Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Oktoba, 2023

BINTI USIONGOZWE NA MACHO YA WATU

 BWANA Yesu ASIFIWE mabinti wazuri kabisa... Leo Ni siku nyininge ambapo natamani tujifunze Jambo moja zuri San kwaajili ya mamufaa yako... Ni kuhusu  MACHO YA WATU YANAVYOHARIBU MAISHA YA BINTI... Ni kweli kabisa kwamba kwenye jamii huwa Kuna watu ambao huongozwa na macho ya watu fulani 👉watu wengi Leo hii wanafanya uamuzi fulani kwasababu ya watu fulani ambaonwapo kwenye jamii yao... 👉ukiangalia maneno ya Yesu alipokuwa akizungumza Ni ishara kamili kwamba alizungumza like alichotumwa na Wala si Kama vile wanavyotaka watu..... Yohana 6:38 Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Sasa hii ilimfanya Yesu kufanya Jambo sahihi kwa wakati ule bila kujali kwamba watu watalikubali au watakataa 👉sasa niketoa mfano huo wa Yesu ili kukuonyesha ni kwa namna gani mabinti wenge na vijana wengi huingia katika ndoa na watu wasiosahihi kwasababu tu ya kuwatazama watu wanaowazunguka..... 👉Ni kweli kwamba Kuna sifa fulani Binti a...

MTU MZUSHI MKATAE

Picha
                                   MTU MZUSHI MKATAE Tito 3:10-11 Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae;  ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.   Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu...karibu katika ujumbe wa leo ambapo tunangalia kuhusu mtu mzushi na nini Biblia inataka tufanye kwa mzushi... Mzushi ni I mtu anayependa kusema mambo asiyo ya kweli ili kukosanisha wengine... 👉Mzushi huwa na lengo la kutawanyisha watu wenye umoja 👉Mzushi huwa na lengo la kukufarakanisha na Mungu 👉Mzushi huwa na ajenda ya kupindisha mapenzi ya Mungu kwako.. 👉Mzushi huwa haonyeki anapokosea Sasa hayo yalikuwa ni maneno ya Paulo alipokuwa akizungumza na mwanae wa kiroho yaani Tito ambaye hapa alikuwa ni mtu, kijana ambaye anaanza huduma...

ASIYEFAA USIMPE KITAKATIFU ATAKUUMIZA

Picha
  ASIYEFAA USIMPE KITAKATIFU ATAKUUMIZA  Mathayo 7:6 [6]Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua. Bwana Yesu asifiwe sana watu wa Mungu... Leo ni siku nyingine karibu tujifunze kuhusu neno la ujumbe wa Leo ...MATHAYO 7:6 Sasa hapo ukitazama ni kwamba Yesu alitoa kama agizo la moja kwa moja kwamba watu wake wasiwape mbwa kilicho kitakatifu.. Wala wasitupe lulu ( vitu vya thamani ) mbele ya nguruwe.. NA hapo mwisho akatoa madhara na sababu kwanini usifanye hivyo... MBWA Hapa Biblia imetumia neno mbwa si kwa maana ya mbwa mnyama bali ..inataka tuzitafakari sifa za mbwa kisha tuone watu wenye sifa hizo na hao ndio ambao hatutakiwi kuwapa kitakatifu... Sifa za mbwa ni kama vile kurarua, kuyarudia matapishi, kuumiza pale anapokuuma hata kukusababishia kifo n.k NGURUWE Lakini pia nguruwe ametumika kuonyesha picha ya tabia ambazo watu wanazo na sisi hatutakiwi kuwapa vitakatifu... Sifa za ...

KUWA MAKINI NA MAMBO HAYA MANNE KWENYE UCHUMBA

Picha
  KUWA MAKINI NA MAMBO HAYA MANNE KWENYE UCHUMBA Bwana Yesu asifiwe mabinti wazuri ndani ya Kristo Karibu katika kujifunza mambo manne kati ya mengi mazuri unayotakiwa kuyafanya kila siku kama unajiandaa kuwa na Familia nzuri... Kwanza awali ya yote ni lazima ujue kuwa familia inaundwa na BABA, MAMA pengine na watoto... 👉Hao wote wanamchango mkubwa sana katika kuisimamisha nyumba hiyo... 👉Lakini ndani ya Biblia ni mtu mmoja tu ndiye mwenye uwezo wa kuivunja nyumba na huyo si mwingine bali ni MWANAMKE na kibaya zaidi anao uwezo wa kuivunja kwa mikono yake mwenyewe... Mithali 14:1 [1]Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake;  Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe. Sasa tutoke huko...Leo tuangalie mambo manne ambayo unatakiwa tuyatazame kila siku kama wewe ni binti unayejiandaa au unayehitaji kuingia ndani ya ndoa.. HAYA HAPA 👇 1: MUOMBEE MUME WAKO Unapokuwa umepata mchumba au hata kama hujapata Basi ni lazima ujue kuwa wewe ni mtu ambaye utakamilisha ...

JE UNA UPENDO WA KWELI

Picha
 JE UNA UPENDO WA KWELI ? Bwana Yesu asifiwe asifiwe watu wa Mungu, Karibuni katika siku nyingine ambapo tutatazama jinsi ambavyo tunatakiwa kuonyesha upendo si kwa Mungu tu bali na kwa watu wingine tunaoishi nao.... Kuna namna ambayo Mungu anauona upendo kama upendo na si kama wanadamu Wengi katika mataifa wanavyotazama ... Hebu soma hapa👇 Warumi 13:8-10 [8]Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria. [9]Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako. [10]Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria. Anaannza kwa kusema MSIWIWE 👉Sasa kuwiwa ni kama kudaiwa kitu, au kuwa na deni na mtu fulani... 👉Anasema msiwiwe na mtu chochote isipokuwa kupenda.... Hapa ni lazima ujue kuwa sheria ya Mungu inamtaka kila mtu apendane au ampende mwenzake au ndugu yake... NA kwa kufanya hivyo maana yake un...

KUDHARAU NI DHAMBI

Picha
                 KUDHARAU NI DHAMBI Bwana Yesu asifiwe watu wa MUNGU, leo ni siku nyingine ambayo Mungu ametupa kibali cha kuendelea kuwa salama katika yeye. Naomba tujifunze kuhusu ujumbe wa leo unaotoka kwenye kitabu cha Mithali 14:21...... Hapo Biblia inasema kuwa 👇 "Amdharauye mwenzake afanya dhambi; Bali amhurumiaye maskini ana heri" . Sasa ukianza kulitazama vizuri neno hilo utagundua kitu cha awali kabisa kuhusu DHARAU na namna dharau inavyoweza kumfanya mtu kukaa mbali na MUNGU. Na dharau inamtenga mtu na Mungu kwasababu ni dhambi... 👉 jambo hili yafaa uwe nalo makini pale ambapo utakuwa unaishi huku ukiwa na vya ziada kuliko wengine kwasababu dharau mara nyingi huwa kwa mtu mwenye kitu zaidi ya wenzake.... 👉 wengine wanapoanza kumiliki gari zuri tu, anaanza kudharau wenzake 👉 mwingine akifanikiwa kiuchumi kuliko wenzake basi anaanza kuwadharau wengine 👉 mwingine akijua tu kuwa yeye noi mzuri basi uzuri wake unafanyika sababu y...

JAMBO LA KUFANYA UNAPOUGUNDUA UZURI WAKO

Picha
 JAMBO LA KUFANYA UNAPOUGUNDUA UZURI WAKO Bwana Yesu asifiwe sana watu wa Mungu, mabinti ndani ya Kristo.. nomba leo tujifunze jambo moja la singi sana kwaajili ya afya yako ya kiroho, kimwili na ndoa yako pia. unajua kila mtu huwa ana desturi ya kujiona na kujijua pale anapojitazama au kuambiwa na mtu kuhusu uzuri alionao..... 👉mabinti wengi huujua uzuri wao pale wanapojitazama kupitia vioo n.k 👉lakini katika kuujua uzuri wake binti huyo hujenga kitu kwenye fikra yake cha kumuhusu yeye.. na wengine huanza kuishi na kufanya mambo sawasawa na vile alivyojiona kwenye kioo. 👉wengine huanza kufanya mambo mabaya wakiutazama uzuri au urembo wao kama kigezo cha kufanya hivyo 👉Wengine huanza kujiingiza kwenye mahusiano kwa kigezo cha uzuri wao 👉wengine huanza kuona kwamba wao ni bora kuliko wengine 👉wengine huanza kufikiri wanauwezo wa kuwakamata au kuwateka wanaume kadiri wapendavyo 👉na wengine huanza kufikiri wanaweza kuwa na mwanaume yeyote atakayemuhitaji soma hapa Mithali 31:30...

EPUKA KUWA MKOSESHAJI, UTAANGAMIZWA...

Picha
 EPUKA KUWA MKOSESHAJI, UTAANGAMIZWA... BWANA Yesu asifiwe watu wa Mungu, leo ni siku nyingine ambapo tutaangalia somo letu zuri la kuhusu kumkosesha Mtu mwingine.... soma hapa             MWISHO WA SOMO KUNA USHUHUDA MZURI KWA AJILI YAKO, karibu sana Mathayo 18:7     Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!     KUKOSESHA Huku kunatoa tafsiri ya kufanya jambo ambalo litafanyika kikwazo kwa mtu mwingine katika kufikia pale ambapo anatakiwa kufika sawasawa na mapenzi ya Mungu.  na jambo pekee ambalo pengine linaweza kumfanya mtu mwingine kushindwa kufika pale anapotakiwa kufika ni DHAMBI kumbe ukifanyika sababu ya mtu mwingine kufanya dhambi maana yake UNAMKOSESHA mtu huyo kufanya mapenzi ya MUNGU. Au unapomzuia mtu asifanye mapenzi ya Mungu, maana yake unamkosesha....kwamfano mchungaji au m...