KWANINI WATU WA DUNIA WANA MAFANIKIO KULIKO WAKRISTO AMBAO WAO NDIYO HUSEMA WANA MUNGU ??

 

KWANINI WATU WA DUNIA WANA MAFANIKIO KULIKO WAKRISTO AMBAO WAO NDIYO HUSEMA WANA MUNGU

Na: Minister Sudai

BWANA YESU ASIFIWE WANA NA BINTI ZA MUNGU

Leo tuangalie ujumbe unaosema

πŸ‘‰jinsi ambavyo watu wasiomjua kristo Yesu wanaweza kuwa na kila kitu tulichopaswa kuwa nacho kuliko sisi tunaomjua Mungu

 SOMA HAPA TUONEπŸ‘‡πŸ‘‡

Mithatli 17:2

Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.

TUONE MAANA ZA MANENO KADHAA HAPA 

πŸ‘‰neno MTUMWA humaanisha mtu ambaye si mwanafamilia fulani na hausiki katika urithi wa baba au wazazi wa familia hiyo.. na mara nyingi huwa ni mtu anayeishi hapo kwa lengo la kufanya jukumu au kazi fulani kwenye hiyo nyumba... pengine ni kazi za ndani n.k

πŸ‘‰neno KUTAWALA huwa linamaanisha namna fulani ya mtu kuwa juu ya kitu fulani au kuwa na amri juu ya kitu fulani au kuwa na umiliki wa kitu fulani....

πŸ‘‰neno MWANA limesimama kumuonyesha mtoto wa familia husika na ni yule ambaye kila alichonacho baba yake ni urithi wake, yaani yeye ni mtawala na mmiliki wa mali zote baada ya baba yake kihalali na kwa haki kabisa

πŸ‘‰neno BUSARA Husimama kuonyesha jumla ya utendeji wa mambo katika namna nzuri na njia sahihi kulingana na utar…

sasa biblia inasema kwamba mtumwa anayetenda au anayeenenda kwa busara atapata vitu au urithi kutoka kwa tajiri, kuliko mtoto wa tajiri ambaye anafanya mambo ambayo ni ya aibu...

 

TAJIRI ni Mungu na sisi tunaomjua au tuliompokea YESU KRISTO ni watoto wa Mungu..

na watu wasimpokea Kristo hao ndio wanafananishwa na watumwa yaani si wahusika au warithi wa baraka za Mungu wetu....

 YOHANA 1:12-13

 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu

 

WARUMI 8:17

Hivyo, ikiwa sisi ni watoto, basi tu warithi, warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo, naam, tukiteswa pamoja naye tupate pia kutukuzwa pamoja naye

 

WAGALATIA 5:19-21

Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu

 

 UNAONA SASA mpaka kufika hapo tumeshajua wana wa Mungu ni watu gani na wasio watoto wa Mungu ni watu gani.....

pia tumeshatambua kumbe watoto wa Mungu ndiyo wenye urithi wa Mungu kwa haki na wale wasio wa Mungu si warithi wa baraka za Mungu kwa halali....

NI HIVIπŸ‘‡

Sisi ni watoto wa Mungu, na ndiyo warithi wa Mungu, na kuna taratibu ambazo baba yetu anataka tuziendee ili kumrudishia au kumpa yeye heshima kama baba yetu.. na kuna mambo ambayo hataki sisi tuyafanye maana hayo yanaleta aibu kwenye ufalme wetu na hayampi BABA yetu heshima bali yanampa aibu....

lakini si hivyo tu ….. bali tujue kwamba sisi ni watoto na hivyo ndiyo tunatakiwa kuwa na urithi aua braka ambazo BABA yetu ametupatia watoto wake na tunakuwa nazo kama tukifuata tu zile taratibu ambazo BABA yetu anataka tuzifuate...

baraka nyingi ambazo tulitakiwa kuwa nazo sisi kama watu waliookoka chaajabu ni kwamba hatuna lakini wenzetu ambao si warithi wa mali hizo lakini ndizo wanazo..... je ji kwanini mambo yanakuwa hivyo???

 

jibu ni rahisi sana

Ni kwasababu wao wanachukua hatua za kutenda mambo kwa usahihi kuliko sisi na ndiyo maana wao wanachukua au wanapata urithi wetu kirahisi na ni BABA yetu ndiye anayewapa wengi wao kwasababu tu wanafanya mambo yao kwa kutumia ustarabu au hatua sahihi kuliko sisi...

UTAJIRI Ulitakiwa kuwa ni wa watoto wa MUNGU lakini cha ajabu ni kwamba watu wasiomjua Mungu ndiyo wanakuwa matajiri kwasababu wao wamechukua hatua ya kuufuata utajiri yaani KUFANYA KAZI KWA BIDII, lakini sisi ambao ni watoto, tumeacha kufuata sheria ya BABA ya kufanya kazi ili tuwe na baraka za utajiri na badala yake tumekuwa ni watu wavivu tusiopenda kufanya kazi.... kwahiyo hiyo hali inaleta aibu kwenye ufalme na badala yake wale ambao ni watumwa ndiyo wanahesabisa urithi wa Mungu yaani baraka za utajiri kwasababu wao wametenda kwa busara kwa kufanya kile kitu sahihi kwaajili ya mtu kufikia utajiri

Wanachotuzidi watu wa dunia hii ni kwamba wanatumia maarifa ya kimungu na kuyatendea kazi, yaani ni watu wa vitendo zaidi pale wanapopata ujuzi....

lakini watu waliopo kanisani ni watu ambao kila siku wanafundisha ujuzi huohuo isipokuwa wao hawachukui hatua yoyote kulingana na kile ambacho wanafundishwa .....

sasa formula ya kufanikiwa ni kuchukua hatua na siyo kujifunza tu bila kuchukua hatua yoyote.....

kwasababu unaweza kuwa na mbinu nyingi sana za kufikia malengo lakini usiochukua hatua yoyote basi jua kabisa kwamba utakufa na mbinu zako katika hali hiyohiyo......

 kumbuka imani yako ambayo unaipata kwa kusikia neno la Mungu huwa inaonekana kuwa hai ikiwa tu utachukua hatua kwa kile ulichokisikia.... lakini ukisikia na usichukue hatua basi imani yako inakuwa imekufa...

WARUMI 10:17

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo

 

 YAKOBO 2:26

Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Kwahiyo unaposikia jambo/maarifa maana yake unaipokea IMANI na unapochukua hatua juu ya maarifa uliyoyapata au neno ulilolisikia basi imani yako inakuwa HAI na inazaa matunda inaleta matokeo....  lakini kusikia pekeyake haikusaidii.... na ndiyo maana Biblia inasema hiviπŸ‘‡

 YAKOBO 1:22

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu.

 

hebu jiulize

ni mambo mangapi ambayo huwa unafundishwa toka umeanza kusikia mafundisho kanisani au kutoka kwa watumishi wa Mungu..??

je huwa unachukua hatua?

hebu jiulize ungekuwa unachukua hatua ya yale unayofundishwa ungekuwa wapi kihuduma, kiuchumi, kifamilia n.,k....??

 

jibu ni kwamba ungekuwa mbali zaidi hata ya wale watumwa ambao kiasiri si watoto wa Mungu....

lakini haujafika huko kwasababu umekuwa msikiaji na si mtendaji ila wao ni watendaji wa kila mbinu ambayo wanaisikia kwamba inaleta mafanikio... tena hasa pale wanapoisikia kutoka kwa watumishi wa Mungu... wanaichukua na kuifanyia kazi vizuri na ndiyo maana wanafanikiwa....

kama wao wanachukua hatua baada ya kusikia lakini wewe unaishia kusikia tu bila kuchukua hatua... hapo kati ya wewe na wao ni nani mwenye imani anayoitaka Mungu na inayoleta matokeo????

 

kimsingi ni wao ndiyo wana imani kuliko wewe ambaye upo kanisani kila siku....

na wanapofanikiwa wao kuliko wewe tambua kwamba

πŸ‘‰hutaweza kuwahubiria kwamba Yesu anaweza

πŸ‘‰Hutaweza kuwaambia kwamba Mungu wako ni mkuu zaidi ya vyote

πŸ‘‰hutaweza kuwatoa dhambini kukufuata wewe

πŸ‘‰hutaweza kuwa na nguvu katika kuwatangazia ufalme wa Mungu

 

na hiyo ni kwasababu WAMEKUZIDI KILA KITU.. Na wakati mwingine wataona kwamba wakiingia kwenye ufalme wenu yaani kwenye wokovu, basi watafanana na wewe, kwasababu siku zote mtu alivyo huitambulisha familia yake....

 

πŸ‘‰tukimkuta mtu ana tabia mbaya basi tunaamini chanzo ni kule alikokulia yaani familia yake

πŸ‘‰ukimkuta mtoto njiani yuko lafu, mchafumchafu, maana yake unaweza kuamini kwamba wazazi wake ndiyo chanzo na unapata picha nzima ya kwao

JE HIYO KWA MUNGU INALETA HESHIMA AU AIBU??... NI AIBU

Lakini akiwepo mkristo mwenye kusikia mbinu za kimungu na kuzifanyia kazi basi atafanikiwa sawasawa na neno la Mungu..... na wale watumwa au wasiomjua Mungu ambao wanazitumia mbinu za Mungu tu basi hao nao pia watafanikiwa katika sekta hiyo ya kiuchumi n.k kwahiyo wote watapata baraka kwasababu wamechukua hatua za kufanya mambo kwa busara... na ndiyo maana Biblia inmasema kuwa

 

Mithatli 17:2

Mtumwa atendaye kwa busara atamtawala mwana atendaye mambo ya aibu; Tena atapata sehemu ya urithi kati ya ndugu.

HATA LEO

πŸ‘‰Kuna watu hawajaokoka lakini ni waaminifu kwa wake/waume zao lakini unakuta mkristo ni mzinzi yaani anakosa kuwa mwaminifu kwa mwenza wake.. lakini sheria ya BABA yake inasema kuwa...... Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. WAEBRANIA 13:4

πŸ‘‰Kuna watu hawajaokoka lakini hawalipi kisasi wala hawamweki mtu moyoni kwa chuki (japo si wote) lakini unakuta mkristo anafanya mambo ya aibu kwenye ufalme wetu yaani anamchukia mwenzake na hataki kusamehe kabisa na bado anajiita mkristo angali sheria ya BABA yetu inasema kuwa... Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa  LUKA 6:37

SASA kanisa la Mungu lazima tuwe na macho ya kuona kwamba tunaleta aibu zaidi kuliko heshima kwa BABA        yetu Mungu pale tunapofanya mambo ambayo hata walioko duniani hawayafanyi.....

 

lakini pia tutambue kuwa walioko duniani wataendelea kuonekana na maana kuliko wewe kwasababu ya uzembe wako wa kutokufanyia kazi kile ambacho Mungu anakufundisha kila siku kupitia watumishi wake.....

KAMA WEWE UNAONA KABISA KWAMBA HUWA HUCHUKUI HATUA YA KILE ANACHOKUAMBIA MUNGU NA KULETA AIBU KWENYE UFALME WA MUNGU KAMA MTOTO WA MUNGU.... BASI HAPO ULIPO ZUNGUMZA NA MOYO WAKO, WALA USICHUKULIE MZAHA, TAFUTA ENEO LENYE UTULIVU UKIWEZA PIGA GOTI ZUNGUMZA NA MUNGU WAKO... MWAMBIE AKUSAMEHE KWAKUWA MJINGA NA MZEMBE MWENYE KULETA AIBU NA SI HESHIMA.....

 

ukishamaliza natamani uweke mbinu sahihi ili uanze kuwa mtoto wa Mungu ambaye utaleta heshima kwa BABA......

unaweza ukamuomba ROHO MTAKATIFU akusaidie na kukukumbusha wakati wote ili uwe unatenda sawasawa na neno la Mungu na wewe uanze kuwa mwaminifu pale unapoambiwa na Mungu basi ufanye sawasawa na Neno lake NA HAPO UTALETA HESHIMA ZAIDI KWA MUNGU na Mungu atakuheshimu mtumishi wake mwema.....

MUNGU AKUBARIKI SANA

 

Mimi ni ndugu yako niliye mdogo kuliko wote mbele za Mungu..

Taifa Teule Ministry

Minister Mathayo Sudai

0744474230/0714732009

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI