SEMA HIVI 👇 KESHONI
SEMA HIVI 👇 KESHONI
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu
Leo naomba tuangalie namna Mungu anavyihitaji kuutumia ugumu wetu wa maisha na vifungo vyetu ambavyo tulikuwa navyo.
👉 Ni lazima ujue kuwa Mungu anavyomuokoa mtu, hamtazami mtu mmoja tu bali kundi kubwa la watu, familia nzima ,kizazi kizima, taifa zima na hata ulimwengu mzima.
👉Na jambo hili alilisema mwenyewe alipowaokoa watu fulani hivi
Tusome hapa 👇
Kutoka 13:14
[14]Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza keshoni, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;
Ukianza kwanzia mistari ya nyuma kidogo kwenye Biblia yako, utagundua kuwa Mungu alikuwa akizungumza kwa habari ya kumweka wakfu mzaliwa wa kwanza, lakini mstari wa 14 ndipo akatoa kusudi lake la ukombozi wa wana wa israel kwa kizazi cha kesho.
👉Kumbe hakuwatoa utumwani kwa ajili yao tu bali na kizazi kujacho
👉Kumbe Mungu anatenda jambo kwa kuangalia mbele zaidi kuliko leo
👉Kumbe hakutaka kuwaweka huru kizazi kilichokuwa utumwani tu bali alihitaji ushuhuda huu na mambo makuu aliyoyatenda yafahamike hadi kwenye vizazi vya leo.
Hii ikusaidie kujua kutoka kwenye taabu fulani, Mungu anahitaji kumtaja yeye na matendo aliyokutendea kwa watu wengine.
👉Wengi huwa wanapambama na hali ngumu ya maisha wakiwa na lengo la kuwaonyesha wengine kuwa wao ni bora
👉Wengine wanapambama na hali hizo ili waje wawakomeshe wengine
👉Wanajitutumua ili kuwadharau wengine.
Lakini leo nakujulisha kuwa ukiwa hivyo basi kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kuteseka kwasababu kufanikiwa kwako kuna madhara na wala hakujengi ufalme wa Mungu bali wa shetani.
👉Kwenye kila kitu ambacho unakihitaji jua kabisa kwa Mungu anakuuliza kuwa " NITAFAIDIKAJE NA KUFANIKIWA KWAKO " Kwasababu mpango wa Mungu ni hadi kesho na si kwako pekeyake.
👉Kwahiyo ni lazima tujue kuwa mateso yetu, Mungu anahitaji ayageuze kwa nguvu ya Roho mtakatifu na yawe maneno ya ushuhuda wa nguvu na matendo makuu ya Mungu kwenye maisha yetu.
👉Usiogope ugumu unaopitia sasaivi kwasababu MUNGU anahitaji siku moja usimame kuwambia watu , watoto wako, na kizazi kingine kuwa hapo ulipo ni kwasababu ya mkono wa Bwana.
👉Jifunze kusema " ni kwa mkono wa Bwana mimi niko hapa " ikionyesha ukiri na jinsi ambavyo huwezi jambo lolote bila Mungu.
Na ndiyo maana hata yeye mwenyewe baada ya kuwaokoa watu wake akawaambia na cha kusema katika siku za mbele ( keshoni ) ili tu Mungu aendelee kutukuzwa
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni