USIOGOPE UPINZANI
*Nehemia 2*
2 Basi mfalme akaniambia, Mbona umesikitika uso wako, nawe huna ugonjwa? Nini hii, isipokuwa ni huzuni ya moyo? Ndipo nikaogopa sana.
3 Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto?
4 Ndipo mfalme akaniambia, Una haja gani unayotaka kuniomba? Basi nikamwomba Mungu wa mbinguni.
5 Nikamwambia mfalme, Mfalme akiona vema, na ikiwa mimi, mtumishi wako, nimepata kibali machoni pako, tafadhali unipeleke mpaka Yuda, niuendee mji wa makaburi ya baba zangu, nipate kuujenga.
📍Mtumishi wa Mungu nabii Nehemia aliposikia kuwa ukuta wa yerusalemu umebomolewa na maadui akaketi chini akitafakari atafanyaje na yupo chini yafalme.
📍wakati akitafakari mfalme akatambua kuwa inawezekana kuna shida kwa nehemia maana moyo wake ulijaa huzuni ndipo mfalme akamuuliza nehemia 👇
Nikamwambia mfalme, Mfalme na aishi milele; kwani uso wangu usiwe na huzuni, iwapo mji, ulio mahali pa makaburi ya baba zangu, unakaa ukiwa, na malango yake yameteketezwa kwa moto?
📍Ndipo mfalme akamruhusu aende yerusalem ili aweze kuujenga ule mji ilioteketezwa kwa moto
wakati anaelekea Yerusalem akakutana na upinzani wa 👇
10 Hata Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, waliposikia habari hizi, ziliwahuzunisha sana, kwa kuwa amekuja mtu kuwatakia heri wana wa Israeli.
*Maana hawakupenda Nehemia aende Yerusalemu kuujenga ule mji ila walitaka abaki na wao kule uhamishoni akimtumikia mfalme (hawakutaka kazi ya Mungu ifanyike).*
11 Basi nikafika Yerusalemu, nikakaa huko muda wa siku tatu.
12 Kisha nikaondoka usiku, mimi na watu wachache pamoja nami; wala sikumwambia mtu neno hili alilolitia Mungu wangu moyoni mwangu, nilitende kwa ajili ya Yerusalemu; wala hapakuwa na mnyama pamoja nami, ila mnyama yule niliyempanda mwenyewe.
📍Lakini alipofika yerusalem ni kweli mji uliharibika sana ndipo akaamua kuanza ujenzi wa mji wa yerusalemu ulioharibiwa kwa moto *Lakini pia aliendelea kukutana na upinzani mkubwa 👇*
Nehemia 2
19 Lakini waliposikia Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Mtaasi ninyi juu ya mfalme?
📍lakini hakukatishwa tamaa kwa maneno yaokwamba hataweza bali alisimama imara ili kutimiza kusudi alilopewa na Mungu.
Nehemia 2
20 Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.
Upinzani alio kutana nao👇
Kudharauliwa sana, kuchekwa na kukatishwa tamaa kwanzia mwanzoni wanawambia
Nehemia 4
3 Basi Tobia, Mwamoni, alikuwa karibu naye, akasema, Hata hiki wanachokijenga, angepanda mbweha, angeubomoa ukuta wao wa mawe.
Bado wakaghadhibika katika mioyo yao kwanini ukuta unajengwa wakaona sasa wake tu kufanya vurugu maana maneno tu hayatoshi.
Nehemia 4
7 Lakini ikawa, Sanbalati, na Tobia, na Waarabu, na Waamoni, na Waashdodi, waliposikia ya kuwa kazi ya kuzitengeneza kuta za Yerusalemu inaendelea, na ya kuwa mahali palipobomoka panaanza kuzibwa, basi wakaghadhibika mno;
8 wakafanya shauri wote pamoja kuja kupigana na Yerusalemu, na kufanya machafuko humo.
*Lakini nimefurahishwa na moyo wa Nehemia hakukata tamaa kwasababu alikuwa na wivu na kazi ya Mungu na alipoona upinzani unazidi Alimtazama na kumwomba Mungu aliyemuweza wa yote maana aliamini katika Mungu inawezekana ukuta kujengwa hata kama adui hataki.*
Nehemia 4
9 Bali sisi tulimwomba dua Mungu wetu, tena tukaweka walinzi, mchana na usiku, kwa sababu yao, ili kuwapinga.
📍Ukiendelea mpaka mwisho utaona kazi ya Mungu ilivyokamilika kwa ushindi mkuu mno.
✍️ Ndugu yangu najua lipo kusudi ndani yako ambalo Bwana amekuita kulitumikia.
Ni lazima utambue kuwa upo upinzani mkibwa katika kuhakikisha haufanikiwi.
Wapo watu wenye tabia za tobia ,sanibalati .............
kazi yao ni kukatisha tamaa,
wamewekwa na wanatumiwa na shetani ipasavyo ili kuhakikisha kazi ya Mungu haifanikiwi bali linakufa.
✨Unachotakiwa /ninachotakiwa kufanya ni kuwa na bidii katika kuombea hilo kusudi na kulifanya bila kujali wakati au upinzani uliopo juu yako kama alivyofanya nehemia.
Na hakika hakuna jambo la kumshinda Bwana
Warumi 8
31 Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Bwana akupe kushinda na zaidi ya kushinda kwa utukufu wake siku zote.
Barikiwa mno
@adzera maneno marco
*TAIFA TEULE MINISTRY*
Maoni
Chapisha Maoni