KUWA MAKINI NA AINA 02 ZA WANAUME
KUWA MAKINI NA AINA 02 ZA WANAUME
Bwana Yesu asifiwe mabinti wa kristo
Leo naomba jifunze jambo moja kuhusu wanaume ambao kama binti ni lazima watakuja kwako.
👉Binti anapofika katika kipindi cha wanaume kumfuata, na kipindi ambacho yupo tayari kuolewa basi ni lazima atafatwa na wanaume wa aina mbili.
1: Mwanaume mwenye kupenda na kuwa na haja ya kuoa
2: Mwanaume ambaye atakuja kwa lengo la kupumzika na kutuliza hisia zake kwa kitambo tu
👉Hawa ni watu wawili ambao kuna wakati wanaweza kuja kwako binti kwa maneno na ahadi zinazofanana.
1c ANAYEHITAJI KUOA
huyu ni mwanaume ambaye huwa na uhitaji wa kupata mke/Mwenza na anapokuja nyuma yake huwa amebeba mapenzi ya Mungu, pengine bila hata ya yeye kujua
👉Hata kwa watu ambao hawajaokoka ni lazima ujue hata wao pia, mtu anapokuwa na ajenda ya kupata mwenza basi amebeba ajenda nzuri ya Mungu bila hata kujua (ana jambo la kimungu ).
👉Hapa sina maana ya kwamba mpagani anaweza kumuoa binti aliyeokoka bali ninaweka tu ule msingi wa nini Mungu anakipenda kuhusu ndoa.
👉Huyu ni mwanaume ambaye hata shetani hupiga vita na kumkatisha tamaa kwa vingi ili tu asiyafanye mapenzi ya Mungu.
2: ASIYE MUOAJI
Mtu/ mwanaume mwingine ambaye ayakufuata ni yule ambaye pengine anaweza kuonekana ni mzuri, maneno yake ni mazuri, ahadi zake zinakufurahisha lakini kumbe hana ajenda ya kukuoa.
👉Wanaume wa aina hii wale ambao huwa wamekuona namna unavyopendeza na kuvutia ndipo wanakuja na haja yao ni kulala na wewe tu, kupoteza muda lakini hana muda wa kukuoa.
👉Huyu huleta Maumivu makubwa kwa binti Anayehitaji Kuolewa kwasababu mabinti wengi wanapokuwa wapo kwenye kipindi cha kuolewa huwa wanakuwa wazi sana ( open sana) kwa mtu yeyote anayekuja
👉Sasa anapokuja huyu wa namna hii humwachia Maumivu makubwa pale baada ya kumaliza haja yake na kuondoka.
👉Lazima ujue mwongozo huu kwasababu unapokuwa mwanamke kuna kipindi ambacho unakuwa na hali ya kufikiri juu ya kile unachokihitaji, na ni lazima ujue kuwa wakati huo huo Mungu atakuwa na wewe lakini pia shetani atakuja kwako kukuharibia kila kitu kupitia mwanaume asiye muoaji
Yohana 10:10
[10]Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.
Ni lazima ujue kuwa katika kila Hatua, shetani anakutazama na anahitaji kukutoa kwenye mstari wa Mungu na ndiyo maana
👉Wanawake wengi wameharibikiwa maisha yao baada ya kusalitiwa
👉Wengi wameacha wokovu baada ya kuwa na watu wasiofaa
👉Wengi wanaishi kwenye majuto kwa kuyakosa yale waliyoyatarajia
👉Wengi walikuwa na nguvu lakini leo hawana nguvu tena
Ni lazima ujue kuwa ukikutana na mwanaume mbaya basi ndicho chanzo cha kuua maono yako, Huduma yako, vipawa vyako n.k
👉Na ndiyo maana unaweza ukashangaa kwamba ulipokuwa kwenye mahusiano na mtu fulani mambo yako mengi yalianza kufa bila kujua sababu
👉Kuna watu ambao hijab kwako si kwa lengo la kuoa bali kuua. Tena wakati mwingine hata shetani huwaleta kwa sura nzuri kabisa👇
2 Wakorintho 11:14-15
[15]Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.
Mtu wa kukuoa akija kwako basi utashangaa
👉Kama ulikuwa na udhaifu anakuhifadhi na kukupenda hivyohivyo
👉Muoaji akija utashangaa mambo fulani hukuwa nayo ghafla yanaanza kuamka, mara promotion, na muamko wa kiroho usio wa kawaida kwasababu huja akiwa na mapenzi ya Mungu ndani yake na baraka za Mungu kuhusu ndoa huwa pamoja naye.
👉Lakini sivyo alivyo asiye muoaji ...huyu akija lazima ataua vya ndani mwako
Utashangaa karama imekuwa,
Utashangaa anakuwa ni mtu mwenye kukutaka ufanye naye NGONO tu hata kabla ya ndoa bila kujali uharibifu
Utashangaa hofu ya Mungu kwako inapote
Utashangaa kile ulichokuwa nacho kinapotea
Unabaki kuwa ni mzuri wa sura kama alivyo kutamani lakini ndani mwako unakufa kabisa na thamani yako, kibali chako kinapote.
Mithali 31:30
Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa.
Ni lazima uwe na akili katika hilo binti yangu kama unahitaji mtu wa kukuoa
👉Na ni lazima ujue kuwa binti aliyeokoka huwa hajiingizi kwenye mahusiano na mtu yqsiyokuwa ya uchumba wa kufikia ndoa.
👉Mahusiano ya binti na kijana aliyeokoka ni yale yanayohusu ndoa na si NGONO zisizo na mpangilio ambazo ni kumkosea Mungu
👉Mwanaume anayekupenda, aliye tayari kukuoa ni mwanaume ambaye hataki kukutenga na Mungu hivyo habari ya NGONO kabla ya ndoa haipo kwake. Lakini ni mwepesi sana kuomba Rehema pale anapokukosea na kumkosea Mungu maana hataki uishi katika hali mbaya
KUMBUKA
Hapa ninazungumza na binti ndani ya Kristo, sizungumzi na watu wote. Maana watu wa dunia hii NGONO kwao ni kawaida kwenye mahusiano yao na huamini kwamba NGONO ndiyo ishara ya upendo. Na ndiyo maana akikutongoza leo, kesho anakutaka ulale nae.
Lakini kwa mabinti ndani ya Kristo ( laddies in Christ ) ni kinyume na hao.
👉Kama Mwanaume anampango na wewe hawezi kukuharibia mahusiano na Mungu.
Katika hayo yote ni lazima ujue tu kwamba BINTI NDANI YA KRISTO unatakiwa kuwa na hekima na akili iliyotulia ili kuendelea kuwa salama kwa utukufu wa Mungu.
Mwl/ Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni