USIWE KAMA NGURUWE ANAYEOGA NA KISHA KURUDIA MATOPE


 USIWE KAMA NGURUWE ANAYEOGA NA KISHA KURUDIA MATOPE

Wakolosai 2:20-22

[20]Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, [21]Msishike, msionje, msiguse;[22](mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu?

  Bwana Yesu asifiwe sana 

Nawasalimu kwa jina la YesuYesu. 

Kwakuwa tulikombolewa kutoka kwenye dhambi, laana mbalimbali na mateso,

Tukatolewa kwenye asili zetu za matambiko na  mizimu ya makabila yetu basi hatupaswi kurudia huko kwenye Mambo yasiyofaa maana tumeokolewa kwa neema. 

Na ukumbuke ukisharudi nyuma gharama ya kuanza kuitafuta neema tena unaweza usiipate mpaka Mungu mwenyewe aamue kukuokoa tena. 

Sikiliza🧏🧏‍♀️ mama, baba, kijana✍️

Kuna vitu vingine haupaswi hata kuvigusa

Wala kuonja,  Wala kushika tena kwasababu;ulishaachana navyo basi haupaswi kuvirudia tena. Umeokoka wewe😊

Unaweza ukajihoji nafsi yako namna unavyoenenda ili roho yako iwe salama. 

Mfano 

Ulizowea kutoa sadaka kwa mizimu ya kwenu. 

Kwasababu umeokolewa haupaswi kushiriki tena kwa sadaka, au ibada zao hata kama huendi kimwili. 

Usiseme mi nawapa tu hizo sadaka za mizimu ila mimi siwezi kwenda😁😊🏃‍♀️🏃‍♀️

Tambua kwamba uwepo wako hapo kwenye ibada za sanamu unawakilishwa na sadaka uliyoitoa hata kama wewe haupo pale kimwili. 

Mathayo 6:21

[21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.

Hapo unakuwa umeipeleka nafsi yako kushiriki zile ibada hata kama muda huo upo kwenye ratiba zako nyingine. 

Nadhani unanielewa hapa😁✋

Yamkini dhambi ya uzinzi ilikutesa sana basi sasa umeshaokoka umeokolewa kwa neema tu, usitamani tena kujihusisha na mambo yote ya uzinzi na yanasababisha uzini. 

Zuia tamaa yako ya mwili isije ikakupeleka jehanamu kwenye ziwa la moto wa milele( huko ni vilio na kusaga meno). Roho mtakatifu akusaidie sana. 

Warumi 8:13

[13]kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi.

Yamkini ulikuwa Unafanya biashara fulani zisizo na utukufu kwa Mungu ( Biasahara haramu) na Mungu akakuokoa, 

Basi haupaswi kuzifanya tena hata Kama zilikuwa zinakupa faida kubwa kiasi gani kwasababu utakuwa unajitia unajisi tena roho yako. 

🔥Ni kama nguruwe kuogeshwa kisha kuyarudia matope

Yamkini ulizowea kudanganya watu, ili ufanikiwe jambo fulani, (utapeli) 

Usitamani mafanikio yasiyokuwa na jasho

Fanya kazi halali Mungu atakuinua zaidi ukimtumaini yeye. 

Maana Mungu anasema yeye atatupatia zaidi ya yale tumwombayo. 

Waefeso 3:20

[20]Basi atukuzwe yeye awezaye kufanya mambo ya ajabu mno kuliko yote tuyaombayo au tuyawazayo, kwa kadiri ya nguvu itendayo kazi ndani yetu;

Yamkini kuna marafiki au mazingira fulani ulizowea kwenda na baada ya kuokoka  moyo unakuhukumu ukienda au ukiambatana na hao marafiki huoni raha, usiende tena. 

Na ili upande ngazi kiroho yaani kutoka utukufu hadi utukufu ni lazima uepuke mambo yote yanayokupelekea wewe kurudia uovu yaani dhambi. 

Huwezi kupandishwa ngazi ikiwa wewe ni mtu wa namna hiyo, badala yake utabaki na wokovu wa kawaida tu, wokovu jina ( wa mazoea) . 

Hitimisho

Nikukumbushe hili kwamba;

WALIO ROHONI HUONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU

Fanya Mambo yakupasayokufanya kwa mapenzi ya Mungu Baba pekee.


Barikiwa sana.


Mwl Beata Tito

@Taifa  Teule Ministry

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI