JE UNA UPENDO WA KWELI
JE UNA UPENDO WA KWELI ?
Bwana Yesu asifiwe asifiwe watu wa Mungu, Karibuni katika siku nyingine ambapo tutatazama jinsi ambavyo tunatakiwa kuonyesha upendo si kwa Mungu tu bali na kwa watu wingine tunaoishi nao....
Kuna namna ambayo Mungu anauona upendo kama upendo na si kama wanadamu Wengi katika mataifa wanavyotazama ...
Hebu soma hapa👇
Warumi 13:8-10
[8]Msiwiwe na mtu cho chote, isipokuwa kupendana; kwa maana ampendaye mwenzake ameitimiza sheria.
[9]Maana kule kusema, Usizini, Usiue, Usiibe, Usitamani; na ikiwapo amri nyingine yo yote, inajumlishwa katika neno hili, ya kwamba, Mpende jirani yako kama nafsi yako.
[10]Pendo halimfanyii jirani neno baya; basi pendo ndilo utimilifu wa sheria.
Anaannza kwa kusema MSIWIWE
👉Sasa kuwiwa ni kama kudaiwa kitu, au kuwa na deni na mtu fulani...
👉Anasema msiwiwe na mtu chochote isipokuwa kupenda....
Hapa ni lazima ujue kuwa sheria ya Mungu inamtaka kila mtu apendane au ampende mwenzake au ndugu yake...
NA kwa kufanya hivyo maana yake unakuwa umetimiza sheria zote...
Kivipi?
Ni hivi...Mungu ametoa makatazo au sheria nyingi juu ya mambo ambayo mtu hatakiwi kuyafanya..kwa mfano usiibe, usizini, usije n.k
Lakini sasa ukiziangalia hizo zote utagundua zinamhusu mtendaji na mtendwaji .....
👉Ukimfanyia mbaya unakuwa umemfanya yeye kuwa sehemu mbaya ambayo hakustahili kuwa nayo...Kwahiyo Hili linaonekana kana kwamba unadeni na mtu fulani....
👉Au unapomkosesha mtu, au unapokosana na mtu, unakuwa hujatimiza sheria za Mungu kwasababu Kuna mtu ambaye unadeni au tatizo naye....
NA ndiyo maana hata Yesu alisema kama Kuna mtu umekosana naye Basi hata sadaka usitoe mpaka upatane naye ndipo uje utoe sadaka..hii ni kwasababu unapokuwa umekosana na mtu maana yake unadeni naye na hujatimiza sheria za Mungu hivyo Mungu haipokei sadaka yako..
Mithali 15:8
[8]Sadaka ya mtu mbaya ni chukizo kwa BWANA;
Bali maombi ya mtu mnyofu ni furaha yake.
Kwahiyo ni lazima uhakikishi hakuna mtu anayekuwia kitu chochote ili kisiwepo kikwazo cha wewe kusogea mbele za Mungu...
Kwahiyo Mungu kusema au kutoa amri zile zote alikuwa anahitaji au anazungumza kuhusu UPENDO
👉Ukimpenda mtu hatazini naye kwasababu hupendi apotee na ndiyo maana Mungu akasema USIZINI
👉Ukimpenda mtu hutaweza kumwibia kitu ukijua kabisa kwamba utamrudisha nyuma katika maendeleo yake na ndiyo maana Mungu akasema USIIBE..
👉Ukimpenda mtu hutamuua ukijua kabisa kumuua ni kukatisha kwa ghafla na kumkosesha kile alichokuwa amepangiwa na Mungu kukiishi au kukipata na ndiyo maana Mungu akasema USIUE....
👉Ukimpenda Mungu, hutaweza kumchanganya yeye na miungu mingine na ndiyo maana akasema ..USIWE NA MIUNGU MINGINE
👉KUMPENDA JIRANI KAMA NAFSI YAKO ni kwamba huwezi kumfanyia kitu ambacho kitamletea madhara ya kumuangamiza au hlkumtenga mbali na dhambi ..
NA ndiyo maana kabla haujaenda kuzini na binti/ au kijana yeyote ni lazima ujue unachoenda kukifanya ni kumkosea Mungu lakini pia ni kumharibia mwenzako maisha Kwahiyo tafsiri ya hapo ni kwamba humpendi ,..HUNA UPENDO..
🤔Kwahiyo amri za Mungu kwaujumla wake zipo ndani ya neno UPENDO ...Kumpenda Mungu na wenzetu pia..
KIONGOZI
NA mstari wa Kumi ndipo anapoweka vizuri kwa kusema PENDO HALIMFANYII JIRANI BAYA..
Maana yake Ukimpenda mtu...
👉Hutamdhuru
👉Hutamuangamiza
👉Hutamtenga na Mungu
👉Hutafurahia kuumia kwake
👉Utapenda afanikiwe
👉Hutaruhusu wewe kuwa sababu ya anguko lake kwa kujua kabisa..
Yaani hutamfanyia ubaya wowote...
Ukiona Kuna mtu anasema anakupenda lakini anakufanyia ubaya, au anapenda uumie au anafanyika sababu ya wewe kuwa mbali na Mungu basi jua kabisa kwamba huyo anakupenda lakini upendo wake una unafki ndani yake ...
Kwasababu hiyo upendo wa namna hiyo hauwezi Kutimiza sheria ya Mungu...
Warumi 12:9-10
[9]Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema.
[10]Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
Unaona hapo kumbe upendo unaweza kuwa na unafiki...
👉Ukiona una upendo wa unafiki Basi hata usijaribu kumwambia mtu kuwa unampenda, kwasababu atajua Ana rafiki na hata pengine kukuamini sana lakini kumbe wewe mwenyewe huelewi maana ya Upendo ....
NA hapa ni lazima kila mtu aukubali ukweli huu kwamba Kuna wakati Ambao wakristo huwa katika mahusiano ya kati ya kijana na binti wakidai wataoana, na kila mtu utakuta anamwambia mwenzake I kuwa anampenda na wanaishi tu...
Kimsingi hakuna tatizo ...
Lakini tatizo huanza pale ambapo hawa watu wataanza kuyaishi maisha nyeti kabla ya wakati wake nikiwa na maana kuwa wataanza kufanya tendo la ndoa kabla ya ndoa...na hapo ndipo maana ya UPENDO anaoutaka Mungu unakuwa umevunjika..
I abaki kudanganyana tu kati ya Hao watu na kujifariji....
👉Ukifikia hatua hiyo Basi jua ni upendo wa kawaida tu kama watu wa Mataifa WASIOMJUA Mungu wanavyopendana wakiamini hiyo ndiyo maana ya upendo...kumbe wamepofushwa macho na Ibilisi baba wa watendao uovu ( Yohana 8: 44 )
👉Kwasababu upendo wa kimungu huwa haumfanyii jirani, ndugu au rafiki ubaya ..Sasa kama unafanya uasherati na mtu huoni kwamba Unamfanya unamtenda ubaya mwenzako ...
NA ndiyo maana hata Kumpenda Mungu kunakamilishwa na wewe Kumpenda kwanza jirani yako( kutomfanyia ubaya kwa kuvunja sheria ya Mungu ) ...kwasababu Kumpenda Mungu maana yake no kushika sheria zake ...
NA wala hatutakiwi kumwambia Mungu kwa vinywa vyetu kwamba tunampenda bali tujipime wenyewe kwa kujiangali kama kweli tumezishikana kuziishi amri zake..???
Yohana 14:21
[21]Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Kwahiyo ukimpenda mtu na bila kuwa na unafiki yani kutokumfanyia ubaya ni ishara pekee kwamba tumezishika amri za Mungu na kwasababu hiyo Basi tunampenda Mungu...
Hebu soma hapa👇
1 Yohana 4:20-21
[20]Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.
[21]Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
HEBU JITAFAKARI, JE UNA UPENDO WA KWELI ???
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni