MTU MZUSHI MKATAE
MTU MZUSHI MKATAE
Tito 3:10-11
Mtu aliye mzushi, baada ya kumwonya mara ya kwanza na mara ya pili, mkatae; ukijua ya kuwa mtu kama huyo amepotoka, tena atenda dhambi, maana amejihukumu hatia yeye mwenyewe.
Bwana Yesu asifiwe watu wa Mungu...karibu katika ujumbe wa leo ambapo tunangalia kuhusu mtu mzushi na nini Biblia inataka tufanye kwa mzushi...
Mzushi ni I mtu anayependa kusema mambo asiyo ya kweli ili kukosanisha wengine...
👉Mzushi huwa na lengo la kutawanyisha watu wenye umoja
👉Mzushi huwa na lengo la kukufarakanisha na Mungu
👉Mzushi huwa na ajenda ya kupindisha mapenzi ya Mungu kwako..
👉Mzushi huwa haonyeki anapokosea
Sasa hayo yalikuwa ni maneno ya Paulo alipokuwa akizungumza na mwanae wa kiroho yaani Tito ambaye hapa alikuwa ni mtu, kijana ambaye anaanza huduma ( Ministry ) Sasa ndipo Paulo akaanza kumpa maelekezo ya kimungu ya jinsi gani afanye na kuendesha huduma yake ....
Lakini alipofika kwenye kipengele cha wazushi alisema WAONYE MARA YA KWANZA NA MARA YA PILI NA WAIPOKUBALI WAKATAE....
Sasa, ni lazima wewe kama MKRISTO mwaminifu au pengine na wewe ni mtumishi wa Mungu katika huduma fulani...ni lazima ujue kuwa wazushi wapo Wengi sana ndani ya kanisa ..
👉Na hapo Biblia inasema kuhusu Wale ambao wanalitaja jina la Yesu na wao husema Bwana asifiwe, huenda kanisani lakini kumbe ni wazushi...wala si wapagani WASIOMJUA Mungu .
👉Ni lazima ujue kuwa adui mkubwa wa imani yako yupo ndani ya kanisa na si nje ...
👉Sasa ukishagundua kwamba huyo mtu hataki kukiri makosa yake na kurudi na ukamuonya mara ya kwanza hata ya pili na asitake Basi huyo ni mzushi mkatae....
👉Mzushi ni mkristo kabisa na wakati mwingine anaweza kuwa kiongozi wako wa kanisa katika nafasi fulani lakini kumbe ndiye anayeua na kutawanyisha kundi la Mungu
Maana mzushi hufikiri tu namna gani anaweza akawaangusha watu, wakamuasi Mungu kama vile yeye alivyoaasi...
Lakini Kumbuka kwamba UZUSHI ni roho kabisa na ndiyo maana ikimvaa mtu, hata yeye wakati mwingine anaweza asijue anachokifanya, bali huitimiza tu ajenda ya shetani ya kuligawanya kundi la Mungu...
Kimsingi mzushi huwa hafuati utaratibu wa Mungu ndani ya wokovu na ndiyo maana hulitaja jina la Bwana, huingia kanisani lakini si mtu salama kwaajili ya kanisa au kwaajili ya watu wa Mungu ...na ndiyo maana Biblia ikasema jitenge nae....
2 Wathesalonike 3:6
[6]Ndugu, twawaagiza katika jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na kila ndugu aendaye bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
Unaona hapo anasema jitenge na NDUGU.....
👉Neno ndugu linaonyesha kwamba huyo mtu upo naye ndani ya nyumba moja au jamii Moja na jamii hiyo au nyumba hiyo ni KANISA...
👉Kuna watu wapo ndani ya kanisa lakini hawafuati utaratibu na maagizo ya Mungu na wala wakionywa kuacha njia zao hawataki , Basi wewe ni lazima ujue kuwa hao ni wazushi na unapaswa kuwakimbia, au kuwakataa kwasababu waakupotezea Muda tu na kuyamaliza mafuta yako....
Ni lazima ujue kwamba nyakati tulizopo ni nyakati ambazo wa awali watano wenye hekima wanajitenga na wanawali watano wapumbavu ( Mathayo 25 )...
Japo wote ni wanawali ( wapo ndani ya kanisa na wanaliita jina la Yesu ) bali watano kati yao ni wapumbavu na watano wao wana hekima..
Lakini ukisoma Biblia inaonyesha kwamba hawa watano wanatengana katika nyakati hizi za mwisho..
👉Hivyo kuwa makini sana kwenye kipindi hiki maana Shetani amepandikiza roho chafu kwa watu ambao walikuwa wazuri tu lakini Leo hii Wamekuwa ni wazushi...
👉Mzushi ukikaa naye anakuwa anatamani uanguke kwenye dhambi na kuacha wokovu ili pengine Uwe kama yeye maana hata akikutazama anaona kana kwamba unajiona sana...
👉Mzushi hutamani mchungaji ateseke na hata kukata tamaa na anapopitia taabu yeye ndipo hufurahia badala ya Kumuombea ....
Hwa wamejaa ndani ya kanisa na shetani amewaweka Kwa siri kabisa ili kuharibu imani za watu wengine...
Yuda 1:4
[4]Kwa maana kuna watu waliojiingiza kwa siri, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, makafiri, wabadilio neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, nao humkana yeye aliye peke yake Mola, na Bwana wetu Yesu Kristo.
Unaona hapo, anasema Wamejiingiza kwa siri....maana yake unaweza usiwatambue lakini kumbe taratibutaratibu wanaua imani yako, wanaua huduma yako na mwisho wa siku wanalitawanya kanisa .....
Kuwa makini sana...
Na Biblia imetoa kabisa habari kwamba kwa watu hao inapowaonya waziache njia zao mbaya na wao wakakataa Basi WAACHE, maana wamejihukumu wenyewe...na pia hata wakipotea damu yao kwako hidaiwi maana uliwaambia lakini hawakutaka kuacha udhalimu wao....
Ezekieli 33:9
[9]Walakini ukimwonya mtu mbaya kwa sababu ya njia yake, kusudi aiache; wala yeye asiiache; atakufa huyo katika uovu wake, lakini wewe umejiokoa roho yako.
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Barikiwa sana na Bwana.
JibuFuta