EPUKA KUWA MKOSESHAJI, UTAANGAMIZWA...


 EPUKA KUWA MKOSESHAJI, UTAANGAMIZWA...

BWANA Yesu asifiwe watu wa Mungu, leo ni siku nyingine ambapo tutaangalia somo letu zuri la kuhusu kumkosesha Mtu mwingine....

soma hapa    

        MWISHO WA SOMO KUNA USHUHUDA MZURI KWA AJILI YAKO, karibu sana

Mathayo 18:7 

 Ole ni wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana budi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletaye jambo la kukosesha!


    KUKOSESHA

Huku kunatoa tafsiri ya kufanya jambo ambalo litafanyika kikwazo kwa mtu mwingine katika kufikia pale ambapo anatakiwa kufika sawasawa na mapenzi ya Mungu. 

na jambo pekee ambalo pengine linaweza kumfanya mtu mwingine kushindwa kufika pale anapotakiwa kufika ni DHAMBI

kumbe ukifanyika sababu ya mtu mwingine kufanya dhambi maana yake UNAMKOSESHA mtu huyo kufanya mapenzi ya MUNGU.

Au unapomzuia mtu asifanye mapenzi ya Mungu, maana yake unamkosesha....kwamfano mchungaji au mtu yeyote yule akiwa anafanya huduma yake sawasawa na agizo la Mungu halafu wewe ukaamsha vikwazo juu yake na kumfanya asifanye mapenzi ya Mungu, maana yake wewe ni mkoseshaji...

lakini Biblia inaweka wazi kwamba mpingamizi wa kwanza au mkoseshaji wa kwanza wa mapenzi ya MUNGU ni ULIMWENGU. Ikiwa na maana kuwa watu wa ulimwengu huu na mfumo wa ulimwengu huu (World) ndiyo huwa vinakosesha ajenda ya Mungu ndani ya mtu..

     sasa kama mtu wa MUNGU ni lazima ujue kuwa katika kila kitu cha kimungu ambacho utakifanya ni lazima vikwazo (vikoseshaji) viamke kwako ili kukuzuia na kukukosesha ...

na vitu hivi huwa na majibu ya aina mbili mbele za mtu👇


👉kumuagusha (kumkosesha) na kuanguka dhambini

👉kumuongeza kiwango (Elevating to higher dimension of the spirit)


Na matokeo hayo yote yanategemea sana wewe mwenyewe na mahusiao yako na Mungu..

lakini katika yote hayo kuinuka na kuanguka, bado Biblia imesema ole wake anayeleta vikwazo hivyo kwako...ulimwengu au mifumo ya dunia hii itaangamizwa kwasababu ya kwenda kinyume na mapenzi ya Mungu na kuwakosesha watu wa Mungu..

hata wewe ni lazima ujue kuwa ukifanyika kikwazo na sababu ya mtu mwingine kumkosea Mungu au kutenda dhambi basi OLE WAKO...


Na Biblia inaposema OLE hubeba maana kwamba nyuma yake kuna laana na adhabu kutoka kwa MUNGU mwenyewe....sasa kwanini uangamie kwasababu ya kumkosesha mtu mwingine?


NI HIVI

👉Unapomkuta binti kasimama na anamtumikia Mungu halafu ukamtoa kwenye njia hiyo kwa kumuingiza kwenye uasherati basi UMEMKOSESHA

👉Unapomkuta mtu anafanya huduma ya kiroho na ukampinga na kumuonea kwasababu ya madaraka au nguvu uliyonayo, basi wewe ni mkoseshaji

👉unapokuta mtu anahubiri injili na wewe ukamzuia kwa kuinua vikwazo basi wewe ni mkoseshaji

👉unapomkuta mtu wa MUNGU ana huduma fulani na wewe ukamuinulia kashifa mbaya za uongo ili kumchafua, jua kabisa unaizuia injili kwenda kwa watu, kwa hiyo wewe ni mkoseshaji

namifano mingi ifananayo na hiyo..inamuonyesha MKOSESHAJI ALIVYO.


Unajua kuna watu wengi sana ambao walitakiwa kuingia mbinguni kwa namna walivyokuwa, lakini kwasababu wakoseshaji waliamka, waliwakosesha na kuwafanya kufa dhambini na mpaka leo hii wapo JEHANAMU.


USHUHUDA

KUNA MAMA AMBAYE ALIKUWA NA MUME PAMOJA NA WATOTO WAKE, LAKINI ILE FAMILIA ILIKUWA HAIMJUI MUNGU, NA WANAISHI KWA MAMBO YA KIMILA KABISA, KWENDA KWA WAGANGA NA MAMBO KAMA HAYO...SASA SIKU MOJA MAMA YULE ALISIKIA INJILI NA AKATAKA KUOKOKA LAKINI MUME WAKE AKAMKATAZA KABISA KWA UKALI...BAADAE KIDOGO YULE MAMA AKAFA AKIWA NA NIA YA KUOKOKA LAKINI HAKUOKOKA NA AKAFIA DHAMBINI KULEKULE...LAKINI BAADAE YULE BABA AKAJA KUSIKIA INJILI NA YEYE... AKAOKOKA. NA HATA ALIPOKUFA NA YEYE ALIKUWA YUPO KWENYE WOKOVU...😢😢...SASA MOJA YA WATOTO WAO NAYE ALIKUJA KUOKOKA NA KUTOKA KABISA KWENYE MAMBO YALE YA KICHAWI NA MILA MBAYA NA BAADAYE AKAJA KUWA MUHUBIRI WA INJILI ...na ndiye aliyetupa huo ushuhuda ......


Hebu jaribu kutazama hali ya mama yule, yupo Jehanam ya moto... halafu yule mkoseshaji akaja kukubali kitu ambacho alimkataza mkewe kwa kumpiga pengiene..

sasa unaweza kujiuliza na ukaumia sana lakini jambo lilopo ni kwamba HATA SHETANI ANAWEZA KUKUTUMIA KWAAJILI YA KUWAKOSESHA WENGINE...hivyo ni lazima uwe makini sana jilinde na uwalinde wengine..

unaposhindwa kuwa mwaminifu kwa Mungu na ukajikuta umemtamani binti wawatu aliyeokoka..utashangaa shetani anakuendesha, unamtongoza binti na baadae unamuangusha kwenye uasherati.. akifa jua kabisa kwamba wewe ndiyo sababu ya huyo binti kwenda JEHANAMU...Kwasababu kuna mabinti wameokoka lakini bado ni dhaifu au wana udhaifu fulani, sasa wewe kama ni mtu wa Mungu ni lazima uwalinde na siyo kuwaharibu....usiwe mkoseshaji bali kuwa mlinzi....

na ndiyo maana hata Yesu alisema mkoseshaji ni heri angefungiwa jiwe na kutupwa majini kuliko ile adhabu ambayo ataipata kwa kuwakosesha watumishi wa Mungu, au watu wa Mungu 


Mathayo 18:6

“Yeyote atakayemkosesha mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini, ingekuwa afadhali afungwe shingoni jiwe kubwa la kusagia na kuzamishwa kwenye kilindi cha bahari.


                   EPUKA KUWA MKOSESHAJI....


Mungu akubariki sana

 

Taifa Teule Ministry

Mwl/Ev.Mathayo Daudi Sudai

0744474230/0628187291

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

JE NI DHAMBI KUSHEREHEKEA VALENTINE'S DAY?

MAANDALIO YA MOYO NI YA MWANADAMU

BWANA TUONGEZEE IMANI