UKIWA MMOJA HUWEZI..


 UKIWA MMOJA HUWEZI..

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu. Leo naomba tutazame ujumbe huu wa msingi kabisa ambao shetani anaupiga na kumvamia hasa katika Kanisa la nyakati za mwisho.


Watu wote waliookoka huwa wana ujuenga mwili wa Kristo, yaani kanisa.

👉Kanisa linafananishwa na mwili ambao una viungo vingi ambavyo vinashirikiana na kufanya kazi pamoja.

👉Mwili wako ukiwa na kiungo kimoja ambacho hakifanyi kazi yake sawasawa au hakipo ndipo watu watakuita kilema

👉Na kilema kuna mambo hawezi kuyafanya kama walio wazima, hivyohivyo kanisa la Mungu ( mwili wa Kristo)...viungo vyake visipofanya kazi sawasawa au vingine visipokuwepo basi kanisa linakuwa dhaifu.

👉Lakini ikumbukwe kuwa kiungo kinaweza kuwepo katika mwili, lakini Kama hakifanyi kazi yake basi ni sawa na kisingekuwepo tu.


Hebu tusome hapa👇


1 Wakorintho 12:12-14

[12]Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo.

[13]Kwa maana katika Roho mmoja sisi sote tulibatizwa kuwa mwili mmoja, kwamba tu Wayahudi, au kwamba tu Wayunani; ikiwa tu watumwa au ikiwa tu huru; nasi sote tulinyweshwa Roho mmoja.

[14]Kwa maana mwili si kiungo kimoja, bali ni vingi.


Unaona hapo Biblia inalilinganisha kanisa na mwili wa Kristo.

Ambapo viungo ndiyo sisi ambao tumeokoka na kubatizwa.


Lakini kwanini kanisa linaonekana kutokuwa na nguvu??


Tuendelee hapa👇


1 Wakorintho 12:15-19

[15]Mguu ukisema, Kwa kuwa mimi si mkono, mimi si wa mwili; je! Si wa mwili kwa sababu hiyo?

[16]Na sikio likisema, Kwa kuwa mimi si jicho, mimi si la mwili; je! Si la mwili kwa sababu hiyo?

[17]Kama mwili wote ukiwa jicho, ku wapi kusikia? Kama wote ni sikio ku wapi kunusa?

[18]Bali Mungu amevitia viungo kila kimoja katika mwili kama alivyotaka.

[19]Lakini kama vyote vingekuwa kiungo kimoja, mwili ungekuwa wapi?


Unaona hapo...ni kwamba mwili hauwezi kuwa mguu tu, au mkono tu au jicho tu bali mwili ni mkusanyiko wa viungo vingi vinavyotegemeana na kufanya kazi kwa pamoja ili kuendelea kuifanya mwili kuwa na uhai.


👉Na hivyo ndivyo watu wa Mungu waliookoka wanatakiwa kuishi na kushirikiana kama wanahitaji kuujenga mwili wa Kristo.

👉Sasa katika namna hiyo hatakiwi mtu yeyote kujiona yeye ni bora kuliko wenzake ndani ya kanisa, au hatakiwi mtu yeyote kudhania huduma yake ndiyo ya maana kuliko wenzake.


Kwasababu kama wewe ni mkono wenye nguvu basi jua unalihitqji jicho ili kuona 

👉Na Kama wewe ni mguu wa kutembelea basi unamuhitaji sikio ili asikie kile unachotakiwa kukiendea.


Soma hapa kukuona hilo👇


1 Wakorintho 12:21-23

[21]Na jicho haliwezi kuuambia mkono, Sina haja na wewe; wala tena kichwa hakiwezi kuiambia miguu, Sina haja na ninyi.

[22]Bali zaidi sana vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa vinyonge zaidi vyahitajiwa zaidi.

[23]Na vile viungo vya mwili vidhaniwavyo kuwa havina heshima, viungo vile twavipa heshima zaidi; na viungo vyetu visivyo na uzuri vina uzuri zaidi sana.


Unaona, hapo anaeleza kwamba

👉SIYO kwasababu jicho linaona basi ni la thamani kuliko vingine

👉Si kwasababu sikio linasikia ndiyo LIWE la muhimu kuliko vingine 


Bali vyote vinategemeana ili kufanya kazi bora.


Na ndiyo maana mtu mwenye macho lakini hana miguu anaweza akaona kitu kizuri mbele yake lakini asikifuate kwasababu hana miguu.


👉Na mtu mwenye miguu bila macho anaweza akatembea bila kujua anaenda wapi.

👉Lakini akiwa na vyote basi atafanikiwa...na hivyo ndiyo kanisa ilivyo.


👉Hata kama wewe ni mdogo na unajidharau ni lazima ujue kuwa unathamani sana japo wengine wanaweza wasikuone, kwasababu hata wew ni kiungo cha mwili.


Hili litusaidie kujua namna ambavyo shetani analichezea kanisa letu kwa kuondoa umoja ndani yetu kiasi kwamba watu wanajivunia na kujitapa kwa huduma zao.

👉Uliona hilo utagundua katika kipindi hiki kila mtu mwenye huduma anapambana mwenyewe tu wala hashirikiani na wenzake.

👉Leo hii kumekuwa na ugomvi wa wachungaji kwa wachungaji.

Manabii na wachungaji, waimbaji kwa waimbaji...


Sasa kwa namna hii ni lazima ujiulize kama viungo havipatani mwili unawezaje kutenda kazi???


Manabii hawatakiwi kudhani kuwa hawamwitaji mtu kwasababu kazi kuu ya NABII ni kuona..lakini ukiishia kuona na asiwepo mwalimu wa kufundisha wengine ulichokiona ina faida gani ??


Mwinjilisti ukiwahubiria watu wakamkubali kristo ni nani atakaye walea hao watu katika wokovu kama hakuna mchungaji.

👉Wengine Mungu amewabariki kipato kizuri na wanatoa kwa kazi ya Mungu...lakini hiyo haitakiwi kukufanya udhanie ya kwamba wewe ni muhimu kuliko wengine kwasababu hata wasiotoa kama wewe, kuna mambo wanayafanya vizuri zaidi kuliko wewe.


Hivyo mtumwa , bwana( boss), Tajiri na maskini wanapookoka hawa wote ni wa thamani sana mbele za Mungu na mbele za kanisa.


Leo hii shetani analifanya kanisa kuwa dhaifu sana kwasababu ameondoa ushirikiano na umoja ndani ya kanisa....


Ushirikiano ni jambo la msingi , hata wewe katika maisha Hutakiwi kuwa pekeyake tuuu..bali unawahitaji watu pia na ndivyo ilivyo ndani ya kanisa, hatuwezi tukaziona nguvu za Mungu bila umoja.


Soma hapa uliona hilo👇


Mhubiri 4:9-10

[9]Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; 

Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.

[10]Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!


Hebu kaa kama Mwana wa Mungu yatafakari hayo kisha chukua hatua sahihi.


Mungu akubariki sana 


Taifa Teule Ministry 

Mwl / Ev Mathayo Sudai 

0744474230 /0628187291 


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI