MUNGU YUPO NA WEWE USIOGOPE.
MUNGU YUPO NA WEWE USIOGOPE.
Yeremia 1:5-7
[6]Ndipo niliposema, Aa, Bwana MUNGU! Tazama, siwezi kusema; maana mimi ni mtoto.
[7]Lakini BWANA akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
Yeremia alikuwa ni nabii wa Mungu, ambaye alifanikiwa Kuanza huduma ya kumtumikia Mungu akiwa na umri mdogo Sana ( alitumwa na Mungu mwenyewe.)
Oooh Kumbe udogo wa umri / Miaka uliyonayo siyo kigezo Cha wewe kutokujua Siri za Mungu aliye hai na kutafuta namna ya kumtumikia Mungu ingali bado una nguvu sasa. Usisubiri mpaka ukiwa mzee ndipo utumike ,mtumikie Mungu Sasa.
Angalia Mungu anamwambia Yeremia kwamba ; Tazama kabla sijakuumba tumboni nalikujua, Tena kabla hujatoka tumboni nalikutakasa, Tena nimekuweka kuwa nabii wa mataifa mengi. maana Yake hakumfanya kuwa mtumishi wa watu wachache pamoja na udogo wake hapana, bali alimuamini katika utumishi mkubwa hivyo akamwambia USIOGOPE nipo pamoja na wewe, Tena nimekusanya kuwa nabii wa mataifa.
Mpendwa, kabla hujaumbwa Mungu alikujua maana ulikuwepo tangu mwanzo huko kwa Baba, alipokutuma ulimwenguni akakuweka tumboni mwa mama yako ili uzaliwe, na ulipozaliwa akakutakasa, maana Yake akakuweka wakfu kwa kazi yake, ukawa safi Kama chombo kilicho tayari kutumika na Mwenye nacho, (Mungu anakujua wewe).
Ndio maana upo mpaka leo , Mungu hakumruhusu mabaya yakupate kwasababu alikusudia tangu mwanzo, hivyo hutakufa bali utaishi ili uyasimulie matendo makuu ya Mungu.
Zaburi 118:17
Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
Usiogope Kumtumikia Mungu katika mazingira yeyote Yale, Usiogope kumtangaza Yesu mahali ulipowekwa. Usiweke sababu wakati wa Kumtumikia Mungu, kwasababu;
Mungu amekuamini wewe Muimbaji kuwa muimbaji wa kimataifa.
Mungu amekuamini wewe mwalimu wa Neno la Mungu uwafundishe wengi wapate kumjua Kristo na kuijua kweli ya Kristo Yesu.
Mungu amekuamini wewe Mwombaji ili uweze kuomboleza na kuwabebea wengine mizigo yao.
Mungu amekuamini wewe mwinjilisti ili uweze kuwatafuta kondoo waliopotea na kuwarudishia kwa mchungaji wao Yesu.
Wahubiri na watumishi mbalimbali fanyeni kazi ya Mungu bila kuona haya, maana Mungu amewaamini ili mlitunze KUNDI lake na kulilida lisipotee mpaka siku atakapokuja aje aione kazi ya kila mmoja.
Usiwe Kama Yule mtumwa mjinga aliyezika talanta yake katika ardhi asiweze kuzalisha.
Usizike karama yako, ipeleke shambani izalishe matunda bora zaidi kwa utukufu wa Mungu.
Panda mbegu ya utumishi wako ili Mungu ayakute matunda bora kwako
Katika kiwango ulicho nacho hichohicho fanya kwa usahihi na Mungu atatukuzwa ndani yako.
Yeremia alisimama na akafanya utumishi alioitiwa bila kuogopa Tena ,bila kuona haya.
Nawe usione haya, usiogope wewe ni Bora tena ni shujaa Sana na mshindi haleluya.
Barikiwa Sana.
TUOMBE
Yesu Kristo mfalme mwema tunalitukuza tunaliinuaa jinablako maana wewe ndiwe Baba Yetu, Tena Baba mwaminifu usiyetuacha kuwa mawindo kwa meno ya adui zetu.Ni asubuhi tena tunakurudishia Heshima na utukufu kwa kuwa umetuamsha salama sisi na jamaa zetu pokea sifa Yesu .Tunakusihi Bwana Uturehemu na makosa yetu.Tunaomba uongozi waa Roho wako Mtakatifu ,tukakutumikie wewe daima kwa mapenzi na utukufu wako Jehovah.Ratiba zetu zipo mikononi mwako BabaRatibisha kwa mapenzi yako, fahamu zetu na mawazo yetu yakanyamaze kimya Bali wewe ukainuliwe mahali hapa Yesu.Tunaomba ulinzi wako Mtakatifu ,tulinde dhidi ya Mahitaji wetu Shetani ,ili TUISHI maisha ya ushindi na kibali kila mahali kwa utukufu wa jina lako Yesu Amen
Taifa Teule Ministry
Mwl Beata Silwimba
0742442164/0620507212
Maoni
Chapisha Maoni