BINTI USIWE PETE PUANI KWA NGURUWE


 BINTI USIWE PETE PUANI KWA NGURUWE

Bwana Yesu asifiwe mabinti na wanawake ndani ya Kristo.

Leo naomba tujifunze thamani ya mwanamke na jinsi inavyopotea pale tu anapokosa akili.

Kumbuka Mwanamke ni mtu ambaye amebebeshwa dhamana ya nyumba au familia kama msaidizi wa Mume

👉Hivyo mtu huyu anategemewa kuwa makini zaidi ili kupinga na kulinda dhidi ya kile kinachoitwa uharibifu.

Mara nyingi Mungu amewatumia wanawake wenye akili tu si wanawake tu kwasababu ya jinsia zao.

👉Kwenye ustawi wa eneo lako au nyumba yako, ndoa yako n.k haihitaji jinsia tu bali inahitaji akili ya mtu mwenye jinsia yako

Ni lazima ujue kuwa unatakiwa kuwa na akili ya ziada ili tu kuziba mianya na matatizo ambayo pengeni yanaweza kuamka ndani ya familia yako.

👉Tena ni lazima ujue kuwa mwanamke mwenye akili ni simba jike aungurumaye kuweka mazingira yake katika usalama.

👉Kila mwanamke ambaye hana akili ni lazima familia, ndoa, na majukumu yake yatamshinda kwasababu ya kukosa kile kinachoitwa hekima na mwongozo .

Hebu tusome hapa👇

Mithali 11:22

[22]Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe, 
Kadhalika mwanamke mzuri asiye na akili.

Ukisoma hapo lazima ujue vitu hivi 👇

👉Nguruwe ni mnyama ambaye kwa asili anapenda kukaa kwenye mazingira machafu tena hasa ya matope, na hujilza hapo na kuyakorogakoroga matope hayo na kisha kutoka akiwa mchafu sana,pia nguruwe ni mnyama asiyejali hali

👉Sasa Biblia inajaribu kutumia picha hiyo kwamba mwanamke mzuri asiyekuwa na akili ni sawa na Pete ya dhahabu kuwa katika pua ya nguruwe.

Pete ya dhahabu inapokuwa kwa mnyama ambaye hupenda uchafu, matopeni na asiyejali maana yake usalama na thamani ya hiyo dhahabu inafichika maana hata yenyewe itakuwa imepakwa matope tu.

👉Kumbe ndivyo ilivyo kwa mwanamke mzuri asiye na akili

👉Kuna mabinti wengi wazuri mtaani ambao wanafanya mambo mabaya kama vile uvutaji wa sigara, kujiuza n.k

👉Lakini pia mbali na hao kuna wale ambao huwa wanaweka uzuri wao mbele badala ya kuweka akili mbele.

👉Ni lazima ujue kama mwanamke kwamba kitakachokufanya uwe mshindi si uzuri wako bali ni ile akili ambayo Mungu amekupa,,basi itimie hiyo acha kuutumainia uzuri wako.

Katika hili utatambua kwamba, kuna mwanamke unaweza kumuona ni mzuri wa sura na ni mrembo kweli lakini ukaambiwa hajaolewa, au ameachika,

👉Katika namna hii usitumie nguvu kubwa sana ya kujipamba ili kuongeza urembo ukidhania kuwa ndoa inataka urembo tu...hapana

👉NDOA inataka AKILI yako zaidi ya urembo wako. Kwasababu utakapokuwa mrembo asiyekuwa na akili basi jua litakukuta kama lililowakuwa wake uliowaona warembo na kisha ukashangaa kwanini wapo kwenye hali mbaya.

Kitu cha kukitazama kwa makini katika maisha yako ni AKILI na namna nzuri ya kufanikiwa kwenye mipango yako, ndoa yako, na kila sehemu na siyo kuhangaika kama wanawake wengine wanavyohangika wakidhani kuwa kuongeza urembo na uzuri ndiyo sababu ya kupendwa...hapana

👉Leo tambua kuwa kuongeza uzuri na urembo kwa gharama ni kuongeza kutamaniwa na si KUPENDWA

👉Unapoongeza urembo basi unawafanya wanaume wepesi( dhaifu ) wakutamani kingono na kila mmoja kutamani kulala na wewe, maana hisia ya mtu mume huamshwa na kile kizuri alichokiona au kukusikia kuhusu mwanamke.

👉Bali ili KUPENDWA na mwanaume ambao kila mwanamke anatamani ( mwenye akili ) ni lazima kutumia akili.

Ukiwa mzuri bila kutumia akili basi jua unawaalika wenye kukutamani zaidi kuliko kukupenda kwasababu kila mwanaume mwenye akili wa kukuoa wewe ni lazima ujue kuwa ataangalia akili yako na zi uzuri wako.

👉Katika hili sina maana kuwa usiwe mzuri ...hapana. Pengine wewe ni mtu unayependa urembo n.k basi ni lazima uitumie akili kuliko urembo na uzuri wako.

Jua tu👇

👉Mwanaume mwenye kukupenda ataangalia akili maana huwa wanaume wanavyooa mwanamke wanakuwa na mawazo kwamba mwanamke huyo awe mlezi wa watoto wake na familia kiujumla na ndiyo maana ataangalia akili

👉Mwanaume mweny kukutamani ataangalia uzuri wako na urembo ulionao maana akili yako hana shida nayo kwasababu hajakupenda kwa malengo ya baadae bali ameuangalia uzuri wako tu na kutamani kuwa na wewe.

Hivyo binti usiwe kama dhahabu puani kwa nguruwe bali uwewanamke shupavu.

Mungu akuwezeshe kwa jina la YESU


Laddies in Christ 

Mwl /Ev Mathayo Sudai 

0744474230 /0628187291 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI