MWENYE HAKI ATASHIBISHWA MEMA NA MUNGU

 
MWENYE HAKI ATASHIBISHWA MEMA NA MUNGU

Isaya 54:14

[14]Utathibitika katika haki; utakuwa mbali na kuonewa, kwa maana hutaogopa; na mbali na hofu, kwa maana haitakukaribia.

Shalom.

Ili uhesabiwe haki lazima uwe thabiti na Mungu, umjue Mungu hasa. (Ayubu 22:21)

Mungu anaposema  utathibitika katika haki,  maana yake, haki yake Mwenye haki itamthibitisha mahali popote.

Wewe Mwenye haki hupaswi  kuishi maisha ya kuonewa , alionewa Yesu ili sisi tuwe na ujasiri

Aliteswa ili sisi tuwe huru.

Mwenye haki usitaabishwe na dhambi , Usitaabishwe na Mambo ambayo unajua kabisa ni haki yako kuwa nayo lakini huna kwa Sasa.

Jua kabisa kwamba haki yako ipo palepale  ila ni suala la Muda tu Muda wako ukifika Wala hakuna atakayesimama kuzuwilia baraka zako.

Hanna alikuwa Mwenye haki na alikuwa na sifa za kuzaa lakini wakati tumbo lake limefungwa ulikuwa si wakati wake, tunaona wakati wake ulipofika alifunguliwa na Bwana akampa kicheko.

Mwenye haki  ni jasiri si Kama wao,  Bali Kama Mwenye haki.

Mungu humjibu Mwenye haki kwa wakati sahihi?,wenye haki hula mema ya nchi wala haogopeshwi na changamoto.

Wewe ishi kwa mpangilio mzuri, ishi kwa Heshima na hekima, Uonekane kwenye mizani ya wenye haki wa Mungu waioonewa na mtu. Wewe Simama na Mungu naye atakutendea kwa wakati wake jifunze kusubiri 

TUOMBE

Baba katika jina la Yesu Kristo wa Nazareth aliye hai, wewe ni Mungu  mwema unatuwazia mema  Sana, wewe ni Baba Yetu, tena ndiwe Mungu wa kesho Yetu,

Tuna kila sababu ya kukushukuru Yesu mwema, umekuwa Baba na mlezi wetu tangu mwanzo hata sasa tuko salama kwasababu ulitupenda  tangu zamani na unatuwazia mema sana.Asante Bwana Yesu kwa Neema hii ya ajabu, umetupa Uzima, afya na akili njema tunalibariki jina lako Yesu.Tunajikabidhi mikononi mwako sisi na ndugu zetu na watoto wetu usituache Bwana.Siku ya leo tunaikabidhi mikononi mwako Bwana,Wokovu, Huduma, kazi ,  Biashara ,na  masomo Yetu Bwana utuinue katika hayo kwa utukufu wa jina  la Mungu Baba, Mungu Bwana na Mungu Roho Mtakatifu  naomba na Kuamini Amen.


Taifa Teule Ministry 
Mwl Beata Silwimba
0742442164 /0620507212 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI