BINTI USIKATE TAMAA, MUNGU ANATENGENEZA LOVE STORY YENYE MVUTO
BINTI USIKATE TAMAA, MUNGU ANATENGENEZA LOVE STORY YENYE MVUTO
Bwana Yesu asifiwe mabinti wa kristo
Leo naomba tujifunze jambo ambalo lina nguvu ya kurejesha tumaini kwa mabinti wengi ambao huwa wanaingia kwenye kipindi cha kukata tamaa.
👉Ni kweli kwamba watu wengi kulingana na kawaida ya ulimwengu huu na dunia tunayoishi ,,kuweka vichwani mwao muda na majira ambayo yakifika ni lazima awe ameshaolewa na inaposhindikana kwa wakati huo wengi hukata tamaa.
👉Kukata tamaa kwa Mwanamke kwenye kipindi hiki siku zote husababisha Maumivu na pengine matatizo makubwa sana kwa binti huyo kwasababu huwa katika hali ya kufanya maamuzi ya ambayo yanalenga kile kinachomuumiza akili yake wakati wote ( kuolewa ).
👉Lakini leo nakuja kwako binti na ujumbe huu wa kuiponya nafsi yako na pengine hata maisha yako yasiharibiwe.
👉Ni lazima uwe na akili na mawazo ya juu zaidi kuliko kutumia mtazamo wa chini wenye Maumivu kwako.
👉Je umesahau kwamba silaha mojawapo ya Mungu anayoipenda na kuitazamia kwa watu wake ni USHUHUDA ?
👉Siku zote ushuhuda hubeba mambo makuu ambayo Mungu ameyafanya kwenye maisha ya mwanadamu
👏Ushuhuda hulenga kumtukuza Mungu juu ya mataifa ili wote wajengwe kwa hilo neno
👏Na huu ushuhuda hutengenezwa na Mungu mwenyewe.
👏Na ushuhuda unapotengenezwa na Mungu, kwa mwanadamu huonekana ni mateso, huonekana ni taabu, huonekana ni msumbufu , na wengi hufikiri wameachwa.......
Lakini umesahau kwamba ni yeye ndiye aliyesema hawezi kumwacha mtu wake akateseka😢
Zaburi 37:25
Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa
Wala mzao wake akiomba chakula.
Usiwe na mawazo kwamba Mungu amekuacha na kukuhuzunisha
Je umesahau kwamba ni yeye ndiye aliyesema hapendi tuteseke na wala kuhuzunika ?
Maombolezo 3:31-33
Hata milele.
[32]Maana ajapomhuzunisha atamrehemu,
Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.
[33]Maana moyo wake hapendi kuwatesa wanadamu.
Wala kuwahuzunisha.
Mungu huhitaji kujitwalia heshima mbele ya watu wote na ndiyo maana hutengeneza ushuhuda na ili kila adui yako na asili mbaya ya familia yako ijue kwamba yeye ndiye awezaye tena hakuna mwingine kama yeye.
Kutoka 14:4
[4]Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo.
Hebu jiulize hapo👆
Mungu alitufanya moyo wa farao kwa lengo la kiwaumiza watu wake ?
Jibu ni hapana...Mungu alikuwa anatengeneza ushuhuda.
👉Katika kipindi hicho Mungu alipokuwa anafanya ushindi na ushuhuda mkuu kwa watu wake mbele ya farao, wana wa israeli walikuwa wakiteseka na kulia.
👉Japo waliteseka na kulia kwa kufikiri wanateswa tu lakini kwenye ulimwengu wa roho Mungu alikuwa anafanya jambo la furaha isiyoisha. Na ndiyo maana hadi leo bado ushuhuda ule unaishi mpaka kwetu sisi.
Binti, Mungu hajakuacha bali anatengeneza ushindi usioisha na ushuhuda wa milele ili siku moja uje ukae na familia yako na watoto wako
👉Uwafundishe jinsi ya kumwamini Mungu
👉Uwaambie haikuwa rahisi mpaka wewe kuwapata wao bali ni Mungu tu
👉Uwaambie wajue kumtegemea Mungu
👉Uwaambie wawaambie watoto wao matendo makuu ya Bwana.
Na hili Mungu hulifanya ili watu wasimsahau yeye
Hebu jiulize usipokuwa na ushuhuda wa kumtaja yeye, itakuwaje ?
Maana yake ni kwamba hutawaambia watu kwamba nini Mungu amekutendea, maana yake hutayasimulia matendo ya Bwana na kwasababu hiyo kizazi kijacho hakitajua ukuu wa Mungu kupitia ndoa yako, pia kuna uwezekano wa wao kutokujua kumwamini na kumtegemea Mungu.
Kwani hujui tumbo la HANA lilikuwa limefungwa na Mungu mwenyewe.??
1 Samweli 1:4-6
[5]lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa BWANA alikuwa amemfunga tumbo.
[6]Ila mwenzake humchokoza sana, hata kumsikitisha, kwa sababu BWANA alikuwa amemfunga tumbo.
Kwakufungwa tumbo lake kulimfanya kupitia manyanyaso kutoka kwa mke mwenza, lakini hii haikuwa na maana kuwa Mungu amemwacha bali alikuwa anamtengenezea ushuhuda, na huu ushuhuda tinao mpaka sisi
👉Ni kweli, pengine wenzako wanakuona unamkosi na ndiyo maana huolewi
👉Ni kweli kwamba pengine unajiona hufai kwasababu umehitajo sana bila kupata n.k
Lakini kumbuka wewe sio wa kwanza kuonekana hufai....Hana Alishaonekana hivyo kwa wenzake.
👉Lakini kwakumtumaini Mungu tu Hana alifunguliwa tumbo na Mungu mwenyewe ushuhuda ukatengenezwa na akazaa mtoto bora kuliko wale waliokuwa wanaonekana bora, kwasababu yeye hakuzaa mtoto tu bali mtoto mtumishi wa Bwana Nabii samweli
Ni lazima ujue Mungu anapohitaji kukufanya bora kuliko wengine basi utalipa gharama kubwa kuliko wengine.
👉Ukitaka usiwe na ushuhuda na kukurupuka hata kwa mataifa watu wasiomjua Mungu basi jua kwamba utakuwa wa kawaida kama walivyo wao.
👉Tambua kwamba wewe si binti tu bali ni Binti aliye na Mungu. Hivyo ushuhuda wako ni mkubwa kuliko unavyodhani.
TAHADHARI
BINTI, nakupa Tahadhari ya kukaa mbali na walimu ambao watakwambia kwasababu hujaolewa mpaka sasa hivi basi UMEROGWA, pengine hata marafiki wakakushawishi kumwacha Mungu na kwenda kwa waganga pengine ukiamini utaenda kumjua na kumshughurikia aliyekuroga.
👉Ukiona hivyo tambua hao ni vibaraka wa adui na wamekuja kukuharibia ushuhuda maana tayari wameshajua nini kinatengenezwa rohoni.
👉Wewe ni lazima uendelee kububujika kama HANA mpaka watu wakadhani amechanganyikiwa na kulewa pombe kwasababu hakuwa anamtazama mtu bali alikuwa anamimina roho yake kwa Bwana ili Mungu ampe haja yake.
Unapoomba kwa bidii na kukaa na Mungu
👉Unafanya maadui Zako kukimbia na kushindwa kuzuia baraka zako.
Tambua tu wewe ni Mwana wa Mungu, binti wa thamani sana na kwasababu hiyo Mungu hawezi kukuacha bali anakutengenezea LOVE STORY yenye mvuto.
Mungu akutie nguvu kwa jina la YESU
Laddies in Christ
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni