HATARI YA MTU ANAYEJIPENDEKEZA
Bwana Yesu asifiwe wana wa Mungu...
karibu tujifunze kitu juu ya watu wenye tabia za kujipendekeza....
KUJIPENDEKEZA ni kutoa sifa au kumsifu mtu zaidi ya sifa alizonazo au kumsifu kwa sifa ambazo si zake kwa lengo la wewe kupata kitu kutoka kwake....
katika maisha ya leo kuna kitu ambacho watu huwa hwajui madhara yake na jinsi ambavyo kuna hatari nyuma ya mtu ambaye anajipendekeza kwako...
ukiona mtu anajipendekeza kwako maana yake ni kwamba anakuwa anakupa sifa zaidi, na wakati mwingine sifa anazozitaja zinakuwa si zako kabisa, na wakati mwingine sifa yako lakini jinsi anavyokusifu ni zaidi ya hiyo sifa ilivyo... lAKINI lengo la yeye kufanya hivyo siyo kukuonyesha kwa watu kwamba wewe ni mzuri sana bali kuna faida amabyo anakuwa anaitaka kutoka kwako...
✋pengine ni pesa
✋pengine anataka apate cheo fulani
✋pengine anataka umpe nafasi fulani ya kipekee n.k
HEBU TUSOME MAANDIKO HAPA CHINI
MITHALI 29:5
Wenye kujipendekeza kwa jirani yake, Hutandika wavu ili kuitega miguu yake.
Mwenye kujipendekeza ni kama mpambe fulani ambaye anakuwa kwako kwa lengo lake fulani... na atakuwa tayari kukufanyia kitu fulani ili tu aonekane mwema kwako na huku akikusifia pale unapokuwa naye lakini hatari ni kwamba sifa hizo anazitoa ndivyo sivyo...
je mwenye kujipendekeza kwako anakutandikiaje nyavu za kunasa au kutega miguu yako....
Biblia inaposema kuhusu kutega miguu inamaanisha mtu anakuwa ametegwa katika kutembea kwake na Mungu... yaani mtu akisababisha wewe ukakosana na Mungu maana yake aliitega miguu yako...
sasa huyu mtu mwenye kujipendekeza anakutega miguu kwasababu....
1. unaweza kuanza kuwa na kiburi....
mtu anapokusifu sana anaweza kukufanya ukajiona kuwa wewe ndiyo kila kitu na hakuna usiloliweza.... saa unapoanza kuwa na majivuno kama hayo basi jua utaanguka na hutaweza kutembea na Mungu kwasababu Mungu hapendi mtu mwenye majivuno na yeye mwenyewe Mungu huwapinga watu wa namna hiyo...
1 PETRO 5:5
Kadhalika ninyi vijana watiini wazee. Jivikeni unyenyekevu, mnyenyekeane kwa maana, Mungu huwapinga wenye kiburi bali huwapa neema wanyenyekevu.”
kiburi kitakuja kwasababu ya vile ambavyo umepewa sifa nyingi na zile zisizokufaa
1.
Mtj
AMINA
JibuFuta