TAFUTA KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.
TAFUTA KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.
Na Mwl: ADZERA MANENO MARCO
Karibu katika kipindi hiki tujifunze kama watu wa Mungu tunavotakiwa kuwa na ndivyo impendezavyo Bwana.
TAFUTA KWA BIDII KUWA NA AMANI NA WATU WOTE.
Tusome hapa
Waebrania 12
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Kwa neno hili mwana wa Mungu unatakiwa kujua kwamba :
✍️Tunaishi wa watu wenye mitazamo tofauti.
✍️Tunaishi na watu wa rika tofauti
✍️Tunaishi na watu wenye uwezo tofauti (wenye nacho na wasio nacho)
✍️Tunaishi na watu wenye tabia tofauti
wengine wakorofi,wachokozi na wenye matusi na wenye lugha mbaya.
✍️Tunaishi na wetu wenye hila wasiopenda mafanikio ya wengine......
✍️Tunaishi na watu ambao kwao dhambi ni kawaida maana hawana hofu ya Mungu ndani yao.
✍️Tunaishi na watu ambao mtu anapolia,na kuhuzunika kwao ni kicheko.
Je sisi kama watu tunaomjua Mungu tunatakiwa kufanya nini..............................................
💫💫Hatutakiwi kufanya na kuyaishi 👆
kwasababu tunamjua Mungu wetu hapendezwi kabisa na mambo mabaya.
✍️✍️✍️watu wa Mungu tunatakiwa kutafuta amani kwa juhudi ili kumpendeza Mungu wetu........
kwa kufanya haya 👇
⭐kutafuta kupatana na kila mtu katika mazingira yanayokuzunguka .
⭐Kuzungumza lugha nzuri katika mazingira yoyote (lugha chafu si asili ya Mungu).
⭐Kuchukuliana na watu tunaoishi nao (nyumbani ,kazini n.k).
⭐kusamehe na kuachilia kabisa (usiweke kinyongo juu ya mtu Fulani kwa kuwa alikukosea).
⭐Kuwa na upendo,unapoona mwingine amekosea mwonye kwa upendo na si kumgombeza atazidi kupotea.
⭐Tujikite katika kuwarejeza wengine kwa Mungu kwa kuzitubu dhambi zao na kuziacha kwa kuwaombea na kuwafundisha kweli ya Mungu.
💥Mtu wa Mungu hutakiwi kulipiza kisasi wala kumhukumu mtu ila unatakiwa kumsaidia arejee kwa Mungu wake.
Warumi 12
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
💥watu wa Mungu tuyatende mema tuzidi kupata Kibali kwa Bwana.
Hitimisho
Hakuna namna nyingine tunaweza kumwona Mungu katika maisha yetu nje na kutafuta amani kwa bidii maana *NDIO* namna ya kutufanya kuwa safi (watakatifu )na wenye kibali mbele za Mungu wetu.
UbarikiwenakutunzwanaMungu.
Na Mwl adzera maneno marco ... *TAIFA TEULE MINISTRY.*
Maoni
Chapisha Maoni