ASIYEFAA USIMPE KITAKATIFU ATAKUUMIZA
ASIYEFAA USIMPE KITAKATIFU ATAKUUMIZA
Mathayo 7:6
[6]Msiwape mbwa kilicho kitakatifu, wala msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe, wasije wakazikanyaga chini ya miguu yao, wakageuka na kuwararua.
Bwana Yesu asifiwe sana watu wa Mungu...
Leo ni siku nyingine karibu tujifunze kuhusu neno la ujumbe wa Leo ...MATHAYO 7:6
Sasa hapo ukitazama ni kwamba Yesu alitoa kama agizo la moja kwa moja kwamba watu wake wasiwape mbwa kilicho kitakatifu..
Wala wasitupe lulu ( vitu vya thamani ) mbele ya nguruwe..
NA hapo mwisho akatoa madhara na sababu kwanini usifanye hivyo...
MBWA
Hapa Biblia imetumia neno mbwa si kwa maana ya mbwa mnyama bali ..inataka tuzitafakari sifa za mbwa kisha tuone watu wenye sifa hizo na hao ndio ambao hatutakiwi kuwapa kitakatifu...
Sifa za mbwa ni kama vile kurarua, kuyarudia matapishi, kuumiza pale anapokuuma hata kukusababishia kifo n.k
NGURUWE
Lakini pia nguruwe ametumika kuonyesha picha ya tabia ambazo watu wanazo na sisi hatutakiwi kuwapa vitakatifu...
Sifa za nguruwe ni kama vile kuishi pachafu, anapenda sehemu za matope, hata chakula chake anaweza kukilia kwenye hayo hayo matope yaani hajali kitu chochote....hajui kwamba hapo ni pachafu yeye hufurahia sana mazingira hayo ...
KITAKATIFU /LULU
LULU ni vitu VYA thamani ambavyo mara nyingi watu huvivaa kama vitu VYA thamani sana.
Kimsingi Lulu ni madini fulani ya thamani sana..ambayo hayachimbwi kutoka ardhini kama madini mengine yachimbwavyo bali asili yake ni baharini…Madini haya yanatengenezwa ndani ya mwili wa samaki, wanaojulikana kama OYSTER
Sasa hayo madini yanayoitwa LULU yanaanza kujitengeneza kama chembe ndogo ya mchanga, tumboni mwa hao samaki, na kwa kadiri muda unavyozidi kuendelea..yanaongezeka ukubwa kidogo kidogo na hata kufikia ukubwa wa kama hizi gololi wanazochezea watoto wadogo..kwa jinsi inavyokuwa kubwa ndivyo thamani yake inavyozidi kuongezeka. Watu wanaokwenda kuyatafuta madini hayo baharini wanatumia gharama nyingi na muda mwingi na hatari nyingi..kwasababu inawagharimu waende mbali kwenye vilindi vya maji na wazame chini mpaka kwenye sakafu ya bahari na kuanza kuangalia angali huku na huko kama mtoto anayetafuta hela aliyoiangusha njiani..inawaachua hata siku nzima kukaa chini ya maji,..
🤔 hiyo inaweza kwenda kwa miezi kadhaa, Na kwa tabu nyingi wakibahatika kuwapata hao samaki wanawachukua na kwenda kuwapasua na kutoa hayo madini..
👉Sasa jiulize madini ya thamani namna hii uyaweke mbele ya nguruwe ambaye yeye mara zote Utamkuta kwenye matope ..unategemea nini kitatokea ..ni kwamba utaikuta hiyo lulu yako haieleweki, imechafuka kiasi kwamba unaweza hata usiione tena .....
Sasa Biblia inatuonya tusiwape mbwa vitu vitakatifu yaani vitu VYA thamani ambavyo tunavyo...
Sasa ukitazama hapo ni kwamba hao wanyama wametumia kuwaeleza WATU WASIOFAA kwako kulingana na tabia zao...
KITAKATIFU kinaweza kuwa ni siri ya kanisa ...unapoichukua siri ya kanisa na ukaipeleka kwa watu wasiohusika na WASIOFAA Basi Kuna uwezekano mkubwa wa hao hao watu kugeuka fimbo ya kulipiga kanisa
Si hivyo tu, ni lazima ujue kuwa unapokuwa na jambo fulani la maendeleo hata Kwenye maisha yako ya kila siku Basi kuwa makini sana na Aina ya mtu unayemwambia ...
Kuna mtu ukimpa siri Basi Jiandae kuikuta kwa wengine maana atakutangaza mpaka utashangaa..kumbe wewe ulimshirikisha kwa lengo la kupata msaada...
Basi kwa namna hiyo ni lazima ujifunze kwamba kabla ya kuwashirikisha watu mambo yako ili wakusaidie Basi Hakikisha hao/ huyo mtu anasifa ya kwanza kuu ambayo ni HOFU YA MUNGU...si kwasababu huenda kanisani ukafikiri ana hofu ya Mungu ..HAPANA..
Kama mtu hana hofu ya Mungu hatoweza kuvumilia ni lazima ataipeleka kwa mwingine, hata kama siyo siku hiyo hiyo Ila itakwenda tu ...
👉Tena mwingine ukimwambia siri au udhaifu wako inageuka fimbo na kitu cha kukutawala ..utashangaa anakutisha na kukufanyia chochote akijua huna cha kumfanya kwasababu anajua udhaifu wako mwingi tu ...
👉Na ndiyo maana hata Leo utaona mtu ameshikiria ushahidi wa video au picha au sauti ya mtu fulani na anamtishia kwasababu tu anajua udhaifu wake....
👉Siri yako( kitakatifu ) kikifika sehemu ambayo si sahihi Basi jua kabisa kwamba kitaharibika lakini pia na wewe mwenyewe utaumizwa...NDIVYO ALIVYOSEMA YESU..kwamba wakishaharibu warakugeukia na kukurarua..🤔
Hata Kwenye maendeleo yako, usiwe mwepesi sana kumwambia kila mtu ...
👉Pia hata Yale maisha Yako ya dhambi ambayo uliyaishi kale ..pia usiwe mwepesi kuwaambia watu maana wapo wapumbavu kati ya hao ..WATAKUSHAMBULIA NA KUKUUMIZA
NA ndiyo maana hata Paulo alilisema hilo wakati anaongea na Timotheo kwahabari ya kile cha thamani alichonacho na Aina ya watu ambao anatakiwa kuwaamini na kuwakabidhi...alisema wawe WAAMINIFU
2 Timotheo 2:2
[2]Na mambo yale uliyoyasikia kwangu mbele ya mashahidi wengi, hayo uwakabidhi watu waaminifu watakaofaa kuwafundisha na wengine.
Hakusema awakabidhi watu wote, bali WAAMINIFU akijua kabisa mikono isiyofaa itaua na si kingine ....
HIVYO, USIMPE KITU CHA THAMNI MTU ASIYEFAA ..ATAKURARUA NA KUKUUMIZA ...KAMA UNAHITAJI MSAADA KUTOKA KWA MTU BASI HAKIKISHA UNAMPATA MWENYE HOFU YA MUNGU ...UKIMKOSA BASI KAA NAYO MWENYEWE HIYO SIRI/ THAMANI ....
Mungu akubariki sana
Taifa Teule Ministry
Mwl /Ev Mathayo Sudai
0744474230 /0628187291
Maoni
Chapisha Maoni