JAMBO LA KUFANYA UNAPOUGUNDUA UZURI WAKO
JAMBO LA KUFANYA UNAPOUGUNDUA UZURI WAKO
Bwana Yesu asifiwe sana watu wa Mungu, mabinti ndani ya Kristo..
nomba leo tujifunze jambo moja la singi sana kwaajili ya afya yako ya kiroho, kimwili na ndoa yako pia.
unajua kila mtu huwa ana desturi ya kujiona na kujijua pale anapojitazama au kuambiwa na mtu kuhusu uzuri alionao.....
👉mabinti wengi huujua uzuri wao pale wanapojitazama kupitia vioo n.k
👉lakini katika kuujua uzuri wake binti huyo hujenga kitu kwenye fikra yake cha kumuhusu yeye..
na wengine huanza kuishi na kufanya mambo sawasawa na vile alivyojiona kwenye kioo.
👉wengine huanza kufanya mambo mabaya wakiutazama uzuri au urembo wao kama kigezo cha kufanya hivyo
👉Wengine huanza kujiingiza kwenye mahusiano kwa kigezo cha uzuri wao
👉wengine huanza kuona kwamba wao ni bora kuliko wengine
👉wengine huanza kufikiri wanauwezo wa kuwakamata au kuwateka wanaume kadiri wapendavyo
👉na wengine huanza kufikiri wanaweza kuwa na mwanaume yeyote atakayemuhitaji
soma hapa
Mithali 31:30
Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye Bwana, ndiye atakayesifiwa.
unaona hapo Biblia inasema UZURI HUDANGANYA ikiwa na maana kuutegemea uzuri wako kama silaha ya kufanya uamuzi, ni kosa kubwa maana utakuwa unajidanganya au unadanganywa kwa uzuri wako...
JE NINI UFANYE UNAPOUONA UZURI WAKO
Kwanza ni lazima ujue kila mwanamke anao uzuri wake mwenyewe wa kipekee kabisa kuliko wengine
👉sasa unapougundua uzuri wako au urembo wako..basi usikimbilie kufanya kile ambacho wazuri wengine hukifanya
👉kama wengine uzuri wao unawapeleka kwenye ngono zisizo na msingi, wewe usifanye hivyo
👉kama wengine hutumia uzuri wao kwa majivuno na kujionyesha kwa wanaume, basi wewe usifanye
👉kama wengine hutiwa kiburi na uzuri wao, basi wewe usiwafuate...
lakini unachotakiwa kufanya ni KUUTUNZA UZURI WAKO KWA WAKATI SAHIHI....
👉UKIUGUNDUA uzuri wako kwa wakati huo basi usiutumie kwa wakati huohuo bali uache wakati sahihi na kisha utaona faida ya huo uzuri wako..
👉kwasababu kuna wakati wa ndoa utafika ambapo wengine watakuwa wameshadanganywa na kujiingiza kwenye mambo mabaya na baade wanaanza kuhangaikia ndoa kuliko chochote hata wakadhania wamelaaniwa....
lakini wewe wakati wako wa ndoa, unapowadia unakuwa tayari uzuri au urembo sahihi kwaajili ya ndoa yako/mume wako...
jambo la msingi kujua ni kwamba...UZURI HUA HAUPOTEI MPAKA AWEPO WA KUUPOTEZA....
👉Kizuri ulichonacho ukikitunza, hakitaharibika kamwe mpaka utakapokitumia
👉hata wewe binti unayehitaji kuingia kwenye ndoa nzuri, usiruhusu mwanaume ambaye si mumeo akautumia uzuri na urembo wako...kwasababu urembo wako ni kwajili ya mume wako na si kila mwanaume...
👉usikubari kuchoshwa na wanaume wa ajabu kabla ya kuingia kwenye ndoa yako
👉usiruhusu kuishi kwenye maisha ya kesho kabla ya kesho yenyewe huku ukiwa na mtu ambaye si muhusika/mwenza wako
👉kataa kuingia kwenye ndoa na majeraha yanayoletwa kwa kuutazama uzuri wako wa leo na hata ukakudanganya.....
👉Ni lazima ujue kuwa shetani huwaletea mabinti wengi wanaume kwa makusudi ya kuwaondolea uzuri wao tu na si kuwaoa..na hufanya hivyo ili kupoteza msingi na uzuri wa mwanamke huyo katika wakati sahihi utakapowadia....na ndiyo maana wengi ukiwakuta utasikia wanajuta tu kwasababu ya wanaume ambao waliwachezea wakidhani watawaoa kumbe walikuwa ni maajenti kabisa wa kuondoa kibali kwa mwanamke...(AMKA)
UKWELI NI HUU....Mwanamke mwenye uzuri sahihi si yule anayeutumia uzuri wake kwasababu tu ni mzuri bali ni yule ambaye akiisha kuujua uzuri wake basi atauhifadhi uzuri huo kwaajili ya matumizi katika wakati sahihi...
Mungu akubariki sana
Laddies in Christ
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni