KUDHARAU NI DHAMBI
Bwana Yesu asifiwe watu wa MUNGU, leo ni siku nyingine ambayo Mungu ametupa kibali cha kuendelea kuwa salama katika yeye.
Naomba tujifunze kuhusu ujumbe wa leo unaotoka kwenye kitabu cha Mithali 14:21......
Hapo Biblia inasema kuwaπ
Bali amhurumiaye maskini ana heri".
Sasa ukianza kulitazama vizuri neno hilo utagundua kitu cha awali kabisa kuhusu DHARAU na namna dharau inavyoweza kumfanya mtu kukaa mbali na MUNGU. Na dharau inamtenga mtu na Mungu kwasababu ni dhambi...
πwengine wanapoanza kumiliki gari zuri tu, anaanza kudharau wenzake
πmwingine akijua tu kuwa yeye noi mzuri basi uzuri wake unafanyika sababu ya kuwadharau wengine..
lakini leo ninatamani ujue kuwa kuwadharau wengine ni dhambi na hiyo ni kwasababu unapoonyesha kumdharau mtu mwingine maana yake unaudharau uumbaji wa Mungu, kwasababu alivyo mtu ni matokeo ya uumbaji wa Mungu hivyo usimdharau mtu ni DHAMBI...
πkuna mtu huwa anapenda kuwaheshimu matajiri tu kwakudhani kuwa ndiyo watu wazuri kuliko maskini
πmwingine utamkuta ni mtu wa kuwabagua watu kwa kutazama hali zao, elimu zao, kabila, kipato, n.k bila kujua kwamba anafanya dharau...
hebu soma habari hii
5 Ndugu zangu, sikilizeni: Je, Mungu hakuwachagua wale walio maskini machoni pa ulimwengu kuwa matajiri katika imani na kuurithi Ufalme aliowaahidi wale wampendao? 6 Lakini ninyi mmemdharau yule aliye maskini. Je, hao matajiri si ndio wanaowadhulumu na kuwaburuta mahakamani? 7Je, si wao wanaolikufuru Jina lile lililo bora sana mliloitiwa?
8 Kama kweli mnaitimiza ile sheria ya kifalme inayopatikana katika Maandiko isemayo, “Mpende jirani yako kama unavyoipenda nafsi yako,” mnafanya vyema. 9 Lakini kama mnakuwa na upendeleo kwa watu, mnatenda dhambi, na sheria inawahukumu kuwa ninyi ni wakosaji "
πhivyo usimdharau mtu mmoja na kumweshimu mwingine maana heshima yako kwa huyo itaonekana kuwa si kitu machoni pa Mungu
kwasababu baya moja huharibu mema yote, hivyo kumheshimu mmoja tajiri na kuwadharau wengine maskini ni jambo lisilokuwa na dhawabu mbele za Mungu.
AMHURUMIAYE MASKINI ANA HERI
sasa Biblia inapotaja neno heri huwa na maana ya BARAKA, ikiwa na maana kuwa unapochukua jukumu na tendo la kuwaheshimu masikini ni jambo ambalo linakuletea baraka....
Sasa unaweza kujiuliza, mbona hajasema KUWADHARAU MATAJIRI...???
Hapo jibu ni kwamba Biblia imeweka wazi kwamba matajiri siku zote huheshimiwa sana na watu wenye mwili...kwasababu ya utajiri walionao, na masikini budharauliwa kwasababu ya umaskini wao.
Mithali 14:20 Biblia inasema kuwaπ
bali matajiri wana marafiki wengi.
Sasa hapo amezungumza hali halisi iliyopo katika ulimwengu kuhusu namna ambavyo watu huenenda mbele za maskini na matajiri....lakini kwenye mstari wa 21ndipo akatuambia kuwa hutatakiwi kuwadharua wale ambao wanadharauliwa huko duniani maana ni uvunjivu wa amri ya Mungu hivyo ni dhambi...
πTena hapa jifunze kwamba si kwasababu kitu kinafanywa huko duniani basi inatakiwa na wewe ukifanye..HAPANA...bali wewe fanya kitu sahihi kilichotoka kwenye kinywa cha BWANA wa majieshi...kwasababu neno lake ni kweli, ni hakika, pia ni safi na halitenguliwi wala kuvunjwa na yeyote zaidi ya yote ndiyo taa ya kutuongoza miguu yetu tunapotembea katika maisha yetu ili tusipotee...
"Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. "
"Maneno ya BWANA ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba."
Hivyo mtu wa Mungu....USIMDHARAU MTU YEYOTE
Mungu akubariki sana
Mwl/Ev. Mathayo Daudi Sudai
0744474230/0628187291
Maoni
Chapisha Maoni