USIOGOPE UPINZANI
. USIOGOPE UPINZANI ULIOPO JUU YAKO BALI TAZAMA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO UKALITIMIZE . *Nehemia 2* 2 Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana. 3 Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto? 4 Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni. 5 Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga. 📍Mtumishi wa Mungu nabii Nehemia aliposikia kuwa ukuta wa yerusalemu umebomolewa na maadui akaketi chini akitafakari atafanyaje na yupo chini yafalme. 📍wakati akitafakari mfalme akatambua kuwa inawezekana kuna shida kwa nehemia maana moyo wake ulijaa huzuni...