NGUVU YA KUNYAMAZA


               NGUVU YA KUNYAMAZA. 

MAANA :
Kunyamaza ni hali ya kutojibu /kutoeleza kitu/jambo hata kama* unaweza kujibu

Ni Kitendo cha kukaa kimya .
💫Tukumbuke kwamba katika ulimwengu huu tulionao tunaishi na watu tofauti ,wenye tabia tofauti na wakati mwingine wanakera sana.
Lakin si kila kitu unanatakiwa kujibu /kuongea bali kuna wakati unatakiwa kunyamza.
Na unaponyamaza  si kwamba huwezi kujibu/kuongea au huna akili hapana unanyamaza ili uwe salama.Na wakati umenyamaza unaruhusu Mungu akusemee ,akutetee, yeye mwenyewe aliyemsemaji wa mwisho.

Tujifunze kwa wafuatao:

✍️Musa aliponyamaza watesi wake wakapigwa ukoma.

 Hesabu 12
 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi. Wakasema Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.

👉Miriamu na Haruni wakamsema vibaya Musa baada ya kuoa mwanamke mkushi wakidai si Mungu aliyemruhusu am woe Maana Kama Mungu alimruhusu basi na wao wangesemeshwa.
Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

👆Musa hakuzungumza chochote na kitendo cha Musa kunyamaza Mungu anamtetea Musa na kuthibitisha kuwa ndiye aliyemruhusu Musa  kwa kumpiga Miriamu kwa ukoma.

👉kuna jambo jema unalifanya au Huduma unaifanya alafu unakutana watu aina ya Miriamu ,Hutakiwi kuwasikiliza na kuwajibu chochote ilimradi unauhakika Mungu amekuruhusu kuwa na amani endelea mbele.Maana unaponyamaza Bwana anasimama mwenyewe kukutetea ,kuthibitika kuwa yupo pamoja nawe.

✍️Hana aliponyamaza mume wake akampenda zaidi na Mungu akamfungua tumbo lake akapata mtoto samweli.

 1 Samweli 1 :1-5
Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu naye alikuwa na wake wawili; jina lake mmoja akiitwa Hana, na jina lake wa pili aliitwa Penina; naye huyo Penina alikuwa na watoto, lakini Hana hakuwa na watoto. lakini Hana humpa sehemu mara mbili; maana alimpenda Hana, ingawa Bwana alikuwa amemfunga tumbo.
 
👉Elikana alikuwa na wake wawili (Hana na penina) Hana mke mkubwa hakujaliwa watoto na penina mke mdogo alijaliwa watoto. lakini penina alimsema vibaya Hana kwa kukosa watoto japokuwa Elikana alimpenda sana Hana na a limp a sehemu Mara mbili yaani alizidisha kinyume cha desturi.

🫢Hana nyakati zote alinyamaza hakujibu chochote na kitendo cha kunyamaza mume wake alimpenda zaidi na Mungu akasimama kumtetea na kumjibu hitaji lake la mtoto akampa samweli.

 1 Samweli 2:21
Naye Bwana akamwangalia Hana, naye akachukua mimba, akazaa watoto, wa kiume watatu na wa kike wawili. Naye huyo mtoto Samweli akakua mbele za Bwana.

💫mama ,baba ,kijana katika mazingira magumu  ambayo yaweza kuwa ni:
⭐ndoa
⭐mahusiano 
⭐uchumi
⭐Huduma

📌usipende kujieleza sna kwa mtu
wakati mwingine wewe nyamaza acha Mungu mwenyewe akutetee kama alivyomtetea Hana maana Mungu akikutetea Ina nguvu sana kuliko wewe mwenyewe.

✍️Yesu hakujibizana(alinyamaza) Mungu akamtukuza.

 Wafilipi 2:7-11
  Bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.
Kwa hiyo tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina; ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe, la vitu vya mbinguni, na vya duniani, na vya chini ya nchi; na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI Bwana, kwa utukufu wa Mungu Baba.

👉Yesu Ali pita katika Mengi hata kuukamlisha wokovu kwa mwanadamu na hata alipodharauliwa ,alipotemewa mate ,alinyamaza kimya si kwamba hakua na uwezo wa kufanya jambo lakini alijua nini amekuja kufanya.
Na katika kunyamaza kwake ,kutii kwake,kunyenyekea kwake Baba alimkirimia jina lipitalo kila jina.
Haleluyaa!!                     
 🔥Leo hii tunalitamka jina la Yesu wagonjwa wanapona.
👉Mateka wanawekwa guru.
👉viziwi wanasikia 
👉Viwete wanatembea
👉mapepo yanatoweka.n.k

Haiku wa rahisi lakini katika ugumu kuna ushindi,kuinuliwa na kustawi sana.
Mwambie Mungu katika hali yoyote utakayopitia akupe kunyamaza japo maumivu yake ni makali sana lakini 
📌kunyamaza ni dawa inayotibu.
📍kumbuka hata kama unasababu ya kujitetea wakati mwingine jifunze kukaa kimya maana hata ukiongea hutoeleweka zaidi utaongeza tatizo.
🎉Omba sana na Acha Mungu aseme badala yako utaeleweka zaidi.

1 Petro 3
12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana ni juu ya watenda mabaya 13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? 14 Lakini mjapoteswa kwa sababu ya haki mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu .

 Hitimisho
Aliye wa Mungu huyafanya ya Mungu hata kama itamgharimu kiasi gani kusudi akubaliwe na Baba.kwaiyo yafanye ya Mungu ili ukubalike na Baba wa mbinguni.
Barikiwa sana.

Madam Adzera Maneno Marco
 @Taifa Teule Ministry.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI