KITABU CHA SHERIA KISIONDOKE KINYWANI MWAKO......


 KITABU CHA SHERIA KISIONDOKE KINYWANI MWAKO......

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu 

Leo naomba kila mtu ajifunze jambo hili la msingi sana kwa ajili ya maendeleo yake na mafanikio yake binafsi.

Ni kwa habari ya neno la Mungu, sheria za Mungu, au mapenzi ya Mungu ambayo tunayapata kutoka mahali yaliyoandikwa yaani Biblia.

Ikumbukwe kwamba kuna namna ambayo Mungu alikuwa anatembea na Musa katika safari ya wana wa israeli

👉Alitembea naye kwa viwango vya juu hata Musa kumuona Mungu kwa umbo lake 

👉Lakini hii yote ni kwasababu Musa alikuwa ametii maagizo ( neno ) la Mungu kwa ukamilifu na hivyo aliyajua mapenzi ya Mungu.

Soma hapa👇

Hesabu 12:7-8

[7]Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; 
Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;
[8]Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, 
Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; 
Na umbo la BWANA yeye ataliona....

Kwahiyo hayo yote ni kwasababu Musa alikuwa amelishika sana neno la Mungu ( sheria ya Mungu), na hii ndiyo ilimfanya kutembea katika ulimwengu wa roho kwa mamlaka ya juu sana

👉Musa mara nyingi sana alikuwa anakutana na Mungu katika ulimwengu wa roho, na hata KUPENDWA sana na Mungu.

Sasa baada ya Musa kuwa amekufa tunauona Mungu akimpa Yoshua nafasi ya kuwaongoza wana wa israeli

👉Lakini ukisoma utagundua kuwa Mungu anaonyesha Siri ya Yoshua kutembea nae kama Musa....akamwambia hivi👇

Yoshua 1:8

[8]Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Sasa ni kwamba Mungu hakumpa amri mpya Yoshua iliyo tofauti na ile ya kwa Musa bali alimwambia aishike sana ile torati( sheria/ neno/maandiko ) na kufanya sawasawa na alivyomwamuru Musa.

Soma hapa 👇

Yoshua 1:7

[7]Uwe hodari tu na ushujaa mwingi, uangalie kutenda sawasawa na sheria yote aliyokuamuru Musa mtumishi wangu; usiiache, kwenda mkono wa kuume, au wa kushoto, upate kufanikiwa sana kila uendako.

Unaona hapo 👆

Mungu alikuwa akimsisitiza sana Yoshua kuyasoma maagizo yake, kuyatafakari pia kila siku kwasababu akiyatenda hayo basi atafanikiwa sana katika mwili na roho na kuwa na haki mbele za Bwana.

👉Hapa Mungu alifunua habari ya watu wake kulishika sana neno lake, kulitafakari kila siku na kuliishi na pia hiki ndicho chanzo cha mafanikio, kwasababu wengi hawafanikiwi kwasababu ya kutokulijua neno la Mungu juu ya baraka zao

👉Wengi wanatenda dhambi kwasababu ya kutokulijua neno la Mungu 

👉Lakini unapokuwa na neno la Mungu ndani mwako basi jua ni lazima uwe na mafanikio katika kila unachokifanya kwasababu utakuwa unajua maana na sababu ya unachokifanya.

Zaburi 1:1-3

[1]Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki; 
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji; 
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo, 
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.
[3]Naye atakuwa kama mti uliopandwa 
Kandokando ya vijito vya maji, 
Uzaao matunda yake kwa majira yake, 
Wala jani lake halinyauki; 
Na kila alitendalo litafanikiwa.

👉Mungu alikuwa anamwambia Yoshua kwamba kwa neno la Mungu, litamfanya Yoshua kukutana na Mungu kama vile ilivyokuwa kwa Musa.

👉Na hata wewe leo ni lazima ujue kuwa unatakiwa kulishika neno la Mungu na kulitafakari kila siku.

👉Jambo hili linafanya neno la Mungu kuwa kama sehemu ya maisha yako na hata matendo yako yatakuwa yanaoongozwa na Roho tu, kwasababu neno ndilo lililokaa katika fikra yako.

👉Unapolitafakari neno la Mungu kila siku basi ujue kabisa kwamba, fikra zako, maneno yako, matendo yako, na hatamawazo yako yatakuwa sawasawa na neno la Mungu.

Na nin lazima ujue kuwa unachokiwaza ndicho kichotokea kwenye maisha yako.

👉Maisha yako ya kesho ni matokeo ya mawazo yako ya leo.

Kivipi??

Ni hivi👇

Mawazo ya mtu yanatoka katoka fikra ya mtu( human mind), na fikra ya mtu ndiyo huwa inaongoza nafsi kuufuata utashi fulani, na nafsi ndiyo unayouamrisha mwili kufanya sawasawa na kinachozunguka kwenye fikra ya mtu.

Kwahiyo kwa kuwaza tunatengeneza uhalisia wa maisha yetu kwa kile tunachokiwaza.

Na ndiyo maana Mungu alisema tuangushe kila mawazo mabaya kwa nguvu ya Roho mtakatifu👇

2 Wakorintho 10:5

[5]tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo;

Lakini unapokuwa unasoma neno la Mungu na kulitafakari sana unajikuta hata unavyowaza ni sawa na neno la Mungu na ndivyo unavyotengeneza uhalisia wako kesho.

Na ndiyo maana Biblia inasema " aonavyo/awazavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo "

👉Unapokosa neno la Mungu la kukufanya ulitafakari/ kuwaza ndicho chanzo cha Shetani kuvamia fikra yako na kuijaza giza na mwisho wake unaanza kuwaza mawazo mabaya

👉Ukikaa unawaza usinzi

👉Ukikaa unataaa ya dhambi

👉Ukikaa unawaza kunywa pombe

Na mawazo mengine mengi ambayo shetani anaanza kuyaweka kwenye fikra yako akijua kwamba ukiwaza sawasawa na hayo basi ni lazima utayafanya kesho. Na hutakuwa na uwezo wa kuzuia kwasababu umeruhusu uhalisia kujengwa ndani ya fikra yako.

Na ndiyo maana Mungu anataka tuwaze vizuri hivyo akasema maneno ya sheria yake yasitoke vinywa mwetu bali tuyatafakari kila siku.

Mungu ukusaidie uelewe habari hii


Taifa Teule Ministry
Mwl / Ev Mathayo Sudai
0744474230 / 0628187291 

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI