana na matarajio ya Mungu katika mambo hayo. Mfano : Hanna alitamani kupata mtoto kwa muda mrefu, lakini Alikuwa amefungwa tumbo lake. Kilichomfanya atamani zaidi na wakati mwingine kumuomba Mungu ni kwasababu ya mke mwenzake ambaye alikuwa anamcheka, na kumdhihaki. Si jambo la Kupinga kuwa Hanna alitaka mtoto ili aweze kumfunga mdomo mke mwenzake.  Pia alitamani amfurahishe mumewe na apate amani katika nyumba yake.  Lakini vipi kuhusu Mungu? Mungu alikuwa na kusudi juu ya uzao wa Hanna, ukizingatia Eli na watoto wake walishaharibu, Mungu alitaka kuinua kuhani mwingine. Tunajua Utumishi wa Mungu hauji tu kawaida

SEMA HIVI 👇 KESHONI

Picha
  SEMA HIVI 👇 KESHONI Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu Leo naomba tuangalie namna Mungu anavyihitaji kuutumia ugumu wetu wa maisha na vifungo vyetu ambavyo tulikuwa navyo. 👉 Ni lazima ujue kuwa Mungu anavyomuokoa mtu, hamtazami mtu mmoja tu bali kundi kubwa la watu, familia nzima ,kizazi kizima, taifa zima na hata ulimwengu mzima. 👉Na jambo hili alilisema mwenyewe alipowaokoa watu fulani hivi Tusome hapa 👇 Kutoka 13:14 [ 14]Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake; Ukianza kwanzia mistari ya nyuma kidogo kwenye Biblia yako, utagundua kuwa Mungu alikuwa akizungumza kwa habari ya kumweka wakfu mzaliwa wa kwanza, lakini mstari wa 14 ndipo akatoa kusudi lake la ukombozi wa wana wa israel kwa kizazi cha kesho. 👉Kumbe hakuwatoa utumwani kwa ajili yao tu bali na kizazi kujacho 👉Kumbe Mungu anatenda jambo kwa kuangalia mbele zaidi kuliko leo 👉Kumbe hakutaka kuwaweka huru

USIMDHARAU UNAYEMDHARAU

Picha
  USIMDHARAU UNAYEMDHARAU Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu Leo ni siku nyingine naomba tujifunze jambo la msingi kwa jinsi ya kuishi katika usalama pamoja na wale wanaoonekana kuwa ni wanyonge. Biblia inasema hivi👇 Mithali 22:22-23 [22]Usimnyang’anye maskini, kwa kuwa ni maskini;  Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni; [23]Kwa sababu BWANA atawatetea;  Naye atawateka uhai wao waliowateka . Kuna watu wengi huwa wanapokuwa katika nafasi fulani, kazi fulani, cheo fulani au kuwa na kitu chochote ambacho wengine ( maskini) hawana...basi huwa ni kama fimbo ya kuwapigia wenzao. 👉Unapoishi katika maisha yako pamoja na baraka zote apizokubaliki Mungu basi Usimnyang’anye haki ya maskini kwa kudhania kuwa ni maskini hawezi kukufanya lolote. 👉Pia Biblia inasema USIMDHULUMU... 👉Sasa ni lazima ujue kuwa unapokuwa katika nafasi yoyote ile ya mafanikio ya namna fulani, jitahidi sana usije ukafikiri labda wewe ni bora kuliko wengine au wewe ni wathamani kuliko wale wasipokuwa nacho. 👉Kuna watu weng

UKIWA MMOJA HUWEZI..

Picha
  UKIWA MMOJA HUWEZI.. Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. Leo naomba tutazame ujumbe huu wa msingi kabisa ambao shetani anaupiga na kumvamia hasa katika Kanisa la nyakati za mwisho. Watu wote waliookoka huwa wana ujuenga mwili wa Kristo, yaani kanisa. 👉Kanisa linafananishwa na mwili ambao una viungo vingi ambavyo vinashirikiana na kufanya kazi pamoja. 👉Mwili wako ukiwa na kiungo kimoja ambacho hakifanyi kazi yake sawasawa au hakipo ndipo watu watakuita kilema 👉Na kilema kuna mambo hawezi kuyafanya kama walio wazima, hivyohivyo kanisa la Mungu ( mwili wa Kristo)...viungo vyake visipofanya kazi sawasawa au vingine visipokuwepo basi kanisa linakuwa dhaifu. 👉Lakini ikumbukwe kuwa kiungo kinaweza kuwepo katika mwili, lakini Kama hakifanyi kazi yake basi ni sawa na kisingekuwepo tu. Hebu tusome hapa👇 1 Wakorintho 12:12-14 [12]Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. [13]Kwa maana katika Roh