KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.


 KUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU.

Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu

Luka 4:1
Na Yesu, hali amejaa Roho Mtakatifu, alirudi kutoka Yordani, akaongozwa na Roho muda wa siku arobaini nyikani,


 Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni Mungu katika nafsi ya Roho (Yohana 4:24).

Tuendelee..........

📍Uhai wa mwamini unahitaji pumzi ya Mungu ndani yake ili aendelee kuishi na kufanya kazi zake kwa ufasaha na ufanisi.

Pasipo pumzi ndani ya mtu maana yake hakuna uhai.

Katika uumbaji wa Mungu kwa mwanadamu ilihitajika pumzi ya uhai ili iweze kumfanya mwanadamu awe nafsi hai hata kwa hiyo pumzi aweze kuongozwa kwayo. "


 Mwanzo 2:7 
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai .


📍Kristo Yesu alikuja duniani kumrudisha tena mwanadamu katika nafasi yake aliyokuwa ameiacha baada ya anguko.

Kwa kazi ya msalaba, Yesu ameleta wokovu ili kila anayemkubali anapata nafasi ya kuzaliwa mara ya pili. 

Mtu anapozaliwa mara ya pili, maana yake ameumbika mara ya pili na amekuwa kiumbe kipya. 

2 Wakorintho 5:17
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.

Kama ambavyo kwa mwanadamu wa kwanza Mungu alimpulizia pumzi ya uhai ili awe nafsi hai hata aongozwe kwayo, hata kwa huyu anayezaliwa mara ya pili anahitaji pumzi ya uhai ili aweze kuwa na ushirika na Mungu.

📍Roho Mtakatifu ndiyo pumzi pekee ya uhai inayoweza kumfanya mtu aliyezaliwa mara ya pili kuendelea kubaki na uhai hata kuwa na ushirika na Mungu.

Uhai wa mwamini unafanywa na uwepo wa Roho Mtakatifu ndani yake. Pasipo Roho Mtakatifu ndani ya mwamini ni sawa na gari lisilokuwa na mafuta maana yake haliwezi kwenda popote.

📍Mwamini unahitaji kuwa na mwongozo wa Roho Mtakatifu pekee katika ulimwengu huu wa uovu mwingi.

✍️✍️ Tunaongozwaje na Roho Mtakatifu? 

📍Ili uongozwe na Roho Mtakatifu lazima kwanza Roho Mtakatifu awe na nafasi ndani yako. Mambo yafuatayo yanahusika;

     👉🏽Lazima uwe umeokoka kwa kutubu dhambi zako ukimaanisha kuziacha kabisa.

 Matendo ya Mitume 2:38
Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu

  

  👉🏽.Kama umeokoka kubali kuiacha dunia.

 Warumi 12:2
Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.

👉🏽. Tamani/kuwa na kiu naye.

 Yohana 7
37 Hata siku ya mwisho, siku ile kubwa ya sikukuu, Yesu akasimama, akapaza sauti yake akisema, Mtu akiona kiu, na aje kwangu anywe.
39 Na neno hilo alilisema katika habari ya Roho, ambaye wale wamwaminio watampokea baadaye; kwa maana Roho alikuwa hajaja, kwa sababu Yesu alikuwa hajatukuzwa.

📍Utendaji kazi wa mwamini unahitaji kuongozwa na Roho Mtakatifu. Mwamini asiyeongozwa na Roho Mtakatifu ni hatari sana katika ulimwengu huu wa uovu maana anaweza kutumiwa na adui kwa ajili ya kuuwa kanisa.

Wakati Yesu anataka kupaa mbinguni alisisitiza wanafunzi wake wakae kwanza mpaka wavikwe nguvu za Roho Mtakatifu ndipo waingie kufanya kazi yake.

 Luka 24:49
 Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu.

 Matendo ya Mitume 1:8
Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.

🤷‍♀️Ni maombi yangu kwako utamani sana kuongozwa na Roho Mtakatifu katika jambo au hatua yoyote. Lolote ufanyalo fanya kwa kumshirikisha yeye wala usiende peke yako.

Musa alimwambia Mungu uso wako usipoenda nami mimi siendi.

Kutoka 33
15 Naye akamwambia, Uso wako usipokwenda pamoja nami, usituchukue kutoka hapa.
16 Kwa maana itajulikanaje kuwa nimepata neema mbele zako, mimi na watu wako? Siyo kwa sababu unakwenda pamoja nasi, hata mimi na watu wako tutengwe na watu wote walio juu ya uso wa nchi?

Miongoni mwa mambo machache ya kuzingatia;

👉🏽. Maombi. Luka 18:1 

👉🏽 Usafi (Utakatifu). 1Petro 1:16

👉🏽Ibada.

  Barikiwa sana.               

Madam: Adzera Maneno marco

 *Taifa Teule Ministry* .

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI