USIMDHARAU UNAYEMDHARAU
USIMDHARAU UNAYEMDHARAU
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu
Leo ni siku nyingine naomba tujifunze jambo la msingi kwa jinsi ya kuishi katika usalama pamoja na wale wanaoonekana kuwa ni wanyonge.
Biblia inasema hivi👇
Mithali 22:22-23
Wala usimdhulumu mtu mnyonge langoni;
[23]Kwa sababu BWANA atawatetea;
Naye atawateka uhai wao waliowateka.
Kuna watu wengi huwa wanapokuwa katika nafasi fulani, kazi fulani, cheo fulani au kuwa na kitu chochote ambacho wengine ( maskini) hawana...basi huwa ni kama fimbo ya kuwapigia wenzao.
👉Unapoishi katika maisha yako pamoja na baraka zote apizokubaliki Mungu basi Usimnyang’anye haki ya maskini kwa kudhania kuwa ni maskini hawezi kukufanya lolote.
👉Pia Biblia inasema USIMDHULUMU...
👉Sasa ni lazima ujue kuwa unapokuwa katika nafasi yoyote ile ya mafanikio ya namna fulani, jitahidi sana usije ukafikiri labda wewe ni bora kuliko wengine au wewe ni wathamani kuliko wale wasipokuwa nacho.
👉Kuna watu wengi wakipata mali wanakuwa tishio kwa wengine
👉Kuna watu wanawanyanyasa wengine kwasababu ya cheo alichonacho
👉Wengine wanawataabisha wengine kwasababu ya pesa walizonazo
👉Wengine wana wadharau wengine kwasababu ya aina ya maisha walionayo yanawapa kiburi na kuwaona wenzao hawana maana tena.
Jitahidi kujua kuwa anayewalinda wanyonge na wenye nguvu ni Mungu pekee na wote anawatazama na kuwathamini kwa wakati mmoja.
👉Maskini na Tajiri wote ni wa Mungu na Kristo alikufa kwa ajili yao wote.
👉Unapomuona dhaifu kana kwamba hana maana ni dhahiri pasipo kujua unasema kuwa Yesu alikufa kwa ajili ya wasio na maana maana yake kufa kwake ni bure.
Soma hapa👇
Wagalatia 3:28
[28]Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke. Maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu.
👉Ni lazima ujue kuwa liziki, utajiri, karama, kipawa, na baraka zote hutolewa na Mungu kwa wote kama apendavyo yeye kwa wakati wake na hivyo ni lazima kila mtu asiwe fimbo ya kumchapia mwenzake kwa kigezo cha umaskini au udhaifu alionao.
Lakini Kama haitoshi ni kwamba wale wanaowaonea wanyonge, wanaowadhulumu maskini na kuwaona si kitu...basi ni lazima wajue kuwa Mungu atawaadhibu na kuwashusha.
👉Mungu ni mlinzi wa wanyonge
👉Mungu ni baba wa wote
👉Mungu ni mtetezi wa wenye udhaifu
👉Mungu pia ni mlinzi wa maskini.
Hivyo mtu yeyote atakaye wadhuru hao, Mungu naye atamdhuru yeye
👉Mtu yeyote atakayewapiga hao, Mungu naye atampiga
👉Mtu atakayewadharau hao, Mungu naye atamdharau.
Naye atawateka uhai wao waliowateka.
23 For the lord is their defender. He will ruin anyone who ruins them.
Proverbs 22:23
👉Mtu akikidharau unachokilinda maana yake amekudharau hadi wewe,ni sawa na kukwambia kuwa unalinda kitu kisichokuwa na maana..na kama ni hivyo kumbe hata wewe akiri yako haiko sawa ndio maana unalinda kitu kisichokuwa na maana.
👉Sasa Biblia inasema hao dhaifu, maskini na wanyonge wote ni wa Mungu na wanakindwa na Mungu mwenyewe hivyo kuwadharau hao ni sawa na kumdharau Mungu kwa kumwambia analinda kisichokuwa na maana.( hilo ni kosa kubwa)
👉Na ndiyo maana kwa watu wengi, Mungu anapowabariki tu..shetani naye huwajaza kiburi na majivuno pamoja na dharau akijua kwamba wanapoanza kuwadharau wenzao basi moja kwa moja wamemdharau Mungu ( hivyo kuwa makini unapofanikiwa)
👉Jambo hilo linamfanya Mungu kukushusha chini na kughairi baraka zote alizohitaji kukupa. Japo kuwa alikuahidi kukubariki zaidi ya hapo, ni lazima ujue unapoingiliwa na shetani kwa namna hiyo basi Mungu atakushusha badala ya kuendelea kukupandisha
ni hivi👇
1 Samweli 2:30
[30]Kwa sababu hiyo, BWANA, Mungu wa Israeli, asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda mbele zangu milele; lakini sasa BWANA asema, Jambo hili na liwe mbali nami; kwa maana wao wanaoniheshimu nitawaheshimu, na wao wanaonidharau watahesabiwa kuwa si kitu.
Hii ikusaidie kujua kuwa Hutakiwi kumuonea mtu yeyote kwasababu ya
👉Uwezo wako
👉Mali zako
👉Cheo chako
👉Mafanikio yako
Hata unapotangulia kupata mafanikio kabla ya wengine basi usianze kudhania kuwa umemaliza safari na ukaanza kuwadharau ambao bado kwasababu hata wao wanatafuta kama ulivyokuwa unatafuta wewe isipokuwa Mungu alionao vyema kukupa wewe kabla ya wao. Na hii haibebi maana kuwa wewe ni bora kuliko wao.
👉Ni lazima ujue Mungu anaweza kukupa leo akakunyang'anya kesho ukiwa na tabia zisizompendeza yeye.
Soma hapa👇
Danieli 2:21
[21]Yeye hubadili majira na nyakati; huuzulu wafalme na kuwamilikisha wafalme; huwapa hekima wenye hekima; huwapa wenye ufahamu maarifa;
👉Unapotangulia kupata usidhani wengine hawana thamani
👉Unapotangulia kupanda cheo usifikiri wengine ni wabaya kuliko wewe
👉Unapotangulia kuolewa usifikiri wengine hawaonekani machoni PA Mungu
👉Unapotangulia kuwa na maisha bora usijaribu kudhania kuwa wengine hawana akiri kama uliyonayo wewe.
YAANI SISI SOTE NI SAWA MACHONI PA BWANA.
Mungu akubariki sana
Mwl / Ev Mathayo
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni