SISI NI NURU YA ULIMWENGU
SISI NI NURU YA ULIMWENGU
MAANA
:NURU ni mwanga(sisi ni mwanga wa ulimwengu)
5 Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.
đź“ŤYesu alipokuwepo duniani katika mwili anasema yeye ni nuru ya ulimwengu .
4 Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.
đź“ŤIkiwa Yesu yupo ndani yetu ,yeye aliyenuru na sisi ni nuru ya ulimwengu. Na nuru yetu inaangaza katika ulimwengu yaani watu wanatufahamu tulivyo.
14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima.
đź“Ťsasa kama Sisi ni nuru ya ulimwengu tunatakiwa kufanya itupasavyo kufanya kama watu wa nuru.
mambo muhimu yakuzingatia👇
✍️ Kuishi maisha ya kumpendeza Mungu
21 Bali yeye aitendaye kweli huja kwenye nuru, ili matendo yake yaonekane wazi ya kuwa yametendwa katika Mungu.............................
đź“ŤMaisha yetu na mwenendo wetu umthibitishe Mungu anayeishi ndani yetu na si vinginevyo.
✍️ kujiepusha na kila uovu
3 Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;
12 Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia, basi na tuyavue matendo ya giza, na kuzivaa silaha za nuru.
13 Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu; si kwa ulafi na ulevi, si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.
14 Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.
đź“ŤNdugu yangu Ikiwa bado kuna dhambi/uovu bado upo ndani yako wewe upo gizani maana waliokatika nuru uovu na dhambi si sehemu ya maisha yao.
đź“ŤUnatakiwa kufanya hima uondoke gizani kwa kumkiri na kumpokea Yesu moyoni mwako aondoe Giza na kuweka nuru ndipo utakuwa salama.
✍️ Kuishi kwa upendo
9 Yeye asemaye kwamba yumo nuruni, naye amchukia ndugu yake, yumo gizani hata sasa.
10 Yeye ampendaye ndugu yake, akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo.
11 Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
đź“ŤTunatakiwa kuishi kwa upendo maana sisi ni nuru na aliyendani yetu (Yesu) ni wa upendo ambao hauhesabu mabaya ya mtu ila umejaa msamaha na huruma ya kusidia wenye kuhitaji bila kujali mazingira.
✨Ndugu yangu hakuna njia ya mkato kufika katika ufalme mkuu (Mbinguni )ni lazima kuyaishi maneno ya Mungu na kuitenda haki yake.
Kumbuka👇
19 Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye muhuri hii, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila alitajaye jina la Bwana na auache uovu.
Tengeneza maisha yako sasa na Mungu ,bado neema ya kutubu ipo.
*Hitimisho*
:sisi wa nuruni tutende yanuruni.
Barikiwa sana
TAIFA TEULE MINISTRY
Maoni
Chapisha Maoni